Dkt. Slaa ulisahau nini huko CHADEMA?

Dkt. Slaa ulisahau nini huko CHADEMA?

Nafasi ya balozi haoimo kwenye chama, balozi ni mtendaji wa serikali na huteuliwa na rais ambaye ni mtendaji wa serikali. Balozi anapokuwa kwenye nchi anayotuwakilisha hafanyi mambo ya siasa, isipokuwa balozi wa China ambao huwa wanakawaida ya kutotii sheria za nchi husika, kwahiyo ujue hskuenda kuiwakilisha CCM, alikwenda kuiwakilisha Tanzania.
Niambie balozi mmoja tu wa TZ ambaye si CCM
 
Once Chadema always Chadema. Ile imani ya Chadema ni kama umelogwa vile.

Hata akina Joshua Nasari na akina Waitara ni basi tu wale ni Chadema watupu
Kwa hiyo wote hawa walinunuliwa na hela ya Dr Bashiru Kakurwa?
 
Utachanganyikiwa mshikiwa akili kama wewe! Ulihoji Lowasa anafanya nini Chadema? Sumaye? Kuna CCM kuliko hao? Mlibeba hadi wahuni ambao huko CCM wenyewe waliowaona ni takataka lakini mlishangilia leo mnajifanya mna uchungu na Chadema kuliko Dr Slaa!

Ninavyoelewa kuna movement inaendelea kukusanya nguvu ya kudai katiba na Dr Slaa ni moja ya silaha. Wataibuka wengi ambao hata si Chadema lakini kwa kazi hiyo tu. Kwenye katiba ni rahisi Dr Slaa kusimama na Chadema kuliko upande mwingine.

Kwenye katiba hata mimi nitasimama na Chadema na sina kadi ya chama chochote! Ni issue ya kupigania future ya Taifa langu sio uvyama wenu.

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
Tupo wengi wa aina Yako tunaounganishwa na course ya KATIBA mpya.

CDM hawana sababu ya kupingana na SLAA Kwa sasa, sababu ana mchango mkubwa ktk move ya Katiba mpya.
 
Suala kubwa ninaloliona hapa si Dr. Slaa kupanda kwenye jukwaa la CHADEMA bali suala kubwa ni jee CHADEMA wamejifunza nini kutoka na matukio ya nyuma ya wanasiasa wanahamahama?

Ushauri wa bure kwa CHADEMA wawe makini sana kwa wanasiasa wanahamahama kama Dr. Suala. Wawe chini ya ungalizi kwa angalau miaka mitano kabla hawajakabidhiwa cheo chochcote hata kama ni ujumbe wa tawi.
 
Hakuna chama au Nchi inayoweza kuzuia mapandikizi,

Kinachofanyika ni kuwa makini na kuishi nao Kwa AKILI.

Kusimama ktk misingi.
 
Kwani kuna tatizo yeye kurudi CDM? ..... hebu vijana tupunguze upuuzi jama!!!
 
Nafasi ya balozi haoimo kwenye chama, balozi ni mtendaji wa serikali na huteuliwa na rais ambaye ni mtendaji wa serikali. Balozi anapokuwa kwenye nchi anayotuwakilisha hafanyi mambo ya siasa, isipokuwa balozi wa China ambao huwa wanakawaida ya kutotii sheria za nchi husika, kwahiyo ujue hskuenda kuiwakilisha CCM, alikwenda kuiwakilisha Tanzania.
Ha hebu ujidhihirishe we ni CDM uone kama utapewa huo ubalozi. Ubalozi = Ukada!
 
Et alidai ndani ya CDM kulokuwa na watekaji,alikuwa rafiki wa Jiwe mkubwa,Mama kampiga chini na yeye kajiongeza anawaset CDM.Njaa mbaya sana.
Ngoja nione kama Lisu atasimama Jukwaa Moja na huyu Babu Mihogo.
 
Chadema mbona mnawachukua hadi Hawa mnaowaita wasaliti? Au huyu sio msaliti? Kokolo 🤪🤪
 
View attachment 2533331
View attachment 2533342
Huyu mzee kweli ni oppurtunist.
Alishachaguliwa kuwa Balozi wetu huko Canada Sweden, na alichaguliwa na serikali ya CCM.
Sasa tunamuona tena, mdomo juu, kakimbilia CHADEMA na magwanda yake.
Kiapo chake cha utii kwa serikali ya CCM kiliisha lini?

Na kasahau kitu gani huko CHADEMA!
Mapambo ya kivita yanakiasi chake yakizidi imatafsiriwa ni uoga ndyo huyo mzee alipoona wenzake wapo katikati ya mapambano akasepa kwa uoga na tamaa hafai.
 
Back
Top Bottom