Pre GE2025 Dkt. Tulia awataka vijana kujitokeza kugombea kwakua CCM imejipanga kushika dola

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

the guardian 17

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2024
Posts
395
Reaction score
570
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa, ambaye pia ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mlezi wa CCM kwa Mikoa ya Kusini na Kaskazini Unguja, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, amesema kuwa CCM imejipanga kikamilifu kuhakikisha inaendelea kushika dola katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025, kwa kuwa kazi iliyofanywa na Serikali inatosha kutangaza sera za ushindi.

Dkt. Tulia ametoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza na Wanachama wa CCM katika Ukumbi wa CCM Hanyegwamchana, mara baada ya kuhitimisha ziara yake ya kikazi katika Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar, leo tarehe 20 Februari 2025. Ziara hiyo ililenga kukagua miradi mbalimbali ya CCM pamoja na kuwaeleza wananchi kuhusu malengo ya CCM katika mkoa huo.
1740115930496.png

Aidha, Dkt. Tulia amewahimiza vijana wa CCM wenye sifa za kugombea nafasi mbalimbali za Uongozi kujitokeza kwa wingi, ili waweze kuonesha uwezo wao na kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa taifa. Amesisitiza kuwa CCM ina sera shirikishi zinazotoa fursa kwa kila mtu wakiwemo vijana, kushiriki katika Uongozi na maendeleo ya nchi.

Soma: Sama: Pre GE2025 - Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
 
View attachment 3243065

well done and well said 💪👊
 
Lakini kuna vijana walitaka kugombea Urais wakapokonywa hiyo haki yao pale Dodoma 🐼
 
Napataje kadi na tishet mwaka huu lazima nibubujikwe na machozi ya furaha km lucas
 
Back
Top Bottom