Dkt. Wilbert Kleruu - Utata wa kifo chake, historia na maisha yake

Dkt. Wilbert Kleruu - Utata wa kifo chake, historia na maisha yake

muuuuuuuuuh muuaji angekuwepo leo, hakika angemuua afisa elimun wa mkoa wa mbeya bwana JJK, MAANA NI MCHAFU KWA WAKE ZA WATU MIE SIJAONA
 
asant Paka mweusi kwa maelezo ya kina, wengine tulikuwa hatujui Historia hiyo. Kweli mkuu huyo alikosa adab lakini hakustahili adhabu hiyo.
 



Jana Jumamosi jioni nilikuwa na mazungumzo marefu na Bw. Amani Mwamwindi. Mstahiki Meya wa Iringa aliyemaliza muda wake. Huyu ni mwana wa marehemu Saidi Mwamwindi ambaye simulizi juu ya kilichotokea kule Isimani mwaka 1971 tumeifuatilia.

Bw. Amani Mwamwindi alikubali kufanya mazungumzo nami hiyo jana nyumbani kwake Mlandege hapa Iringa. Ni simulizi ya kusikitisha, kusisimua na yenye kutoa mafunzo. Inahusu pia maarifa ya uongozi na dhana nzima ya utawala bora. Naandika haya saa saba za usiku Jumapili. Ngoje nikapumzike. Baadae Jumapili ya leo nitaanza kuwasilimua niliyosimuliwa.

Kumekucha. Jumapili saa kumi na mbili asubuhi. Naanza kusimulia nilichosimuliwa;

Nimefika Nyumbani kwa Amani Mwamwindi. Ni majira ya saa kumi na nusu jioni. Ni nyumba ya kawaida sana katikati ya eneo wanaloishi watu wengi, karibu kabisa na soko. Ni kata ya Mlandege.

Nagonga mlango mkuu. Anayenifungulia ni Amani Mwamwindi.
” Karibu Bwana Mjengwa”. Tunafahamiana, tumewahi kukutana kabla. Miguuni hana viatu, amevaa soksi nyeusi.


Ananikaribisha kiti sebuleni. Anaagiza nilitewe kinywani. Naye anakaa kitini. Mazungumzo ya ana kwa ana. Kichwani najiuliza; unaanzaje mahojiano na mtu aliyefiwa baba yake kwa kunyongwa miaka arobaini iliyopita?

”Bw. Mwamwindi, pole sana kwa tukio lile la mwaka 1971. Mimi nimelifuatilia kiasi. Kuna simulizi nyingi mitaani. Nimeanzisha mjadala bloguni. Vijana wengi wanaonyesha kuwa na kiu ya kutaka kujua ukweli hasa wa tukio lile. Kwa vile uko hai, nikaona nikutafute tusikie kutoka kwako.”

Mwamwindi ananiangalia usoni.
” Alaa!” Anatamka. Kisha kinafuata kimya.

Nakumbuka, kuwa nimetoa maelezo ya utangulizi, sijauliza swali.
” Je, ni kweli kuwa Dr Kleruu alikwenda Isimani kwa marehemu mzee Mwamwindi kuhimiza suala la kilimo ndipo akakutana na kifo chake? ” Namwuliza kwa staili ya kurusha mshale bila kulenga hasa ninachotaka kupiga. Namjengea mazingira ya kuogelea katika kile anachokijiua. Na swali hili kwake analiona zuri sana.

” Swali zuri, umeuliza kama Kleruu alikwenda kuhimiza kilimo. Hapo ndipo lilipoanzia tatizo.”

Nakumbuka swali muhimu kabla hajaendelea.

” Mzee Mwamwindi, hivi ulikuwa na umri gani siku hiyo ya tukio?”
” Nilikuwa na miaka 21, na marehemu mzee alikuwa na miaka 42.”

Nauliza tena.
” Tunasoma kuwa ilikuwa siku ya Krismasi. Je, ilikuwa ni Jumapili au siku gani? Na wewe ulikuwapo nyumbani kwa mzee?”
” Ni kweli ilikuwa siku ya Krismasi, Desemba 25, 1971. Ni siku ya Jumamosi” Anajibu Mwamwindi.

” Turudi kwenye tatizo lilipoanzia” Namwomba Mzee Amani Mwamwindi.

” Kulikuwa na tofauti ya kimtazamo. Na ugomvi ulianzia siku ya Alhamisi, Desemba 23 kwenye ukumbi wa welfare pale Mshindo. Kleruu aliwakusasanya wakulima wakubwa wa Isimani. Nataka ujue kuwa Isimani ilikuwa na wakulima wakubwa sana na mmoja wao ni marehemu baba yangu. Mle ukumbini kulitokea malumbano makali sana baina ya wazee wale na mkuu wa mkoa Kleruu.

