Dkt. Tulia: Nyanda za Juu tumechoka kuwa washangiliaji na sisi tunataka treni ya umeme kama 'Wenzetu'

Dkt. Tulia: Nyanda za Juu tumechoka kuwa washangiliaji na sisi tunataka treni ya umeme kama 'Wenzetu'

Na je ya kati hakuna magofu na majengo kama vibanda umiza lakini wanajengewa treni ya umeme,kumbuka mikoa ya nyanda za juu kusini ndio zamani ikiitwa big 4 na sasa ni big 6, tunawalisha nyie wote, na tunalipa kodi zaidi hata ya hao ambao unawakingia kifua.
Big 4 kwa kilimo cha mahindi siyo mazao yote!

Ahsante

kny Dr Tulia
 
Dr Tulia hajamtaja Sugu bali ameilalamikia serikali!
Kwani nani alikuwa mbunge wa Mbeya na alifanya nini katika kipindi chake, narudia tena maana ya kutuma hizo salamu ni kuona wenzake wanavyofanya kazi na kuteteta Mbeya na si kutetea CCM,Sugu alitumia miaka mingi kuteteta SACCOSS yenu wakati haitusaidii kitu. Kama umesoma fasihi tena ya kidato cha pili ungeelewa ni kwanini nimeandika hivyo ,shida shule yenu ni kukalili hatua kwa hatua bila kufikiri nje ya box.
 
Japo napongeza mradi wa SGR lakini mpaka leo sijui ni kwanini waliamua reli ipitie kigoma na mwanza na sio nyanda za juu kusini. Mbeya ina border mbili, boda ya Tunduma kuingia zambia, zimbabwe congo na South Africa. Pia border ya Kasumulu kuingia malawi, na msumbiji kupitia ziwa nyasa. Hata mizigo ya transit inayopita 'corridor' hii ni mingi sana hasa ya zambia na Congo DRC.

Pili, mikoa ya mbeya, iringa, Njombe na Rukwa ina mazao mengi ya kilimo ambayo yatapakiwa kwenye treni ikiwa inarudi baada ya kupeleka mizigi. Kule wanalima mazao karibu mazao yote ikiwemo na dhahabu ya kijani 'parachichi.'

Miundombinu ya barabara kwa mkoa wa mbeya ni mbovu sana. Kwa miaka mingi mkoa ule ni kama unatengwa kimaendeleo. Haiwezekani Jiji kua na barabara kuu mbovu namna ile. Kwa kweli wafanye kitu cha ziada pale

Sent from my Android using JamiiForums mobile app
 
Kwani nani alikuwa mbunge wa Mbeya na alifanya nini katika kipindi chake, narudia tena maana ya kutuma hizo salamu ni kuona wenzake wanavyofanya kazi na kuteteta Mbeya na si kutetea CCM,Sugu alitumia miaka mingi kuteteta SACCOSS yenu wakati haitusaidii kitu. Kama umesoma fasihi tena ya kidato cha pili ungeelewa ni kwanini nimeandika hivyo ,shida shule yenu ni kukalili hatua kwa hatua bila kufikiri nje ya box.
Hayo ni yako wewe kajambanani!

Dr Tulia na bilionea Sugu hawana ugomvi wowote ndio maana Tulia amewazungumzia " wenzetu" lakini wewe unaleta ushabiki maandazi.

Ile CCM yenu ya " mashambani" siyo hii ya mama Samia bwashee.
 
Na je ya kati hakuna magofu na majengo kama vibanda umiza lakini wanajengewa treni ya umeme,kumbuka mikoa ya nyanda za juu kusini ndio zamani ikiitwa big 4 na sasa ni big 6, tunawalisha nyie wote, na tunalipa kodi zaidi hata ya hao ambao unawakingia kifua.
Iboresheni kwanza TAZARA kabla ya kulilia hiyo treni ya umeme.
 
Bora hata wangeililia watu wa kutoka Tanga, Kilimanjaro na Arusha! Ila siyo Nyanda za Juu Kusini! Maana hao wamejengewa treni ya kisasa kabisa ya TAZARA! Lakini wameshindwa kuishawishi Serikali kuiboresha ili iwe na tija.

