upupu255
JF-Expert Member
- Sep 4, 2024
- 418
- 550
Spika wa Bunge la Tanzania na Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini, Dkt. Tulia Ackson, kupitia Taasisi yake ya Tulia Trust, wamesema pamoja na kuendelea na ujenzi wa nyumba ya Mzee Obed Ambonisye, anayeishi kwenye mazingira magumu pamoja na familia yake katika Kijiji cha Matema, Wilaya ya Kyela, Mkoa wa Mbeya, bado wana mpango wa kujenga nyumba nyingine tatu kwa wahitaji ndani ya Jiji la Mbeya.
Afisa Habari wa Taasisi ya Tulia Trust, Joshua Edward, amesema ujenzi huo ulioanza Machi 12, mwaka huu, unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi huu na nyumba hiyo kukabidhiwa kwa familia ya Ndg. Obed Ambonisye, ambaye ni mlemavu wa miguu na anaishi kwenye mazingira magumu kwa kukosa makazi.
Joshua amesema ujenzi wa nyumba hiyo yenye vyumba vinne vya kulala na vyoo viwili—ndani na nje—kukamilika kwake kutakuwa ni mwanzo wa kuanza ujenzi wa nyumba nyingine tatu za wahitaji zitakazojengwa Mbeya Mjini katika Kata za Uyole, Itezi, na Igawilo.
Soma: Dkt. Tulia kuijengea nyumba familia yenye uhitaji Kyela, atoa msaada wa chakula na mavazi
Kwa upande wa familia ya Mzee Ambonisye na wananchi wanaoishi karibu naye, wameishukuru Taasisi ya Tulia Trust kwa kasi kubwa ya ujenzi wa nyumba hiyo na kuwaomba waendelee kutoa msaada kwa kuwasaidia zaidi wenye uhitaji wilayani Kyela.