PAYE
JF-Expert Member
- Jun 19, 2025
- 459
- 644
Taasisi ya Tulia Trust chini ya Mkurugenzi wake ambaye ni Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Mbunge wa Jimbo la Uyole Dkt. Tulia Ackson imekabidhi vifaa kwaajili ujenzi wa nyumba ya Philipo Mwakalindile anayeishi kwenye mazingira magumu kata ya Nsalaga.
Mwakalindile (54) anaishi mtaa wa Igamba kata ya Nsalaga kwenye nyumba ambayo inachangamoto ya paa kuvuja na nyufa ambazo zingeweza kusababisha nyumba hiyo kuanguka hivyo Tulia Trust imechukua jukumu la kumjengea nyumba nyingine ya kuishi na kufikisha idadi ya nyumba 25 zilizojengwa na Tulia Trust kupitia mpango wa Tulia Trust Mtaani Kwetu.
Ujenzi wa nyumba hiyo unatarajiwa kukamilika ndani ya siku 30 na kumkabidhi Mwakalindile anayefanya vibarua ili kujiingizia kipato kwani anaishi mwenyewe baada ya kutengana na mke wake tangu mwaka 2007 alipopata ajali ya gari iliyopelekea ulemavu wa mkono.
Soma zaidi;
- Dkt. Tulia Ackson aijengea nyumba familia iliyopatwa na janga la moto Uyole
- Dkt. Tulia amkabidhi nyumba mwananchi mwenye uhitaji jimbo la Uyole
- Dkt. Tulia ampa tabasamu mwananchi mwenye ulemavu kata ya Mwakibete
- Dkt. Tulia Ackson kumjengea Nyumba Bibi aliyebakwa na watu wasiojulikana Mbeya
- Dk. Tulia aifuta machozi familia iliyopoteza nyumba kwa moto, Igawilo