LGE2024 Dkt. Stergomena Tax: Msiridhike na shamrashamra za Kampeni na mafuriko ya Mikutano, kapigeni kura

LGE2024 Dkt. Stergomena Tax: Msiridhike na shamrashamra za Kampeni na mafuriko ya Mikutano, kapigeni kura

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

BigTall

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
525
Reaction score
1,257
WhatsApp Image 2024-11-26 at 09.22.08_507272f5.jpg

WhatsApp Image 2024-11-26 at 09.22.07_ce7bb7a7.jpg
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Stergomena Lawrence Tax (Mb), tarehe 25 Novemba 2024, ameshiriki Kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya Magu, kwa kuwanadi na kuwaombea kura Wagombea wa nafasi za Wenyeviti wa Vitongoji, Mitaa, pamoja na Wenyeviti wa Vijiji kupitia Chama hicho katika Kata za Kandawe, Nkungulu pamoja na Kata ya Ng’haya katika vijiji vya Ihimbili, Nhobola na Bugatu.

Akiongea katika kuwanadi wagombea hao wa chama cha Mapinduzi,Dkt. Stergomena Tax, amewaomba na kuwakumbusha wananchi umuhimu wa kuwachagua Wagombea wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ili kiendelee kushika dola na kuwaletea maendeleo.

Akifafanua zaidi, Dkt. Tax amekumbusha kazi kubwa na nzuri inayofanywa na serikali ya Chama cha Mapinduzi, kupitia kwa Mwenyekiti wake Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika nyanja mbalimbali ikiwemo ujenzi wa miundombinu, Ujenzi wa vituo vya Afya, Ujenzi wa vyumba vya madarasa na Miradi mingine mikubwa ya Kimkakati ni uthibitisho tosha kwamba Chama cha Mapinduzi ndicho Chama pekee kinachoweza kuwaletea maendeleo Wananchi.

Hata hivyo, Dkt. Stergomena Tax amewakumbusha Wananchi wa Kata za Kandawe, Nkungulu pamoja na Ng’haya kutokuridhika na shamrashamra za Kampeni na Mikutano kufurika watu, bali kila mmoja anapaswa kuhakikisha anakwenda kupiga kura tarehe 27 Novemba 2024 na amewakumbusha kuwa, hakuna Mgombea atakayepita bila kupingwa bali kura nyingi za Mgombea ndizo zitakazompatia Ushindi wa mtaa, kitongoji, kijiji au kata.
WhatsApp Image 2024-11-26 at 09.22.07_eec34dfd.jpg

WhatsApp Image 2024-11-26 at 09.22.12_fc90367f.jpg
 
Hizi kampeni za CCM zinaonyesha jinsi hii nchi waliyoitawala kwa miaka 60 ilivyo maskini. Angalia wananchi walipokaa, mavazi yao, majengo, takataka, sura zao wengine zimekosa nuru sababu ya kutopata chakula cha kutosha.

Mazingira haya ni ushahidi kwamba CCM hawajali wananchi hata wanaCCM wa chini bali wanajali viongozi wao tu.
 
Back
Top Bottom