Dkt. Tulia amkabidhi nyumba mwananchi mwenye uhitaji jimbo la Uyole

Dkt. Tulia amkabidhi nyumba mwananchi mwenye uhitaji jimbo la Uyole

PAYE

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2025
Posts
459
Reaction score
644
Aprili 2, 2026 Mkurugenzi wa Taasisi ya Tulia Trust ambaye pia ni Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani(IPU) na Mbunge wa Jimbo la Uyole Mhe. Dkt. Tulia Ackson amesema nyumba zinazojengwa kwaajili ya watu wenye uhitaji zinajengwa kulingana na mahitaji ya familia husika.

1775660746751.png

Dkt. Tulia ameyasema hayo kwenye hafla ya kumkabidhi nyumba Bi. Elizabeth Jimmy mkazi wa mtaa wa Mwasote kata ya Itezi Jimbo la Uyole ambaye amejengewa nyumba yenye vyumba vitatu na sebule huku akibaisha kuwa nyumba ndogo zaidi inayojengwa na Tulia Trust inakuwa na vyumba viwili vya kulala na sebule, huku akiwasisitiza wadau wengine kujitolea kusaidia kaya zenye uhitaji.

1775660756486.png

Katika hatua nyingine Dkt. Tulia amesema wale wote waliofikiwa na bendera ya upendo watasaidiwa kulingana na mahitaji yao ambapo atasaidia katika matibabu kwa wale wenye uhitaji zaidi, kugawa viti mwendo na kutoa mitaji kwaajili ya kuendelea kuwainua wananchi kiuchumi huku akiitaka jamii kujenga utamaduni wa kusaidiana.

Aidha Viongozi wa kata hiyo wakiongozwa na Diwani James Kapolesya, wadau mbalimbali wakiwemo Bodabdoa na Bajaji Jimbo la Uyole pamoja na wananchi wamemuunga mkono kiongozi huyo kwa kutoa misaada kwenye familia hiyo ikiwa ni pamoja na Vyakula, Godoro, Kitanda na fedha.
1775660767300.png

1775660781246.png

1775660796423.png

1775660803186.png

1775660813535.png
 
Kazi nzuri sana mh mbunge.
Mungu aendelee kukuongoza vema katika hayo unayoyafanya
 
Huna jema.
Jema gani mkuu! Huoni kabisa kuwa hii ni public stunt. Wema wanakuwaga hivi kweli? Wema hawahitaji dunia nzima ijue wanapofanya wema. Wema hatembelea ma-rolls royce huku wanatunuku vibanda kwa maskini huku wakitangaza dunia nzima ione. Hawa ni wauaji siyo watu wema.
 
Ukiachana na siasa hili ni jambo la kibinadamu amefanya.
 
Jema gani mkuu! Huoni kabisa kuwa hii ni public stunt. Wema wanakuwaga hivi kweli? Wema hawahitaji dunia nzima ijue wanapofanya wema. Wema hatembelea ma-rolls royce huku wanatunuku vibanda kwa maskini huku wakitangaza dunia nzima ione. Hawa ni wauaji siyo watu wema.
Ila kutoa hicho kidogo na kutotoa kipi Bora ?

Sometimes , open ur eyes and think effectively.

Kuna wanasiasa wangapi Wana mapesa ya ufisadi na hawasaidii MTU

She can be wrong ila unabidi kujua kuwa anaweza asifanye na bado akapata publicity
 
Hello! Ni bora kutotoa kabisa kuliko kutoa kwa malengo ambayo ni maovu kama wanavyofanya hawa CCM. Kutoa kidogo namna hiyo tena kwa mtu mmoja kuna negative effect na mdhara yake yanaenda mbali. Kna watu wanapumbazika, wanaacha kukabilina na matatizo halisi na kujikutana wanapambana na matatizo bandia na matokeo yake ni society kuendelea ku-suffer. Najua kwa watu waliokulia kwenye umaskini wa mali na akili siyo rahisi kuliona hili na hudhani kupewa ''posho'' kama kuku ndiyo kuonyeshwa upendo, lakini kama unafikiri kwa kina utagundua kuwa upendo wa kweli ni ule unamfanya watu wengi wajitegemee wenyewe na siyo kusaidia mtu mmoja mmoja. Mfundishe mtu kuvua samaki na siyo kumpa makombo ya samaki... hutatatua shida yake. NOTE: sipingi mtu mmoja mmoja au kiongozi kusaidia mtu binafsi hata kwa kidogo namna gani ila napinga ile kiongozi kuishi kwa ufahari huku akifanya ufisadi na kuua raia wengi kwa ufisadi au kwa risasi huku akitoa makombo kwa mtu mmoja ili aendelee ku-maintain status yake.
 
Hao raia wote wameenda kumshuhudia mtu mmoja akikabidhiwa nyumba?!
 
Ila kutoa hicho kidogo na kutotoa kipi Bora ?

Sometimes , open ur eyes and think effectively.

Kuna wanasiasa wangapi Wana mapesa ya ufisadi na hawasaidii MTU

She can be wrong ila unabidi kujua kuwa anaweza asifanye na bado akapata publicity
Wanasiasa wote wabunge Tanzania huwa wanatoa misaada binafsi kwa watu wawili watatu kwa mkakati wa kujionyesha ila ukweli ni kwamba ni vitu visivyo na impact kwa watu wao. Ingekuwa na maana zaidi kama angewatengenezea bararaba ambazo kila mtu kuanzia wanafunzi wa shule mpaka wauza mboga wangenufaika nazo.
 
Don't confuse dues and responsibility
 
Jema gani mkuu! Huoni kabisa kuwa hii ni public stunt. Wema wanakuwaga hivi kweli? Wema hawahitaji dunia nzima ijue wanapofanya wema. Wema hatembelea ma-rolls royce huku wanatunuku vibanda kwa maskini huku wakitangaza dunia nzima ione. Hawa ni wauaji siyo watu wema.
You can see the glass half full or half empty.
 
Back
Top Bottom