Dkt. Sulle: Mwinyi kuitwa "Mzee Ruksa" ilitokana na vurugu bucha la nguruwe Tandale 1993

Dkt. Sulle: Mwinyi kuitwa "Mzee Ruksa" ilitokana na vurugu bucha la nguruwe Tandale 1993

Nimemsikiliza yule sheikh, ameongea ukweli hilo la rhuksa tu, lakini mengine mengi ni FIX kayabahatisha tu kwenye stories za vijiweni.Eti anadai hali ngumu wakati ule ililetwa na azimio la Arusha la 1967, wakati sio kweli . Hali ngumu ililetwa na vita vya Uganda na Mwalimu alipowatilia ngumu IMF. Pia ni kipindi hicho hicho Tanzania ilikua mstari wa mbele kwenye ukombozi wa nchi za kusini mwa Africa kwahio mabeberu yalihakikisha bongo inabanwa kiuchumi haswaa. Ukimsikiliza yule sheikh ni mtupu sana kichwani stories zake nyingi za vijiweni tu.
 
Nimeona clip moja ya Sheikh mwanaharakati, Dr Sulle akisema watu wengi hawajui au wanapotosha hayati Rais Mwinyi kuitwa Mzee Ruksa.

Akitoa historia fupi Dr Sulle anasema mwaka 1993 kulitokea vurugu kubwa Dar es Salaam baada ya msichana mmoja wa Kiislamu aliyetumwa kununua nyama kukosea na kwenda kununua kitimoto katika bucha mojawapo la Nguruwe lilikuwepo Tandale.

Baada ya habari hiyo kusambaa anasema walifanya vurugu kubwa iliyosababisha uharibifu mkubwa wa mali pamoja na kutishia amani. Ndipo hayati Rais Mwinyi alipohutubia taifa katika kutuliza hali kwa hekima na katika kuwafanya Wakristo na Waislamu waishi kwa pamoja kwa upendo baada ya kutoa nasaha nyingi akatamka katika hotuba yake nchi hii haina dini, kila mtu mwenye kutaka chake na ale, mwenye kutaka jongoo ale ruksa, mwenye kutaka panya ale ruksa, na hapo ndipo neno ruksa lilianzia.

Pamoja na hilo, Dr Sulle anasema pia Mwinyi ndiye baba wa mageuzi wa uchumi na siasa wa taifa hili na hakuna Rais aliyelitendea haki taifa hili kumzidi Mwinyi.

Mwanahistoria Mohamed Said ni kweli hayati Rais mwenye kuitwa Mzee Ruksa sio kutokana na yeye kuleta uhuru wa biashara na siasa nchini bali hilo neno liliibuka kutokana na vurugu zilizohusisha nguruwe Tandale?
Ni kweli ali hutubia Zanzibar
 
Nimemsikiliza yule sheikh, ameongea ukweli hilo la rhuksa tu, lakini mengine mengi ni FIX kayabahatisha tu kwenye stories za vijiweni.Eti anadai hali ngumu wakati ule ililetwa na azimio la Arusha la 1967, wakati sio kweli . Hali ngumu ililetwa na vita vya Uganda na Mwalimu alipowatilia ngumu IMF. Pia ni kipindi hicho hicho Tanzania ilikua mstari wa mbele kwenye ukombozi wa nchi za kusini mwa Africa kwahio mabeberu yalihakikisha bongo inabanwa kiuchumi haswaa. Ukimsikiliza yule sheikh ni mtupu sana kichwani stories zake nyingi za vijiweni tu.
Yule jamaa ni maamuma sana.. sasa hv kaja na stori za majini mwamba anaweza yaamrisha
 
Back
Top Bottom