Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,352
- 15,876
Dkt. Tulia ameyasema hayo leo tarehe 25 Aprili 2025 wakati akizungumza na wananchi wa wa Mkoa wa Pwani wakati wa Mkutano wa hadhara uliofanyika katika stendi ya Kibaha ikiwa ni sehemu ya shughuli za Maadhimisho ya Miaka 61 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mara baada ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo iliyofanyika katika mkoa huo.
“Tanzania haiwezi kuwepo bila Muungano, Muungano huu umejengwa katika misingi imara umedumu na utaendelea kudumu. Kila mmoja wetu anapaswa kutafakari matendo na maneno yake yawe chachu ya kudumisha Muungano wetu, niwahakikishie kwamba Bunge litaendelea kuwa daraja katika pande zote mbili ili kuhakikisha Muungano unazidi kuwa madhubuti, unadumu na kuwa imara zaidi” Amesisitiza Dkt. Tulia.