Dkt. Wilbroad Slaa asema zuio la maandamano sakata la bandari ni kinyume cha sheria

Dkt. Wilbroad Slaa asema zuio la maandamano sakata la bandari ni kinyume cha sheria

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
Dkt. Slaa: Leo naomba kuzungumza nanyi kidogo kwa mujibu wa katiba yetu ibara ya 20. Nina taarifa kwamba kesho asubuhi majira ya saa mbili vijana wataandamana kutoka Temeke kwenda kukabidhi maoni yao, hoja zao, kwa mpendwa Rais wao kule Magogoni.

Vijana hao ambao wanaandamana walipeleka barua yao polisi kama mujibu wa Sheria ya Jamhuri ya muungano inavyotaka, nafahamu kwamba mkuu wa polisi kanda maalum ametoa taarifa lakini taarifa yake hiyo ni kinyume na sheria za Tanzania na kwasababu hiyo vijana wameona wanaendelea na maandamano yao.

Mimi naomba kuungana nao na naomba wananchi mjitokeze kwasababu kwa mujibu wa katiba yetu ibara ya 27 ibara ndogo ya kwanza na ya pili ni wajibu wa kila mtanzania kulinda rasilimaliza nchi yetu.

Inapendeza sana kuona watanganyika wameamka kudai mali yao iliyoporwa kwa uzembe wa mtawala, licha ya jitihada za vyombo karibia vyote vya habari kutaka kulizima hili suala la bandari na ule mkataba wa kinyonyaji.

Kitendo cha polisi kuyazuia hayo maandamano kwanza wanazidi kumharibia msaliti aliyetutoa sadaka kwa wajomba, afadhali wawaache waandamanaji wapeleke ujumbe wao sehemu stahiki, lakini kinyume cha hapo, ndio polisi wanazidi kutuonesha vile msaliti alivyotupeleka utumwani kwa kukusudia.
 
Sidhani kama tunaweza kufanikiwa Kwa kutumia ubabe ukianza kujiona kwamba hakuna mtu wa kukubabaisha wewe ni Mkuu juu ya Wakuu jaribu ujitafakari Sana.

Maisha ni mafupi MWILI WA Binadamu ni minyama minyama ambayo haihitaji misukosuko,Haki zipo lakini pale zinapoanza kuingilia haki za mwingine huwa zinakoma.

Kumbuka haki ya kuandamana IPO kinachotakiwa usivunje sheria za nchi.

Yangu macho nasubiri nione Nani mbabe au ndiyo tutahamisha agenda ya kuomba tuonewe huruma oooh! Hatukuwa na silaha,tumepigwa bila sababu nk. KESHO kutwa tutaandamana kupinga mabomu yasitumike.
 
he huyu mzee yupo.hakika tanzania tuna watu wa ovyo sana.Na wepesi kusahau.huyu mzee hakustahili hata kuongea
 
Dkt. Slaa: Leo naomba kuzungumza nanyi kidogo kwa mujibu wa katiba yetu ibara ya 20. Nina taarifa kwamba kesho asubuhi majira ya saa mbili vijana wataandamana kutoka Temeke kwenda kukabidhi maoni yao, hoja zao, kwa mpendwa Rais wao kule Magogoni.

Vijana hao ambao wanaandamana walipeleka barua yao polisi kama mujibu wa Sheria ya Jamhuri ya muungano inavyotaka, nafahamu kwamba mkuu wa polisi kanda maalum ametoa taarifa lakini taarifa yake hiyo ni kinyume na sheria za Tanzania na kwasababu hiyo vijana wameona wanaendelea na maandamano yao.

Mimi naomba kuungana nao na naomba wananchi mjitokeze kwasababu kwa mujibu wa katiba yetu ibara ya 27 ibara ndogo ya kwanza na ya pili ni wajibu wa kila mtanzania kulinda rasilimaliza nchi yetu.

Ifike wakati sasa ieleweke

Nchi hii ni mali ya genge fulani la watu na sisi wengine ni wapangaji, Katiba ipo ila kinachopewa kipaumbele ni kutetea maamuzi batili ya viongozi ambao nao wanafanya mambo kwa kubahatisha, wanaposhauriwa wanatafsiri ushauri kama attack na ku react kwa kutumia vyombo vya dola
 
Mimi nashauri yeye akae safu ya mbele kabisa sio awashawishi wananchi alafu yeye asemee mitandaoni.
Huyo anayeuza hiyo bandari naye ajitokeze akae mbele ili kuwazuia waandamanaji, asitumie vyombo vya dola kuzuia waandamanaji. Hayo ni maandamano ya amani kuzuia mali za watanganyika kuuzwa na Mzanzibari.
 
Back
Top Bottom