Pre GE2025 Dkt. Tulia akosoa maandamano ya CHADEMA Mbeya

Pre GE2025 Dkt. Tulia akosoa maandamano ya CHADEMA Mbeya

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Siku chache baada ya kufanyika kwa maandamano ya CHADEMA mkoani Mbeya, Mbunge wa jimbo la Mbeya mjini Dkt. Tulia Ackson (CCM) ametoa wito kwa wakazi wa Mbeya kuacha kuhangaika na maneno ya wanasiasa wasiowatakia mema kwa kuwa wakati uliopo sasa ni wa kupelekewa maendeleo na si maneno

Dkt. Tulia ambaye pia ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mkurugenzi wa taasisi isiyo ya kiserikali ya 'Tulia Trust' amezungumza hayo Februari 23.2024 wakati wa hafla ya kukabidhi nyumba kwa Hosea Kalemali ambaye ni mmoja wa wanufaika wa nyumba tisa (9) zilizotolewa na taasisi hiyo kupitia mpango wa 'Tulia Trust na Jamii'

Kuhusu kufana kwa maandamano hayo Dkt. Tulia amesema ameshangazwa kusikia maandamano hayo yalikuwa na muitikio wa watu wengi jambo ambalo amedai si sahihi kwa kuwa wengi waliojitokeza haifahamiki wametokea wapi kwa kuwa hawafahamiki hata na wenyeji yaani wakazi wa Mbeya

Dkt. Tulia pia amekosoa kitendo cha CHADEMA kuwatembeza watu kwa miguu (waandamanaji) umbali mrefu akitolea mfano wa kutoka Mbalizi hadi uwanja wa Ruanda Nzovwe jijini Mbeya kwenda kwenye mkutano jambo ambalo amedai CCM haiwezi kufanya hivyo kwa kuwa ikiwahitaji watu hao itawatumia usafiri wa kuwafikisha kwenye eneo husika.

Credit - JamboTv
Si aende kugombea kwao Tukuyu?Mbona hata wao wanawabeba kwenye malori?Sasa hata wakitembezwa mbona hawajalalamika na yeye anawajua watu wote wa jiji la mbeya.mbona hata kwao mabonde Tukuyu hawamjui?
 
Ngoja uone Tulia aluchofanya siku ya maandamano. Aliitisha mkutano shule ya Mkapa pale siku hiyo hiyo ya maandamano. Mkutano ulikuwa wa waendesha Bajaj wa Mbeya hasa wa Mbeya Jiji ambao wako katikati hapo maeneo ya Kabwe kujadili nauli za Bajaj. Kumbuka kwa hapo Mbeya Kabwe ndo kama kitovu ama center ya 'vijana'. Pamoja na hiyo diversion lakini watu walikuwa shazi ktk maandamano.

Kilichozingua maandamano ni mvua. Asee mvua ilipiga yaani kama siyo mvua CDM walijipanga sana.

Nilichoona Mbeya CDM inakubalika saana. Tulia ana kazi ya kufanya kutetea ubunge wake.
Aende kwao mabonde Tukuyu akapambane na Sauli
 
Back
Top Bottom