Do you feel LOVED?


kweli kabisa mkuu unayoongea,mm niko mbali na mke wangu yapata mwaka sasa ila tunaaminiana sana na sina wasiwasi nae ata kidogo na yy pia hana wasiwasi na mm coz hatukuoana kwa bahati mbaya ni kitu ambacho tulipanga na tukalidhika sote na kila mmoja aliona kuna sababu ya kuwa pamoja na tunawasiliana kila siku inayopita kwa msg na kuongea nahisi kama tuko pamoja maana tunashare kila kitu same toka kuamka mpaka kulala!sina sababu ya kuwa na wivu coz najiamini.
 

mkuu naona umenisoma sana na umechambua haswa kile nilichomaanisha,hii imenigusa sana kumtima ahsante kwako,asha dii,gaga na wengine wote zidumu fikla za wana jf
 
Saying “I Love you”
Ukimwambia I love you… anakujibu “Thank you” OR kutumia phrases za kijanja kama “I love the way you say you love you” na kuishia hapo na kukupotezea (the good thing ni kua at least s/he is frank…lol)

Sometimes inatokea kwangu,akiniambia "i love you"
naishia kusema "me too"!!!!
Sio kwa sababu simpendi,ila sometimes unakua umechoka,
hujisikii kuongea chochote na yeyote ndo yanakuja hayo "i love you"

Na the thing inanichosha sana ni "i miss you",...ambayo utarudia kusema "i miss you too"
kwa siku unaweza ambiwa mara 10,inachosha na nikichoka kuisikia unaweza dhani sikupendi.

Kutumia maneno ya aina ileile mara nyingi inachosha,...creativeness inapalilia mapenzi
 
...mizani ya mapenzi. Katika siku 30 kila mwezi, au siku 365 za mwaka, mwenza wako anatumia muda gani ku behave namna hiyo?...inawezekana ni circles/phase mbali mbali tofauti za mapenzi i.e, motomoto, vuguvugu, au baridi...
 
<br />
<br />
Safi sana,unajua binadamu tumeharibu uhalisia wa mambo mengi na tunatafuta sababu ya kuyahalalisha!God help us!
 
AshaDii.. Thanks for the post..Nimeikubali.. Tunashukuru umetukumbusha wajibu wetu!! Nami naomba niweke machache..

At glance..

Mawasiliano..
Naamini mawasiliano ni translation ya kwanza ya Human Feelings and Reaction. Naamini jinsi gani tunavyopeleka message kwa wapenzi wetu ndio tunaonyesha jinsi gani tunavyowapenda. Binafsi sipendi artificial feelings na Lugha za ki-uwongo toka kwenye video na magazeti..yaani “darling” ya uwongo ya kila mara.. Napenda kusikilizwa na kusahihishwa. Lakini kama Mwanaume nina kasumba yangu ya uanaume yaani inabidi Mama amwage data ili nikubaliane na ushauri wake.. Lakini mara kwa mara napokubaliana na ushauri wake nadhani nae anajisikia kupendwa. To be loved ni kusikilizwa, to be loved ni kuheshimiwa na to be loved ni kusahihishwa pale unapokosea na sio kuogopwa kwa sababu wewe unaleta mkate na chakula nyumbani..Mapenzi ya woga ni sumu ya maisha.


Ushirikiano…
Katika ushirikiano.. To be loved ni pale mwenzako anapokuamini. Utakuta watu wanajenga hadi nyumba inafika juu lakini mwenzake hajui.. Wengine hawajui hata Payroll ya baba ikoje? Mnasema eti mnapendana… Mtapendana vipi bila kuaminiana? Yaani kila mtu mshahara wake anaujua mwenyewe.. Kama mnafichana payroll ..mtawezaje kupanga bajeti ya nyumba? Kama unamficha mpenzi wako Investments zako..Ukifa unataka nani afuatilie? I believe, Kama mtashirikiana katika mambo ya uchumi na jamii, mtaweza onyesha what is really love..kwani mapenzi ni kuaminiana .. Mapenzi ni Sacrifice yaani usiogope kumwonyesha vitega uchumi vyako kwa mke wako hata kama ni mtani wangu wa jadi toka kule Machame, Moshi..Mwamini kwa sacrifice..litakalotokea na litokee.. Mungu yupo!

Sweet Haven…
Kumkaribisha mpenzi wako kwako hata kama ni jalalani maana yake ni kujifunua. Maana yake umemwamini nae aone uko vipi. Mara nyingi nyumba inaficha siri nyingi. Tabia ya mtu utaijua nyumbani. .. Msafi.. Mchafu… mkarimu kwa majirani.. Ni kweli..To be loved ni kujivua gamba la kwenda hotelini na kujikita nyumbani kwako hata kama kuna panya, viroboto, na uswazi! Home sweet heaven..Ukifanya hivyo mpenzi wako atakupenda jinsi ulivyo na wala sio kama alivyokuona siku ile pale Kilimanjaro kempinski..

