Ulikuwepo enzi hiyo mkuu? Mbokomu itakuwa bucha la Mchagga hilo.
Sawa chief. Humu ndani huwa tunataniana na kutukanana na baba zetu bila kujua 🤣Yes nilikuwepo mkuu ,nilikuwa naenda kuchukua machungwa soko la tandale na nilikuwa naishi Mburahati.
1993 ulikuwa haujazaliwa?Sawa chief. Humu ndani huwa tunataniana na kutukanana na baba zetu bila kujua 🤣
Sitaki kubishana na mpumbavu endelea na mambo yakokwani we ulizaliwa lini kiasi kwamba usijue kwa nini mzee ruksa aliitwa hivyo?
SawaChanzo cha neno Ruksa ni hizo bucha za nguruwe,ila baada ya hapo ukawa ni msamiati wa kila alichoagiza kifanyike au kilichofanywa ktk awamu yake.
Bado1993 ulikuwa haujazaliwa?
mbona unatokwa povu jingi? Kwani kulikuwa na mabishano gani? Pungusa stress aisee !Sitaki kubishana na mpumbavu endelea na mambo yako
Ni kweli ali hutubia ZanzibarNimeona clip moja ya Sheikh mwanaharakati, Dr Sulle akisema watu wengi hawajui au wanapotosha hayati Rais Mwinyi kuitwa Mzee Ruksa.
Akitoa historia fupi Dr Sulle anasema mwaka 1993 kulitokea vurugu kubwa Dar es Salaam baada ya msichana mmoja wa Kiislamu aliyetumwa kununua nyama kukosea na kwenda kununua kitimoto katika bucha mojawapo la Nguruwe lilikuwepo Tandale.
Baada ya habari hiyo kusambaa anasema walifanya vurugu kubwa iliyosababisha uharibifu mkubwa wa mali pamoja na kutishia amani. Ndipo hayati Rais Mwinyi alipohutubia taifa katika kutuliza hali kwa hekima na katika kuwafanya Wakristo na Waislamu waishi kwa pamoja kwa upendo baada ya kutoa nasaha nyingi akatamka katika hotuba yake nchi hii haina dini, kila mtu mwenye kutaka chake na ale, mwenye kutaka jongoo ale ruksa, mwenye kutaka panya ale ruksa, na hapo ndipo neno ruksa lilianzia.
Pamoja na hilo, Dr Sulle anasema pia Mwinyi ndiye baba wa mageuzi wa uchumi na siasa wa taifa hili na hakuna Rais aliyelitendea haki taifa hili kumzidi Mwinyi.
Mwanahistoria Mohamed Said ni kweli hayati Rais mwenye kuitwa Mzee Ruksa sio kutokana na yeye kuleta uhuru wa biashara na siasa nchini bali hilo neno liliibuka kutokana na vurugu zilizohusisha nguruwe Tandale?
Zam...
Yule jamaa ni maamuma sana.. sasa hv kaja na stori za majini mwamba anaweza yaamrishaNimemsikiliza yule sheikh, ameongea ukweli hilo la rhuksa tu, lakini mengine mengi ni FIX kayabahatisha tu kwenye stories za vijiweni.Eti anadai hali ngumu wakati ule ililetwa na azimio la Arusha la 1967, wakati sio kweli . Hali ngumu ililetwa na vita vya Uganda na Mwalimu alipowatilia ngumu IMF. Pia ni kipindi hicho hicho Tanzania ilikua mstari wa mbele kwenye ukombozi wa nchi za kusini mwa Africa kwahio mabeberu yalihakikisha bongo inabanwa kiuchumi haswaa. Ukimsikiliza yule sheikh ni mtupu sana kichwani stories zake nyingi za vijiweni tu.