Dkt. Tax shirikiana na Waziri Simbachawene kukagua Uhamiaji; punguzeni kamatakamata za Waethiopia mikoani


Mkuu kupewa sheria haifungamani na passport kwani wengi wanakimbia na roho yao tu
Na waliobahatika kuwa na passports huwa wanazitupa kwa kuhofia kurudishwa walikotoka ambapo wengi huteswa zaidi
Ingawa Ulaya wakiingia ni vigumu kurudishwa kwao kutokana na haki za kibinadamu

Wakimbizi hata wale wa Ulyankulu enzi zile walikuwa wanaishi tu bila passport ila baadae walipewa Uraia

Inajulikana UN wanatoa fedha nyingi kwa ajili ya Wakimbizi ila mataifa mengi wanawadhulumu haki zao
 
Wazungu mioyo yao tofauti thus wamebarikiwa.Wazungu ni kimbilio la waafrika wanaoteswa na waafrika wenzao.
 

Uneongea point Sana.
Hata mexico niliona waliamua kuwakubalia wahonduras waliokuwa wanaelekea zao USA kwa miguu wapite nchini mexico bila bughuza ingawaje walikuwa hawana document migration
 
Umeongea vizuri sana mkuu, sijawahi kuona faida yoyote ambayo serikali inapata kwa kuwakamata hawa wahabeshi, sana sana ni hasara tuu tunapata na kujaza Magereza na mahabusu.
 
Wazungu mioyo yao tofauti thus wamebarikiwa.Wazungu ni kimbilio la waafrika wanaoteswa na waafrika wenzao.

Wana huruma sana na pia sheria zao ndio zinalinda watu
Ila waafrika kwa waafrika tunachukiana sana
 
Ni ujinga kuamini kwamba wote wanapita halafu badae tutaanza kuulizana wahalifu wakigeni wanatokea wapi tusirahisishe mambo magumu.
Kweli ujinga ni kipaji, kama kweli issue ni wahalifu je Warundi kule mipakani tumewaweza? Wahabeshi hakuna asiyejua kuwa wanakimbilia South Africa, na ndiyo maana ukiambiwa utoe mifano ya wahalifu from Ethiopia hapa nchini utaishia kutoa mimacho tuu kama kenge..
 
Mbaya sana hii mkuuu, yaani ni kubaniana mwanzo mwisho...
 
46 WAMEEEEDAKWA MANYARANDANI YA GARI LA KUHIFAFHIA SAMAKI HAHAHAHAA
 
Hii mipaka ya wakoloni tumemwekea nani?
 
Ni ujinga kuamini kwamba wote wanapita halafu badae tutaanza kuulizana wahalifu wakigeni wanatokea wapi tusirahisishe mambo magumu.
Kwanini hawakamatwi Kenya wala Zambia?
 
Mkuu bado umezama kwenye mipaka tulioachiwa na mabeberu?futa hii so called mipaka na Africa belongs to Africans
Una akili sana wee jamaa!!! Ethiopia kabla ya mkutano wa Berlini ilikuwa ina enda mpaka Zimbabwe ya leo!! wkt wa ukoloni tulichanganywa tu na ethiopia tukitumia hela moja!

zaidi ya nusu wengi humu Bongo tumetokea ethiopia! leo ukienda Addis ababa kuna watu utakuwa unawastukia km Unganiko la damu......mipaka hii imewekwa na adui yenu!..... km ni ivo waache waje!!! ...

mbona ulaya kwa adui yetu! wakimbizi wanapewa mpaka uji? dawa, blankets, polee kubwaa! lkn sisi tuawasimanga, chuki, tunawazodoa! mpaka wanakufa kwa kuzodolewa jamani!

kwanza hapa bongo wanapita tu jamani sasa eti wanamzuia nini?? wapeni chakula, maji, wakokeeni myoto muwasindikize mpaka mikapakani, angalia mfano kuleee S. america weupe wanawaruhusu tu wapite kuelekea USA! jamani mwee! ivi tuna nini sisi weusi?

Binadamu wote ni sawa na Africa ni moja sijui km alisoma hii!!................Mungu Ibariki Africa......waache waende wanakotaka si wako Africa? kwa nini wenyewe kwa wenyewe wanapenda sana kuwagawa wao kwa wao!

kule Ethiopia kuna kichapo kinacho dhaminiwa na adui wetu sote ajili ya Bwawa la Umeme tu! tena basi kwa faida ya weusi km wewe !sasa anataka wafie vitani? mbona waswahili wana roho mbaya ki hivi?

Kumbukeni kwa siasa zenu hizi za hovyo na nyie mtakuwa wakimbizi one day!! sasa wawafanyie km hivi!! na mnajua fika mshahara wa dhambi ni mauti!! wapo wabongo wengi wakimbizi leo ajili ya jiwe!! kwa nini sasa mjinga mmoja awachukie wakimbizi?
 
Uhamiaji wakiamua hawa waethiopia na wasomali haramu hawatakuwepo
Waende wapi mama D'' ni sheria za kimataifa zina walinda! marufuku kumnyanyasa mkimbizi! kwa vyovyote vile! na sisi tume sign huo mkataba!
 
Nasikia hao jamaa eti ni wayahudi weusi!eti ni watoto wa mfalme suleiman!!kwanini tusiwaache tuzaliane ili tupate Breed nzuri kuliko vilaza wengi tulionao???
 
Nahisi huu ni mradi wa watu. Nchi zote wanazopita hawa watu kuelekea SA hakuna wanakokamatwa ila Tanzania tu. Tena kwa kelele nyingi za "hatari kwa usalama wa nchi"! Ethiopia kwenyewe ukiwauliza serikalini wanashangaa Tanzania kuhangaika na watu wao wanaoenda SA ili kutafuta maisha bora. Tena huko SA inadaiwa kuna namna nyepesi ya kutimkia Ulaya na US. Inaelekea Ethiopia wana sera ya kimyakimya ya kuruhusu watu wao watoke nje kupunguza presha ya kiuchumi na kisiasa.

Labda serikali itufahamishe kama taifa tunapata nini hasa kwa kukimbizana na hawa wahabeshi ambao hawana interest ya kukaa kwetu? Au tunalazimika kuwazuia hapa? Mbona huko SA kwenyewe wanapokelewa tu bila mikwaruzo? Na kwa kadiri kivutio hicho kipo watahangaika tu kuelekea huko siku zote. Na sisi tutaendelea kutumia rasilimali zetu kuhangaika nao hapa kwetu. I believe kuna watu wananufaika. Haiyumkiniki tukawa mazuzu kiasi hicho.
 
Acha wapite zao wakatafute maisha, watu wengine mnazingua sana sijui ni njaa mnataka rushwa au roho mbaya tuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…