Wazee hakukubaliana na Kleruu kuwaita pale kuzungumzia kilimo cha eka mbili au tatu wakati wao kila mmoja ukubwa wa shamba ulianzia eka mia mbili. Na tayari walikuwa na ushirika wao. Mimi nikiwa na miaka 21 nilikuwa karani wa chama cha ushirika.

Siku ile Mzee alitoka kwenye mkutano ule na kuja nyumbani kwangu hapa tulipo, Mlandege. Akanieleza juu ya mkutano ule na jinsi walivyokosana kimazungumzo na Kleruu. Akaniambia, kuwa mle mkutanoni alimwambia Kleruu ni vema akawasaidia wale ambao hawajaanza hata kutembea kuliko kuhangaika na watu wenye uwezo wa kutembea na kukimbia. Na baba yangu hakwenda shule.


Kwenye Umoja wao wa wakulima wa Isimani, baba na wenzake walijipanga vema. Walishaanza kuzungumzia haa uwezekano wa kumlipa mwanasheria, hata kama ni wa kutoka Uingereza, aje kuwatetea katika uovu ule wanaotaka kufanyiwa. Hawakukubaliana na utekelezaji wa sera za Ujamaa kwa staili ile aliyotaka Kleruu. Kuingia kwenye ushirika na wengine wakati wao walishaanza zamani. Fikiri, wao walifyeka mashamba yao tangu miaka ya hamsini. Hoja yao ni kuwa mapori yalikuwa hayajaisha kwa wengine kwenda kufyeka na kulima. ” Anazungumza Mzee Mwamwindi. Anaonekana kuwa na mengi sana, na hamu ya kusimulia zaidi. Nabaini pia, kuwa kwake yeye mkuu yule wa mkoa ni Kleruu na hamtaji kama ' Dr Kleruu'. Namwacha aendelee.

” Sasa baada ya ile alhamisi, mzee akashinda Ijumaa. Jumamosi ikawa siku ya Krismasi. Kwa vile wafanyakazi wake wa shambani walikuwa mapumziko ya krismasi. Na yeye ni mwislamu, na alikuwa mchapa kazi kweli, basi, alikwenda shamba lake la jirani akiwa na mdogo wangu, sasa ni marehemu, anaitwa Mohamed. Wakawa wanalima kwa trekta.

Siku hiyo Kleruu, pamoja na kuwa ni Mkristo, aliamua kutokula Krismasi. Alivaa kofia yake ya pama. Inaaminika alibeba pistol yake pia. Kleruu akaendesha mwenyewe gari lake la mkuu wa mkoa aina ya Peugeot Injection, rangi ya bluu. Katika orodha yake, Kleruu alikuwa na watu watatu wa kuwashughulikia miongoni mwa wakulima wale wakubwa wa Isimani. Target nambari moja alikuwa Bw. Rashid Juma wa Nyangólo. Nambari mbili ni marehemu baba. Namba tatu simjui.

Kleruu alipofika Nyang’olo hakumkuta mkulima Rashid Juma. Siku hiyo ya Krismasi Rashidi Juma alipata habari, kuwa kuna ng’ombe wake walipotelea milimani. Alikwenda huko milimani kusaka ng’ombe wake. Hivyo, Kleruu akafunga safari kurudi kwa target namba mbili, baba yangu Mzee Mwamwindi. Ni njia hiyo hiyo, Nyang´'olo iko mbele ya ilipokuwa ngome ya mzee.” Anasema Mwamwindi akionekana kuzama katika simulizi inayomgusa. Nami namsikiliza kwa makini.

”Basi, Kleruu akafika kwa Mzee. Baba akiwa shambani akaliona gari la Kleruu limesimama nje ya mji wake. Kisha akamwona Kleruu akitembea kumfuata shambani. Baba alihisi tu, kuwa Kleruu amekuja na shari.

Kleruu akamwuliza Mzee kwa ukali, ” Mbona mnafanya kazi leo siku ya Krismasi?”. Baba akamwomba Kleruu waende wakuzungumze nyumbani. Akamwambia mdogo wangu Mohammed aendelee kulima. Mzee akatangulia mbele, nyuma anamfuatia Kleruu. Kabla ya kufika kwenye nyumba yake wakayapita makaburi. Kleruu akamtamkia baba mzee Mwamwindi; ” Hapa ndipo unapozika mirija yako?” Alitamka hivyo huku akimtomasa tomasa mzee na kifimbo alichoshika mkononi.

Jambo hilo lilizidi kumkasirisha marehemu mzee. Akafika nyumbani kwake. Mlangoni alisimama mke wake mdogo. Inaonekana mzee alishafanya uamuzi. Jana yake alikwenda kuwinda. Hakupata mnyama. Bunduki yake moja aia ya riffle kati ya bunduki zake mbili ilikuwa bado ina risasi. Akamwambia mke wake mdogo huku Kleruu akiwa anasikia;
” Kanichulie bunduki yangu”…… ( Simulizi hii inaendelea baadae. Jamani, Jumapili leo, nipumzike kidogo!)
SOURCE BY Brother Maggid Mjengwa.
 
