DNA Test

DNA Test

Inkoskaz

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2010
Posts
6,361
Reaction score
2,378
Hili jambo haliishi kunishangaza... ni vipi madai mengi ya DNA ni ya wababa kukataa watoto na si wababa kudai watoto?
Je ni kukwepa majukumu ama kutowaamini wanawake?
au ni aibu kwa kupata mtoto kwa mzazi mwenza asiyetarajiwa?
ama ni kisasi cha ugomvi wa baba na mama bila kumjali mtoto aliyezaliwa?

inanikumbusha mzee wetu mahita ,kipimo kagoma,mtoto anavyozidi kukuwa masikio ndiyo yanazidi kurandana lakini mzee anakomaaa kukataa kisa kazaa na housegirl au?

mnaoguswa na hili hebu tusemezane ukweli upo wapi
au ndo ile kusema mama ndo ajuaye asili ya mwana baba yake malezi?
 
Tatizo ni watu kuthamini sana kuwa biological father kuliko mlezi, mimi naona mlezi yule anayegharamikia malezi ya mtoto ni bora na anafaa na huyo ndio ana sifa ya kuitwa baba.
 
Yote ni majibu mpendwa ila kubwa kuliko ni hilo la kukwepa majukumu.
Wapo wazee wengine wanataka wanawake walee tu wao waje wafaidi matunda b'dae.
Inaumiza sana hii, naomba yasinikute.
 
Majukumu na pia kufikiria wamebambikiwa na aibu (kundi la kina mahita hili).

Wakuu kama tunafikiri hatupo tayari kuwa wazazi bora tujikinge kuliko kuwatesa watoto kwa kupata malezii ya upande mmoja tu.
 
Mkuu wengi wao wanakataa maana hiyo kitu huwa inatokea ghafla bila kutegemea na pengine kukataa majukumu...lakini nilishasema siwezi kuja kuikataa damu yangu kama najuwa ni mimi ndio mwenyewe...zaidi kama nina wasiwasi kama ulivyosema DNA inafanya kazi!!
 
Hilo la Mahita hata mimi linanishangaza sana kwani huwezi sema anakwepa majukumu kwa vile si masikini, sijui kuna niini nyuma ya pazia kwa issue ya Mahita

Kuhusu kukataa watoto kwa Wababa, pamoja na sababu zingine, mimi nadhani hizi takwimu za vyombo ya habari na utafiti vinavyoonyesha wababa wengi wamebambikiziwa watoto ndio nayo inachangia Wanaume kuingia hofu na kuanza kuhisi tu kuwa pengine na yeye kabambikiziwa.

Hivi hao wanokwenda kwenye hizo wanaita sijui "sperm bank/donnor" wao inakuwaje, wale wanaotoa sperm wanatambulika kisheria kuwa baba halali wa mtoto au kwenye cheti inaandikwa mtoto hana baba!!!?

Mimi nipo tayari kuwa baba mlezi lakini sipo tayari kuaminishwa kuwa mimi ni biological father wa mtoto wakati si kweli.
 
Wanaume kwenye swala la kukataa watoto mnahitaji ukombozi kwa kweli. Sioni sababu ya Msingi lakini daaaa inauma umemzalisha house girl afu unakataa huyo sio mtoto wako. Sasa kwa nini aseme ni wewe??

Duuuuuuu, mioyo ya wanaume sijui iko je, halafu mjue kabisa hilo nalo ni sababu kubwa ya wadada wengi kutoa mimba sasa unaingia kwenye ndoa na kilio cha damu ya watoto wawili mpaka wa nne achilia mbali hao mabinti uliowaumiza halafu ndoa iwe na amani kweli. Matatizo mengine kwenye ndoa yanasukumwa na laana ya maovu kama haya ya kumwaga damu zisokuwa na hatia. Tubadilike na tutubu.
 
Mkuu wengi wao wanakataa maana hiyo kitu huwa inatokea ghafla bila kutegemea na pengine kukataa majukumu...lakini nilishasema siwezi kuja kuikataa damu yangu kama najuwa ni mimi ndio mwenyewe...zaidi kama nina wasiwasi kama ulivyosema DNA inafanya kazi!!

hapo wanaume ni wivu tu anaona mwanamke waliyeachana ana mpenzi mwingine lakini anasahau kuwa aliyepanda mbegu ikaota ni yeye
 
Mimi nadhani inategemea pia na sababu ya kukataa au kuwa na wasiwasi. Mara nyingine kuna sababu za msingi tu...na takwimu/uzoefu unaonesha zipo incedence nyingi tu za kubambikiwa watoto.

Ni kweli mtoto ana haki ya kupata malezi ya 'wazazi' wote wawili lakini hii ni lazima iende pia na haki ya baba kujua ukweli kama huyo anayemlea ni mtoto wake ama la. Kuna kina baba wengi tu wanalea watoto ambao sio wao hata baada ya kugundua ukweli huo. Nadhani cha muhimu ni ukweli na uwazi.
 
yani umepima dna majibu yanaonyesha mtt ni wako bado unakataa majibu au? maana ss kwetu akuna cha dna tunasemaga kitanda hakizai haramu so ukiambiwa huyu mtt wako ni dna tosha unaanza kulea bila kinyongo
 
Ni aibu kwa Mzee aliyekuwa na cheo kama Mahita kuchakachua na kahouse girl. Ndiyo mana amebaki kukataa hata kama DNA imemdhihirishia kwamba ni baba wa mtoto.

