Dkt. Sulle: Mwinyi kuitwa "Mzee Ruksa" ilitokana na vurugu bucha la nguruwe Tandale 1993

Ni kweli alichosema, nikiikumbuja Ile hutuba huwa nacheka, kwani Mwinyi alifoka kweli na jinsi alivyokuwa akitamka 'ruksaa', ilifurahisha!
 
Huyo jamaa huwa ana'arrogant yakuhisi he is master of all
ni mbishi balaa kwenye mambo ya dini, kwanza huo udokta kaupata chuo gani? Huo udokta utakuwa wa mchongo tu. Tuheshimu title za taaluma zilozosomewa
 
ni mbishi balaa kwenye mambo ya dini, kwanza huo udokta kaupata chuo gani? Huo udokta utakuwa wa mchongo tu. Tuheshimu title za taaluma zilozosomewa
Kuna siku anaelezea jambo alikuwa mahala kwamba ukirusha jiwe sehemu hiyo halidondoki..
Sasa hiyo mechaniam ya kisayansi yeye anasema ni allah quran.. alafu kashupaza shingo
 
Neno ruska Halikuanzia kwenye tukio la bucha za nguruwe, lilikua kipindi ambacho mzee mwinyi aliruhusu kila fursa iliyozuiliwa kipindi cha utawala wa nyerere.
Ile watu kuwa na maamuzi huru ya kiuchumi billa makatazo ya sera za serikali ndio mzee mwinyi aliita "ruksa"
Bucha za nguruwe hazikuwa na uhusiano wowote na neno" ruksa " if my memory serves me correct.
 
Lakini hata kwa mtizamo wa kawaida tu unadhani ukikata moto leo bank umeacha 1bill zitakazozua balaa kwenye familia yako wakati wa kugawana huku wakati ulipokuwa hai ulikuwa unajua kabisa wapo watu wenye shida mbalimbali (orphan centers,wagonjwa mahospitalini ect) na uwezo wa kuwafikia ulikuwa nao na hukwenda unategemea sadaka yako uliyotoa msikitini au Kanisani imshawishi Mungu akupokee?

Ktk hilo ana point,shida yetu tulio wengi tukisikia neno kutoa sadaka tunadhani sadaka lazima ikatolewe kwenye nyumba ya ibada lakini sivyo kwa upana wake sadaka ni kutoa kwa wasiojiweza kama ni hela chakula mavazi hata ushauri.

Kwa kusema hivi nasimama nae,yupo sahihi!
 
Mimi ninachojua jina hilo limeanza pale aliporuhusu biashara huria wafanyabiashara waingize bidhaa zilizokuwa adimu kutokana na ukiritimba wa serikali wa kuhodhi kila kitu hali iliyofanya maisha ya wananchi kuwa magumu.
Chanzo cha neno Ruksa ni hizo bucha za nguruwe,ila baada ya hapo ukawa ni msamiati wa kila alichoagiza kifanyike au kilichofanywa ktk awamu yake.
 
Sahihi
 
Kuna siku anaelezea jambo alikuwa mahala kwamba ukirusha jiwe sehemu hiyo halidondoki..
Sasa hiyo mechaniam ya kisayansi yeye anasema ni allah quran.. alafu kashupaza shingo
huyo ni muongo na amewadanganya wajinga wengi wasio na elimu
 
Mbona P,alichelewa kutuamsha usingizini kwa maslahi ya Taifa😁
 
Ruksa ilianza wakati akifungua mipaka ya nchi, ilikua mwaka 1986 kama sikosei Hiyo ‘Ruksa’ ya kipindi cha sakata la Nguruwe ilikuwa ni muendelezo wa ‘Ruksa’ kutoka ile ya Kiuchumi kwenda ‘Ruksa’ ya uhuru wa kuabudu. Tena nakumbuka aliwatolea mfano hadi wale wanaokula panya nao Ruksa. Hadi wwanaoabudu mizimu ‘Ruksa’.
Labda Sheikhe alikuwa bado mdogo kukumbuka yote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…