Naona wazee wa Kinyalu huwa hawapendi dharau kabisa, pia ni fundisho kwa wanasiasa wanaoacha kufatilia wenye shida na kufatilia maisha ya watu waliojiinua kwa nguvu zao wenyewe.
 
Maggid, siku nyingine unakuwa kama chizi vile .... .... sifikirii kama wahehe wangekuwa na tabia kama yako wangeweza kuwapiga wajerumani.
 
Maggid endelea na hiyo hadithi yako, kwa kweeli wengine tunaikumbuka hiyo ya Mwamwindi ijapokuwa tulikuwa wadogo tuko primary siku zile.

Ilikuwa ni hadithi ya kusikilizwa kwenye radio ambayo ilikuwa inatangaza inavyopenda wenyewe. Sasa tunautaka ukweli ulivyo.
 
Kleruu alikasirika kwa sababu Mwamwindi alikuwa anafanya kazi siku ya Christmas. Huyu Kleruu alikuwa mdini.
 
hapo Maggid umechemsha, yaani tungojee mpaka lini? si ungepost habari baada ya kupumzika ?
 
Msaada Hivi DR. KLERUU alikuwa ni nani? na alifanya mambo gani katika nchi yetu? Je ni kweli aliuwawa?
 
yap ndio aliuwawa na mkulima mmoja siku ya krismas hukom ismani, iringa huyu jamaa alikuwa mkuuu wa mkoa.
 
Aliuawa na mr Mwamwindi alikmkuta shambani kwake akilima na tractor lake.akiwa mkuu wa mkoa wa Iringa mwenye itikadi kali ya kishoshalist toka urusi na akihimiza vijiji vya ujamaa.ilitokea kuto kuelewana na jamaa akampiga risasi ,inasemekana alitaka kumnyang'anya mashamba yake ili ayagawe yawe yakijamaa ndipo walipotibuana.kisha baada ya kumwua alimpeleka yeye mwenyewe mpaka Polisi katika gari la mkuu wa mkoa enzi hizo pijo 404 station wagoni.pia inasemekana kati ya watu wawili ambao rais Nyerere aliidhisha wanyongwe mpaka kufa mwingine ni mhindi mmoja wa Songea ambae alimwua mkewe ili apate bima ambayo alikuwa ameikata.na kisa cha mwamwindi kunywongwa ilikuwa kuwaadabisha wahehe ambao kama angeachiwa ingepelekea kujiona kuwa ni watu wenye hasira nyingi sana kumea zaidi ktk vichwa vyao.
 
Thanks a lot nilikuwa namsikia sijui chochote wala hakuna kitabu kinachomwelezea huyu jamaa
 
Mjengwa kafanya mahojiano na mwanae aliyempiga risasi Dr. Kleruu I believe, check it out mjengwa
 
Yule mzee aliyemuua alikuwa kapinda imagine aliupeleka mwili wa marehemu mwenyewe polisi na kuukabizi
Ila nae RC alikuwa amezidi nasikia alikuwa anawachalaza watu bakora
 
..Mjengwa ameandika sehemu ya pili ya kisa hiki.

..kwa kweli inasikitisha, lakini zaidi inatisha.
 
weye lazma Muunguja au Mpemba! sasa Kleruu mbona naye alikuwa kazini Chrismas?

Kwenda kumnyanyasa mtu ni kazi pia?
Refer to history, haya ndio maneno aliyoyasema Kleruu
” Mbona mnafanya kazi leo siku ya Krismasi?”
 
kleruu alikuwa mchaga nini? afu krismass yote hiyo hakwenda moshi?:A S crown-1:
 
Siku hiyo Kleruu, pamoja na kuwa ni Mkristo, aliamua kutokula Krismasi. Alivaa kofia yake ya pama. Inaaminika alibeba pistol yake pia. Kleruu akaendesha mwenyewe gari lake la mkuu wa mkoa aina ya Peugeot Injection, rangi ya bluu.


Bunduki yake moja aia ya riffle kati ya bunduki zake mbili ilikuwa bado ina risasi. Akamwambia mke wake mdogo huku Kleruu akiwa anasikia;
" Kanichulie bunduki yangu"……

Hizo sehemu nilikokoleza wino mbona kama zinanichanganya. Hivi Inawezekana kweli Kleruu pamoja na kuwa na Bastola asubiri mke wa huyo jamaa aende ndani na kumletea bunduki mumewe bila ya yeye kuitumia bastola yake kuzuia hilo?

Ningetamani sana kusikia pia kutoka upande wa pili......
 
Back
Top Bottom