Dkt. Stergomena ashiriki Mkutano wa Tume ya Kudumu ya Pamoja Baina ya Tanzania na Msumbiji

Dkt. Stergomena ashiriki Mkutano wa Tume ya Kudumu ya Pamoja Baina ya Tanzania na Msumbiji

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Stergomena Lawrence Tax (Mb) ameshiriki Mkutano wa Nne wa Tume ya Kudumu ya pamoja ya Ushirikiano katika msuala ya Ulinzi na Usalama (JPCDS) baina ya Tanzania na Msumbiji uliofanyika katika Ukumbi wa Joachim Chisano, Maputo nchini Msumbiji, Waziri akiwa Mwenyekiti Mwenza wa Waziri wa Ulinzi wa Msumbiji, Cristovao Chume.
1eb41836-a5a8-4e25-92f1-0c02ca1c8bfe.jpg


Mkutano huu unafanyika kwa mara ya nne sasa, Mkutano wa kwanza ulifanyika Dar es Salaam, Tanzania tarehe 04 - 06 Februari, 2011 ambapo Tume hii ilianzishwa rasmi.

Mkutano huo umefanyika kwa ngazi tatu, ambapo ulianza kwa kutanguliwa na ngazi ya wataalamu, ukifuatiwa na kikao ngazi ya Makatibu Wakuu na kuhitimishwa na Mkutano wa mawairi wenye dhamana ya masuala ya ulinzi na Usalama wa mataifa haya mawili.

Pamoja na mambo mengine vikao vya ngazi zote vilijadili ushirikiano kuhusu masuala ya kiulinzi, na hatimaye kutoa fursa kwa Mawaziri hawa wawili, kusaini mikataba itakayowezesha kutekelezwa kwa Hati ya Makubaliano kuhusu ushirikiano kupitia sekta ya Ulinzi na usalama, uliosainiwa kwa pamoja tarehe 21 Septemba, 2022 na Mawaziri wa pande zote mbili.
0208e1dd-e918-43db-b34a-58d21d00159a.jpg

Utiaji saini huo, ulishuhudiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan na mwenzake Rais wa Msumbiji, Mheshimiwa Filipe Jacinto Nyusi, wakati wa ziara ya kikazi ya siku tatu, aliyoifanya Rais Samia nchini Msumbiji hivi karibuni.

Mbali na Dkt. Stergomena, ujumbe wa Tanzania ulimjumuisha pia, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makaz, Mheshimiwa Angelina Sylvester Lubala Mabula, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe, viongozi wandamizi wakuu kutoka vyombo vya ulinzi na usalama kutoka mataifa yote mawili.

32ea6b6e-62d5-41bb-8c78-5aba1c9742c2.jpg
 
Katibu mkuu Faraji K. Mnyepe akizungumza katika kikao hicho cha pamoja kuhusu ulinzi na usalama

Mozambique and Tanzania discuss transnational defense



Mozambique and Tanzania seek strategies to combat crimes related to the border connection, trafficking in persons and goods and other transnational crimes, including terrorism.

For analyst Wilker Dias, the resumption of meetings of the Permanent Joint Commission on Defense and Security is due to the fact that the countries in the region have become aware of the challenges faced in the pursuit of development goals in Southern Africa
Source : Voa Português
 
Back
Top Bottom