Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Bibi wa miaka 72 mkazi wa mtaa wa Mwanyanje, kata ya Igawilo jijini Mbeya ambaye aliingiliwa na watu wasiofahamika nyumbani kwake anategemewa kujengewa nyumba na Dkt. Tulia Ackson
Ikumbukwe bibi huyo ni moja ya watu wanaoishi katika mazingira magumu ambao walifikiwa na bendera ya Upendo iliyoongozwa na Taasisi ya Tulia Trust iliyo chini ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mbunge wa Mbeya Mjini na Rais wa Umoja wa Mabunge (IPU) Dk. Tulia Ackson.
Wakati ambao bendera hiyo ilipita ndipo taasisi ya Tulia Trust iliona umuhimu wa kumjengea nyumba bibi huyo kutokana na hali ya nyumba aliyokuwa akiishi kuwa na hali mbaya.
Wakizungumza wakati wa kuanza ujenzi wa nyumba hiyo viongozi wa mtaa wa Mwanyanje na majirani wameeleza hali ambayo bibi huyo alikuwa akipitia huku Afisa Habari wa Tulia Trust Joshua Edward akibainisha ujenzi wa nyumba hiyo unaambatana na nyumba zingine mbili katika kata ya Uyole na Itezi ambazo zote tatu zinatakiwa kukamilika ndani ya mwezi moja kuanzia hii leo.