Ngungenge
JF-Expert Member
- Jun 11, 2016
- 2,914
- 3,386
Inategemeana na tulia anaamini kwenye nnFundi Madilishi anasema Dr. Tulia alikuwa chaguo la Magufuli na hafai kuwa spika, tukia-assume logic ya Madilisha iko sawa, madam SSH alikuwa mteule wa JPM kama running mate, ushindi wa urais ulikuwa wa JPM kuwa rais na SSH kuwa VP, hivyo kufuatia kifo cha JPM, kikatiba VP anatakuwa kuapishwa na kuwa Rais wa nchi.
Mpango alikuwa mteule wa JPM kama kamishina mkuu wa TRA, mbunge na baadae waziri wa fedha, akagombea ubunge akawa aziriwa fedha tena. Baada ya msiba ilitulazimu tuwe na VP, basi Mpango nae awe haafai kwa logic za Madilisha.
Tanzania ni ya Watanzania wote. Dr. Tulia alikuwa Deputy AG wakati wa JK, ni Mtanzania, mifumo ya uteuzi kwenye chama wakiona anakidhi kuwa spika watampitisha.
Isifikie tukabaguana kisa kwa kuwa fulani alikuwa mteule wa fulani hafai. At some point ni lazima tuishi leo; kama kuna mtu au kundi la watu lina tofauti binafsi na JPM isiwe msingi wa kuwaharibia wengine.
Siko hapa kumpingia debe Tulia, ila yeye kuwa Mtanzania wasitokee wachache wakambagaza kwa kuwa tu aliteuliwa na JPM.
Tukifuata logic yako itabidi serikali yote iondoke ikiwamo wakuu wa vyombo vya dola kwa kuwa majority walikuwa wateule wa JPM.
Jana SSH kaongea kitu kizuri sana, Urais ni taasisi ambayo at some point lazima awepo wa kuiongoza, alianza JKN, AHM, BWM, JMK, JMP na leo tuna SSH na ipo siku atakuwa yule ambae zamu yake itafika.
Kama anaona Mama hatoshi anawezaje kumpa ushirikiano wa kutosha.?
Hii hoja ina macho kuwa ili pasiwepo na lawama aje mpya aendana nae