Dkt. Tulia kukusanya Tsh. Milioni 300 za kusaidia jamii kupitia Betika Mbeya Tulia Marathoni

Dkt. Tulia kukusanya Tsh. Milioni 300 za kusaidia jamii kupitia Betika Mbeya Tulia Marathoni

Lexuss

Member
Joined
Mar 24, 2026
Posts
24
Reaction score
28
IMG_8244.JPG.jpeg


Msimu wa 10 wa mbio ya Betika Mbeya Tulia Marathoni umezinduliwa jijini Dar es Salaam, huku waandaaji wakilenga kukusanya Sh300 milioni kwa ajili ya kusaidia kuboresha miudombinu ya afya na elimu.

Mbali ya afya na elimu, pia waandaaji ambao ni Taasisi ya Tulia Trust itasaidia jamii yenye uhitaji, kama ambavyo imekuwa ikifanya kwa kuwaboreshea baadhi ya wenye uhitaji makazi, na mahitaji mengine ya kibinadamu.

Wakati usajili wa kishiriki mbio hiyo ukiendelea katika maeneo mbalimbali jijini Mbeya na Dar es Salaam sanjari na online, waandaaji wamezindua jezi itakayotumika msimu huu.

Akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika Aprili 21, 2026 kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Taasisi ya Tulia Trust, Dk Tulia Ackson amesema msimu huu Betika Mbeya Tulia Marathoni inakwenda kufanyika kwa ubora wa hali ya juu zaidi.

Dk Tulia ambaye pia ni mbunge wa Uyole na rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) amesema mbio hiyo inayofanyika msimu wa 10 mwaka huu, imekuwa ya tofauti ikifanyika kwa mafanikio wakishirikiana na kampuni ya michezo ya kubashiri matokeo ya Betika ambayo ni mdhamini mkuu kwa mwaka wa pili mfululizo.

Amesema Tulia Trust wamepanga kukusanya Sh 300milioni kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya elimu na afya.

"Uboreshaji huu ni kwa ajili ya kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Serikali ambayo imekuwa ikiboresha sekta mbalimbali ikiwamo ya afya na elimu, sisi Tulia Trust huwa tunasaidia kuboresha katika maeneo fulani, mfano wana zahanati, hawana wodi ya wazazi, sisi tunajenga na kutafuta wadau kupeleka vifaa pale, vivyo hivyo katika elimu, tunaunga mkono juhudi zinazofanywa na Serikali," amesema.

Mbali na kuboresha miundombinu ya elimu na afya, amesema pia wanaisadia jamii yenye uhitaji akitolea mfano kusaidia makazi na huduma nyingine za kijamii.

"Hivi sasa tuna mdhamini mkuu Betika, wigo utakuwa mpana zaidi kwa sapoti yao. A kila mwananchi ambaye amekuwa bega kwa bega na Taasisi ya Tulia Trust katika kufanikisha mbio hii," amesema.

Mbio hiyo msimu huu itafanyika Mei 15 na 16 jijini Mbeya ikishindanisha wanariadha wa mbio za uwanjani, kuanzia mita 100 hadi 1500 siku ya kwanza na wale wa mbio za nusu marathoni (kilomita 21) na marathoni (kilomita 42) wakichuana siku ya pili.

Pia kutakuwa na mbio za kujifurahisha za kilomita tano na 10, huku zawadi kwa washindi zikitarajiwa kuongezeka kulinganisha na msimu uliopita.

Meneja Mkuu wa Betika Tanzania, Samuel Mcheru amesema kampuni hiyo imeamua kuwekeza katika mbio hiyo kubwa Tanzania ambayo imekuwa ikikuza mchezo wa riadha nchini.

Alisema kampuni ya Betika inaamini nguvu ya michezo katika kubadilisha jamii, hivyo kwa kushirikiana na Taasisi ya Tulia Trust wameendelea kudhamini mbio hiyo kubwa kwa mwaka wa pili mfululizo.

Wakiizungumzia mbio hiyo, Baadhi ya wakazi wa Mbeya wameeleza fursa ambazo wamekuwa wakizipata kila mwaka inapofanyika wakiielezea kuwa marathoni ya mfano si tu mkoani Mbeya bali na mikoa jirani.

"Kuna fursa nyingi za uchumi na biashara inapofika msimu wa Betika Mbeya Tulia Marathoni, kuanzia kwa mama lishe, wajasiriamali wadogo wadogo, waendesha bodaboda, wamiliki wa hoteli na nyanja tofauti.

Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Rogart Stephen Akhwari amesema mbio ya Betika Mbeya Tulia Marathoni ni miongoni mwa mbio zenye ushindani na zinazotoa fursa kwa wanariadha Watanzania kuchuana kwa upana zaidi kuanzia kwenye mbio za uwanjani hadi zile za barabarani ikifanyika kwa siku mbili mfululizo," amesema.
 
Back
Top Bottom