Vile vile nadhani alikuwa anaogopa kugraduate title ya ufataki.

Mzee Mahita asimkatae huyo mtoto damu yake hwenda ndiye ataekuja mfaa huko mbele.
 
Hili jambo haliishi kunishangaza... ni vipi madai mengi ya DNA ni ya wababa kukataa watoto na si wababa kudai watoto?
Je ni kukwepa majukumu ama kutowaamini wanawake?
au ni aibu kwa kupata mtoto kwa mzazi mwenza asiyetarajiwa?
ama ni kisasi cha ugomvi wa baba na mama bila kumjali mtoto aliyezaliwa?

inanikumbusha mzee wetu mahita ,kipimo kagoma,mtoto anavyozidi kukuwa masikio ndiyo yanazidi kurandana lakini mzee anakomaaa kukataa kisa kazaa na housegirl au?

mnaoguswa na hili hebu tusemezane ukweli upo wapi
au ndo ile kusema mama ndo ajuaye asili ya mwana baba yake malezi?

Thanks for bringing out this one. Let me reserve my comment b'se it really hurt. Anyway big up to my mom who stood up for me, and made me who I am today.
 
Hii sema Mahita hakuicheza vizuri. Lakini kuna wazee wengi na vyeo vyao wanakataa watoto wao hivyo hivyo. Ila wanajua kula na kipofu ndiyo maana issue zinakuwa kimya. Jamani msikatae watoto wenu hamjui nini Mungu amewapangia huko baadae. Wakifanikiwa mnaanza huyo mtoto damu yangu bwana, wakati akiwa mdogo mlimkataa.
 
Hili jambo haliishi kunishangaza... ni vipi madai mengi ya DNA ni ya wababa kukataa watoto na si wababa kudai watoto?
Je ni kukwepa majukumu ama kutowaamini wanawake?
au ni aibu kwa kupata mtoto kwa mzazi mwenza asiyetarajiwa?
ama ni kisasi cha ugomvi wa baba na mama bila kumjali mtoto aliyezaliwa?

inanikumbusha mzee wetu mahita ,kipimo kagoma,mtoto anavyozidi kukuwa masikio ndiyo yanazidi kurandana lakini mzee anakomaaa kukataa kisa kazaa na housegirl au?

mnaoguswa na hili hebu tusemezane ukweli upo wapi
au ndo ile kusema mama ndo ajuaye asili ya mwana baba yake malezi?

Mkuu,

Ni very simple logic,

Kwa mwanamume yeyote, "not every ejaculation deserves a name"! Kwa inataka moyo kama wewe ulijua yaliisha baada ya ngono kumbe kuna mambo ya kujenga historia na ukoo! Ni jambo gumu sana kwa wanaume.

Katika hili suala watu wanahitaji ushauri nasaha wa nguvu sana!
 
ni ukosefu wa imani na kutokuwa na utu, majukumu ya mtoto atatupiwa mama bila ya mwanaume kujali nini vibaya.
 
Majukumu na pia kufikiria wamebambikiwa na aibu (kundi la kina mahita hili).

Wakuu kama tunafikiri hatupo tayari kuwa wazazi bora tujikinge kuliko kuwatesa watoto kwa kupata malezii ya upande mmoja tu.
Na hili ndilo la msingi,kwa nini umzalishe binti wa mtu na umkatae mtoto yeye ampeleke wapi kiumbe hicho?kama unaona haupo tayari kulea kwa nini usitumia kinga?acheni wanaume kutesa watoto!juulize wazazi wako wangekufanyia hivyo ungekuwa nani sasa hivi!wanaume tuwe na huruma
 
Hili jambo haliishi kunishangaza... ni vipi madai mengi ya DNA ni ya wababa kukataa watoto na si wababa kudai watoto?
Je ni kukwepa majukumu ama kutowaamini wanawake?
au ni aibu kwa kupata mtoto kwa mzazi mwenza asiyetarajiwa?
ama ni kisasi cha ugomvi wa baba na mama bila kumjali mtoto aliyezaliwa?

inanikumbusha mzee wetu mahita ,kipimo kagoma,mtoto anavyozidi kukuwa masikio ndiyo yanazidi kurandana lakini mzee anakomaaa kukataa kisa kazaa na housegirl au?

mnaoguswa na hili hebu tusemezane ukweli upo wapi
au ndo ile kusema mama ndo ajuaye asili ya mwana baba yake malezi?

source please!unazungumzia data za wapi?Tanzania,UK,USA au duniani.
 
Tatizo ni watu kuthamini sana kuwa biological father kuliko mlezi, mimi naona mlezi yule anayegharamikia malezi ya mtoto ni bora na anafaa na huyo ndio ana sifa ya kuitwa baba.

Mkulu
Salute, salute nyingi sana.
Nitakuheshimu sana kuanzia sasa kwa mtazamo huu.
Umeitendea haki pseudo-name yako Mkulu...salute...tazama nimekubonyezea thanks hapo
Big up.
 
kaka hapa tunazungumzia tz,but in general it hapens almost all over the world
 
Back
Top Bottom