Atukuzwaye
Senior Member
- Oct 5, 2026
- 191
- 250
Mbunge wa Jimbo la Uyole ambae ni Rais wa Heshima wa IPU Dkt. Tulia Ackson ametoa shukrani za dhati kwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Deogratius Ndejembi kufanya ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo kwa wananchi Jijini Mbeya pamoja na kuishukuru serikali ya awamu ya sita iliyo chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa fedha zote alizozitoa kwa ajiri ya miradi hiyo.
Aidha Dkt. Tulia Ackson amemuomba Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Degratius Ndejembi kuweza kupata barabara za rami kilomita 7 katika Jimbo la Uyole kutokana na kuwepo kwa changamoto ya uchakavu wa barabara za mitaani ambazo wananchi wanazitumia.
Makamu wa Rais wa Tanzania, Deogratius Ndejembi amempongeza Dkt. Tulia kwa uwezo wake na upeo mkubwa aliokua nao kwa kuweza kuanzisha miradi ya kimkakati ambayo inaleta faida kwa wananchi kwenye maendeleo, ametoa pongezi kwa Dkt. Tulia kwa uanzilishi wa ujenzi wa barabara njia nne (TANZAM) barabara inayoenda kuleta chachu ya maendeleo kwani ndio barabara inayozingunisha Tanzania na nchi jirani.
Pamoja na hayo Makamu wa Rais Mhe. Ndejembi amemtaka Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM-TAMISEMI) Prof. Riziki Shemdoe, kukagua barabara hizo katika jimbo hilo na kuweza kumpatia taarifa ilikusudi changamoto hizo ziweze kupatiwa ufumbuzi.
Vilevile katika ziara hiyo Waziri wa Maji, Juma Aweso amempongeza Mbunge wa Jimbo la Uyole kwa maono yake ya kuishauri serikali kuleta mradi mpya wa maji ambapo chanzo chake ni mto Kiwira, mradi huo unaenda kuwa chachu ya kupunguza na kuondoa changamoto ya maji katika mkoa wa Mbeya.