Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Dkt. Tulia Ackson, leo tarehe 17 Septemba 2024, amekutana na kufanya mazungumzo na Spika wa Bunge la Umoja wa Falme za Kiarabu, Saqr Ghobash, katika Ofisi za Bunge hilo zilizopo Abu Dhabi.
Katika mazungumzo yao, Viongozi hao wamejadiliana kwa kina kuhusu namna bora ya kuimarisha na kuendeleza ushirikiano mzuri uliopo kati ya Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na nchi za Umoja wa Falme za Kiarabu pamoja na kuangazia mahusiano kati ya Tanzania na nchi za Umoja wa Falme za Kiarabu.
Mazungumzo hayo yameangazia masuala ya ushirikiano wa kiuchumi, kijamii na kisiasa kati ya pande zote mbili huku lengo likiwa ni kukuza mafanikio ya pamoja na ustawi wa wananchi wao.