Mkuu kuna HOLOCUST kubwa mno inawamaliza wananchi wetu kila siku. Tofauti ni kwamba yenyewe tumeishaikubali kwamba iwepo tuu. Njaa, vita, magonjwa, umaskini nk..mi nadhani hiyo nayo ni holocust au genocide kabisa (ukiita ile ya Rwanda iliyomaliza watu million moja kwamba ni Genocide, je haya niliyoyataja hapa yanamaliza wangapi kwa mwaka?) sema tuu basi..tunaamua kutumia maneno pale tunapotaka ya-fit mawazo yetu. Bush akisema Iran, N Korea na Syria ni axis of evil..sisi tunasema Njaa, magonjwa na umaskini ndo axis of evil wa mwafrika!
gm said:Jokakuu,
Kama Nyerere alichukia adhabu ya kunyongwa angeiondoa lakini katika historia nafikiri sijakutana na sehemu inayosema alijaribu hata kuiondoa hii katiba, kama bunge lingegoma kupitisha angetumia executive power, sina uhakika kama katika katiba yetu tuna executive power ila nafikiri inawezekana.
But do we have executive power provision in our constitution?
gm,
..kwa upande mwingine inawezekana Mwalimu hakuchukua hatua kuifuta sheria ya kunyonga kwa kuzingatia hisia za wa-Tanzania. .
Mkuu you have made my day....... TANGU LINI VIONGOZI WETU WAKAZINGATIA HISIA AU MATAKWA YETU SISI WANANCHI?;-)
Jf imekuwa ni mahali pa kupashana habari na kuweza pia kuzungumzia mambo ya historia yetu na mwelekeo wa nchi. Kuna Huyu bwana anajulikana kama marehemu Dr Kleruu, mie nimekuwa nikimsikia katika wimbo wa Mbaraka Mwinshehe kuwa alikuwa mwanamapinduzi, Je kuna yeyote anaweza kutupatia taarifa kumhususu huyu Dr Kleruu alikuwa nani hasa na uana mapainduzi wake ulikuwa vipi katika historia na siasa za Tanzania?
Naomba kuweka swali lanyongeza hii inayoitwa Historia ya Tanzania imeanza lini Rasmi naoma kuelimishwa na kabla ya hapo ni kipi tunaweza kukiongelea naomba mchango utakao elimisha wengine kama mie...
Mwanzoni mwa miaka ya 1970 Mwamwindi alikabiliwa na shitaka la kumwua Dr Wilbert Kleruu, aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa kwa wakati huo.
Mshitakiwa Mwamwindi alijitetea kuwa alipokuwa anamwua marehemu Kleruu alirukwa na akili akapotewa na fahamu ya kuweza kuelewa kile alichokuwa anakitenda. Jaji Onyiuke alikataa hoja hiyo kwa kutilia maanani kwamba baada ya mshitakiwa kughadhibishwa ndipo alipokwenda ndani kuchukua bunduki ambayo aliitumia kumwua marehemu
Inasimuliwa, kuwa Dr. Wilbert Kleruu alifikia hata hatua ya kuanza kudhihaki makaburi ya mababu zake Mwamwindi akimwambia Mwamwindi: Humu ndimo mlimozika mirija yenu. Mwamwindi alikasirika sana. Akaficha hasira yake kutoka makaburini wakaongozana na Kleruu hadi nje ya nyumba yake. Akamwomba kiongozi huyo abaki nje, yeye akaingia ndani.
Mke wake Mwamwindi alimwona mume wake akichukua bunduki na kusimama dirishani. Mama huyo alidhani mume wake anakwenda kuwinda nguruwe. Kumbe, Mwamwindi alitokea dirishani. Mwamwindi akamlenga sawa kichwani Mkuu wa Mkoa na kumpiga risasi. Kisha akabeba mwili wa Mkuu wa Mkoa na kuuweka nyuma ya boneti ya gari alilojia mkuu huyo wa mkoa. Mwamwindi akaendesha gari hilo hadi kituo cha polisi Iringa. Akaripoti kwa kutamka; " Nendeni mkamchukue mbwa wenu nyuma ya gari!".
Tukio lile bado linatuachia maswali? Je, ni kwanini Dr Kleruu alikwenda nyumbani kwa Mwamwindi siku ya Jumapili?
Je, yawezekana Mwamwindi na Dr Kleruu walikuwa na ugomvi mwingine kabla ya tukio?
Waliopata kusikia simulizi zaidi ya tukio lile watusimulie.
kuiba mke wa mtu kumbe ni hatari hivyo!! Nasikia kuna mwanasiasa mmoja mashuhuri nae kaiba mke wa mtu hivi karibuni sasa kumbe anahatarisha maisha yake ki hivyo!kuna tetesi za kuibiwa mke na mkuu huyo.....ila kama ni kweli basi leruu alikuwa na moyo yaani waiba mke tena watembelea nyumba hiyo hiyo lol.....ila binafsi naamini mwamwindi alikuwa adui wa utekelezaji wa azimio la arusha...adui wa mipango ya maendeleo ya nchi ya kufikirika
mix with yours
Mwaka 1971 hadi mwaka 1972 kulikuwa na operesheni vijiji ambapo watu walitakiwa kuhamia kwenye vijiji vya ujamaa. Mwamwindi alikuwa mmja wa wale waliokataa kuhamia vijijini. Siku ya Krismas mwaka 1971 (au 1972 hivi), Dr. Kreluu aliwatembelea wale waliokuwa wamekataa kuhamia vijijini na ndipo alipokumbana na hiyo dhahama. Kwa vile Kreluu alikufa, mpaka leo haijulikani walikosana nini na Mwamwindi kwa vile maelezo ya mwamwindi yaliyopitakana wakati anajitetea na hakukuwa na mtu mwingine wa kuyathibitiha. Kesi ya Mwamwindi iliendeswa mwaka 1973 na alinyongwa mwaka 1974 huko Dodoma.