Jambo wanajf! Siku moja tulikuwa safarini na kati ya watu waliokuwa kwenye gari wakawa wanatia story kuhusu Dr Kieruu alivyouawa. Kwa kufupisha, walichoongea pale ni kwamba Dr Kleruu alipigwa risasi na mtu aliyeitwa Mamwindi alipokuwa shamba , na huyo Mamwindi akapeleka maiti ya Dr Kleruu polisi na kuwaambia 'chukueni mzoga wenu huo'. Kisa cha kupigwa risasi eti ni kutembea na mke wa huyo Mamwindi. Ninachoshindwa kuelewa ni kwa nini Dr Kleruu anasifika sana Tz mpaka kuna wimbo wa zamani kuna kisehemu unaimba '... Dr Kleruu, alazwe pema kiongozi wetu shujaa, mwanamapinduzi.....' Kama kuna mwenye uelewa tofauti naomba aweke mambo hadharani!