Jealousy….
Watu wanasema wivu ni dalili ya mapenzi.. Binafsi napinga. Utawekaje wivu kwa binadamu ambaye hujui ndani ya moyo wake anafikiri nini. Utafikiri vipi kuwa mimi nin-cheat wakati kama nin-cheat siwezi kukwambia? Wivu ni waste of time na psychological torture. Kama hujui..sahau!

Material Needs…
Chochote mnachotumia pamoja ni chenu..lakini kama mmoja anampiga “mzinga” mwenzake kila mara.wakati anazo ..hizo ni dalili mbaya za kwamba hakuna mapenzi ya kweli zaidi ya kutoaminiana.na biashara. Kama mnapendana ..au to be loved ni kuwa..kabla hajaomba utajua anataka na hana msaaada!


Name Calling…
Inategemea mnaishi mazingira gani na mmekulia katika mazingira gani.. Nenda kwa Morani kwa kimasai na shujaa halafu mwite “baby”.. atasema..aisee mama nanii inaita mimi toto..ni dharau.. Nenda kwa mmasai huyo huyo aliyezaliwa na kukulia kule sehemu sehemu ..ambako wanaitana “baby” yaani atafurahi ukimwita “baby”.. To be loved ni kuitwa vile unapenda wewe.. na si vile kama inavyoandikwa kwenye kitabu..

Public appearances…
Ukiona mpenzi wako anakukimbia ..basi ujue hapo hakuna mapenzi ila biashara! Kama wewe ni “kibosile” umesoma na mke/mume/Partner wako ni maimuna toka shule za kanumba.. Kama ukiweza kumchukua kwenda katika minuso ya vibosile....na ukamtambulisha na kumwambia huyu ni mke wangu..Yaani atajisikia..kuthaminiwa, kuaminiwa, na kupendwa.. Public appearances ni translation ya vitu hivyo..Thamani ya mtu, uwazi, na kujiamini..Ukiona mtu anakwepa public appearances..hujue anakwepa hivyo nilivyosema hivyo wewe tafuta mlango uliowazi na uondoke..
 
People may refuse our love,or reject our message but...........
 
 
Hahaha!!! Lol sipati picha
 
Thanks AshaDii love for sharing this,

Nimesoma kila post so far, hasa SteveDii (sijui ameshamoata yule mchumba akimtafuta hapa) Gaga, Klorokwini, tatizomuda, Chauri, Eiyer na wengineo

Naona tu kuna kipengele ambacho bado kipo contentious:WIVU

For wengine wanaona kuwa wivu haufai, wwengine wanaona wivu kama chachu ya mapenzi

I understand kuwa tumeshajadili sana role ya wivu kwenye mapenzi na hata kuitofautisha na ghubu nk

Lakini kwa upende wangu nadhani wivu wa kiasi ni muhimu...na sio lazima eti ionyeshe kuwa hujiamini au humpendi mwenzi wako..hapana...mi nadhani its something that comes NATURALLY unapompenda mwenzako KIUKWELI. Kwa sababu mapenzi ya ukweli huwa na some degree of possessiveness, kutaka chako kiwe chako peke yako, lakini pia kikitaka chako kisjisikie kuwa ni chako na kipo protected (nadhani kina dada/mama hapa mnanipata).

Nashawishika kuamini kuwa hata wanyama, pamoja na kunyimwa utashi, wana "wivu" wa aina yao ndo maana kuna usemi 'mafahali wawili hawakai zizi moja"...tumeshajiuliza, kama anavosisitiza SteceDii, chanzo cha msemo huu?

Kwa hiyo, penye mapenzi ya kweli hapakosi wivu,suala ni kuangalia tu kwamba wivu suifike kwenye hatua ya Ghubu......maana hiyo sasa inakuwa sio mpango.

Ni hayo tu kwa sasa

Love leo nikitoka tu job nakuja na surprise moja ivi, sikwambii sasa hivi lol
 
Well this means something, nakubaliana na wewe Kaizer kwamba it's something that comes naturally tu
 
kuna mtu aliimba
heri niwe peke yangu mama .......+
heri niwe peke yaaangu...... Inabidi ifike mahali kila mtu aheshimu status yake kwenye mahusiano
huwa sioni sababu ya kumngangania mtu? Kama penzi alibalance sio penzi ilo.

Bebii!!! safi sana hakuna sababu hata moja ya kung'ang'aniana hata kidogo bora kuachia ngazi na kusonga mbele.
 
And then the girl asks her mother: What is love?

Mother: Love is a lie invented by men so that they can have sex with you for free

What ???!!!1
Siamini hili
Love is a lie invented by men so that they can have sex with you for free
Hapana siamini hapa
 
huamini? Ndo ivo sasa?
 
huamini? Ndo ivo sasa?

bebii nikikuuliza what is love kwa maelezo yako wewe
hiyo definition oya huyo hapo juu sio kweli bana
kwani nikikupenda ndo nitakuwa na sex free
je kukutoa out, kukununulia msosi, viwalo, gharama za lodge, pesa kidogo za matumizi sio gharama kweli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…