Leo hii ukisafiri na treni ya TAZARA, utashuhudia tu magofu ya majengo kwenye stesheni zake, na huduma mbovu! Huku abiria na mizigo ikiwa ni ya kutosha tu.
TAZARA ni SGR ambayo haitumi umeme hivyo ni wakati sasa wa huyo Mbunge wa Mbeya kuhakikisha TAZARA inatumua umeme.
 
And so it begins..., or rather it continues....

Sisi na Wao......
 
Kipindi jiwe anapeleka miradi isiyo na idadi chato wala hakuyasema haya.

Zaidi walishangilia na kuunga mkono.
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣

ila niseme tu, Mheshimiwa Magufuli (r.i.p) nahisi alikuwa na kitu flani spesho sana....kama huku kwetu tungesema alimeza nyongo ya simba ambayo hufanya mtu aogopwe kupita kiasi. aisee aliogopwa yule mheshimiwa bwana tuache utani; hakuna hata aliyejaribu kufanya fyoko zaidi ya kushangilia tu kwa kila alilofanya au kusema!

kama si hivyo na kuogopwa kule kulisababishwa tu na uraisi wake, basi niseme uraisi tanzania una nguvu ya ajabu sana nae alijua vema kuzitumia nguvu hizo!!
 
Kuna treni ilikuwa inatoka Mtwara kwenda Ruvuma, iliishia Nachingwea na baadae iling'olewa yote. Nadhani sasa ni wakati muafaka wa kurudisha treni hiyo. Vipi Wabunge wa huko Kusini mbona mko Kimia? Ua kwa sasa hakuna uhitaji wa mawasiliano hayo?
 
Wakati mwenda zake anapeleka miradi ya kimaendeleo chato,uyo naibu spika akuwahi hata kukoroma zaidi ya kugonga meza na kupitisha miradi ya chato kwa kushangilia.
Alikuwa wapi kusema hayo wakati mwendazake anajenga uwanja wa ndege wa chato?!!hayo mabilioni ya chato mbona hakuyapigia kelele?!!
 
Mbunge wa Mbeya Mjini Dr. Tulia amemtaka Waziri wa Ujenzi kuangalia namna ya kuiwezesha TAZARA kuwa na treni ya umeme.
Dr. Tulia amesema Tanzania ni moja na Wananchi wa pande zote wanahitaji maendeleo hivyo Kanda ya Nyanda za Juu Jusini wamechoka kuwa washangiliaji.

Kadhalika Dr Tulia amelalamikia Jiji la Mbeya kutopewa hadhi na Huduma stahiki kama ilivyo katika majiji mengine na badala yake Mbeya imekuwa kama Halmashauri.

Tulia amesema miundombinu ya Mbeya ni mibovu sana na miaka yote wamekuwa wakipewa bajeti ndogo isiyokidhi chochote.

Dr. Tulia alikuwa akichangia hotuba ya bajeti ya Wizara ya Ujenzi.

Source: Bungeni
Enzi za mwendazake asingeweza kuongea haya, halafu anataka treni ya umeme kama wengine ni wengine wepi tz hii wana treni ya umeme?
 
Wakati mwenda zake anapeleka miradi ya kimaendeleo chato,uyo naibu spika akuwahi hata kukoroma zaidi ya kugonga meza na kupitisha miradi ya chato kwa kushangilia.
Alikuwa wapi kusema hayo wakati mwendazake anajenga uwanja wa ndege wa chato?!!hayo mabilioni ya chato mbona hakuyapigia kelele?!!
Kikwetu twasema 'ikupalamasya'. Anatapatapa na kupapasa ashike wapi.
Alikuwa wa Jiwe kwa jeuri na kiburi kilichowazi kabisa.
 
TAZARA ni SGR ambayo haitumi umeme hivyo ni wakati sasa wa huyo Mbunge wa Mbeya kuhakikisha TAZARA inatumua umeme.

..Tazara kiwango chake kinaitwa CAPE GAUGE RAIL au 1067 mm gauge.

..hicho ndicho kiwango cha reli za mataifa mengi ktk nchi za kusini mwa afrika / SADC.

..Reli mpya tunayojenga ni STANDARD GAUGE RAIL au 1435 mm gauge.

..hicho ndicho kiwango cha reli zote mpya zitakazojengwa na nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki / EAC.
 
Back
Top Bottom