Jannatul Firdaus
JF-Expert Member
- Aug 4, 2026
- 446
- 1,113
Mkurugenzi wa Taasisi ya Tulia Trust ambaye pia ni Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani(IPU) na Mbunge wa Jimbo la Uyole Dkt. Tulia Ackson amefanya ziara katika kata ya Ilomba ambapo amewatembelea na kuwapa tabasamu watu wenye ulemavu na wanaoishi kwenye mazingira hatarishi.
Dkt. Tulia amekabidhi viti mwendo 14 kwa watu wenye ulemavu viwasaidie kutembea kutoka hatua moja kwenda nyingine ili waweze kuendelea kufanya shughuri zao mbalimbali bila changamoto yeyote.
Katika hatua nyingine Dkt. Tulia amekabidhi nyumba ya kuishi mjane Bi. Queen Andembwisye ambaye alikuwa anaishi kwenye mazingira hatarishi na familia yake kwa kukosa makazi, hii inakuwa nyumba ya 25 kujengwa na Taasisi ya Tulia Trust kwaajili ya watu wenye uhitaji zaidi kupitia mpango wake wa Tulia Trust Mtaani kwetu.