LGE2024 Dkt. Tulia awataka Wananchi Mbeya kuiamini Serikali, awahimiza kuwachagua Viongozi wa CCM Uchaguzi wa Serikali za Mitaa

LGE2024 Dkt. Tulia awataka Wananchi Mbeya kuiamini Serikali, awahimiza kuwachagua Viongozi wa CCM Uchaguzi wa Serikali za Mitaa

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
WhatsApp Image 2024-11-11 at 16.30.54_f975ab49.jpg

WhatsApp Image 2024-11-11 at 16.30.54_03c9ff53.jpg

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambae ni Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Mbunge Jimbo la Mbeya Mjini, Dkt. Tulia Ackson, amewataka Wananchi wa Mbeya kuendelea kuiamini Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Amewataka Wananchi hao kushiriki kikamilifu kwa kuwachagua Viongozi wa CCM kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, 2024 pamoja na Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwakani.

Dkt. Tulia ameyasema hayo leo tarehe 11 Novemba, 2024 wakati akikabidhi nyumba za kuishi kwa Wananchi waliokuwa wakiishi katika mazingira magumu Jijini humo. Waliokabidhiwa nyumba hizo ambazo zimejengwa na Taasisi yake ya Tulia Trust ni pamoja na Bi. Winifrida Kapingu mwenyeji wa Kata ya Ilemi, Bibi Tusekile Kazimoto na Bibi Mwaine Lumbalile wakazi wa Kata ya Iyunga.

Akizungumza na Wananchi hao, Dkt. Tulia amesema kuwa, Jiji la Mbeya limekuwa na changamoto nyingi na za muda mrefu ikiwemo ubovu wa miundombinu ya barabara, elimu, afya, maji n.k ambapo katika kipindi kifupi cha Uongozi wa Serikali ya awamu ya sita tayari changamoto hizo kwa kiasi kikubwa zimepatiwa ufumbuzi.

WhatsApp Image 2024-11-11 at 16.30.52_7a0b254e.jpg

WhatsApp Image 2024-11-11 at 16.30.53_f16d1d95.jpg

WhatsApp Image 2024-11-11 at 16.30.52_7123b162.jpg
 
Back
Top Bottom