Fundi Madirisha
Senior Member
- Jun 30, 2020
- 184
- 988
Tunatoa sana ushauri humu JF na wakati mwingine tunaonekana kama wavurugaji waliotumwa na wapinzani au watu tusiokuwa na uzalendo na taifa letu, mwisho wa siku ushauri inapuuzwa na kumsikia mama analalamika kua wapo watu ndani ya serikali hawako naye na wengine hawaelewi.
Tulishauri kwamba Mama anapoanza awamu yake ya 6 aingie na damu mpya itakayomfanya na mifumo yake ya utawala. Mtangulizi wake alikua na mifumo yake na watu wake, watu wake si rahisi sana kwenda na mfumo wa Mama. Kwahiyo mabadiliko ilikua ni muhimu sana katika kila wizara na kila taasisi ili mambo yaweze kwenda sawa sawa.
Turudi kwenye bunge letu la sasa ambalo kimsingi ni sawa na la chama kimoja kutokana na wingi wa wabunge wa CCM. Kiti cha spika kwa sasa kipo wazi, nafasi hii inatakiwa kujazwa na mtu ambaye ni mpya kabisa ambaye hana chembe kabisa za utawala wa awamu ya 5. Dkt Tulia alikua ni Mteule wa JPM, naamini kabisa kwa zaidi ya 90% bado kichwa chake kipo kwa JPM, si rahisi kwenda na mifumo ya Mama. Baadaye anaweza kuja kuwa kikwazo katika bunge na serikali. Tunamjua Dkt Tulia hua ni mbishi, anajua kila kitu hasa sheria, sasa akipewa uspika wenye mamlaka na Kinga itakuwaje?
Chama cha mapinduzi chini ya Mwenyekiti wake mpya wawe makini sana kwenye hii nafasi. Atafutwe mtu mpya mwenye sura ya utawala wa awamu ya 6. Awe mtu wa Makamo, mwenye busara na hekima,awe kama Baba/Mama, mlezi, asiwe kijana na anayejua sheria .
Kwangu mimi kwa hakika Mama Majina angechukua form,huyu Mama ameshakua Mwenyekiti wa bunge akiisimamia vizuri. Mzee Zungu ni mlezi na anajua pia kutoa ufafanuzi kwa kina ikiwa kuna tatizo. Mtu mwingine ambaye Kama angeshauriwa achukue form ya uspika wa bunge ni Mama Dr Asharose Migiro, naye busara zimemjaa sana. Mzee vijisenti naye yupo vizuri sana kwa shughuli za kuendesha bunge.
Chonde Chonde CCM msijidanganye mkaweka Spika kijana mtakuja kujuta, zikianza kelele hataheshimika na wala hatasikilizwa, ataishia kufukuza na kutisha tu kama Ndungai ambaye alilivuruga sana bunge. Naibu Spika abakie kua Dkt Tulia aendelee kujifunza ili akifikisha angalau miaka 50 busara zitakuwepo na atapewa nafasi.