Doctor kakimbia mji baada ya kunusurika kuuawa na aliyekuwa mke wake

Doctor kakimbia mji baada ya kunusurika kuuawa na aliyekuwa mke wake

DeepPond

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2017
Posts
41,728
Reaction score
103,997
Kuna jamaa mmoja ni mzaliwa wa huko Kusini alikuwa anasomea mambo ya udaktari ktk chuo fulani cha private hapa hapa Dar.

Kama mjuavyo hulka za vijana vyuoni, jamaa mwishoni mwishoni anamaliza akaja kuingia kwenye mahusiano ya kimapenzi na binti mmoja wa mzaliwa huko Kaskazini aliyekuwa anasomea mambo ya unesi Ila kwa ngazi ya certificate.

Hawakukaa Sana,
Pale chuoni zikabandikwa ratiba na taratibu kwa wanafunzi watakaohusika Kwenda field na wale wanatakiwa kwenda internship.

Kwamba Kama una sehemu unapafahamu iwe serikalini au private na unataka Kwenda kufanyia field au internship yako pale. Basi Wasiliana na uongozi wa chuo wakupe barua rasmi ili ukatume maombi mapema.

Sasa uyo mpenz wake akamshauri jamaa kua kwakua internship ya jamaa ndo itatangulia afu field ya wanafunz wa certificate ndo itafata. Basi Kama itawezekana jamaa atume maombi yake ya intern kwa Taasisi za mkoa wa kaskazini ili iwe jiran na kwao binti ili waweze kua karibu zaidi waenjoy kipind chote Cha field na intern.

Jamaa akakubali Ila changamoto akasema Ni Hana connection wala ndugu yyt kule kaskazini.
Binti akamwambia kua kule ndo nyumbani kwao na anafahamiana madaktar na manesi wengi.

NgoJa amtafte nesi mmoja ni mzoefu Sana kazin na wanaelewana Sana amfanyie mpango wa kumuunganisha na uongozi wa pale hospitali ya dini alikofanyia field yake ya kwanza ili process zianze mapema na akituma barua yake ya maombi waipitishe moja kwa moja. Jamaa akasema Haina shida,lifanyie KAZI.

[emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kweli binti kamtafuta huyo Nesi na kamwambia anataka kurud pale pale Tena kutanya field ila pia Kuna jamaa pia anataka Kuna kufanya intern hapo.

Nesi kasema Haina shida,tuma barua zenu wote kwa Basi, Kisha yaliyobaki niachieni Mimi. Wakafurahi na kweli barua zikatumwa na majibu yajarudi kua wamekubaliwa na mda ukifika waje TU Haina shida. Ikawa imeisha hivo.

Mda ulivofika wa jamaa Kwenda intern, binti kampigia nesi kua jamaa kesho anakuja uko kwahiyo anaomba umtaftie chumba kizur Cha kupanga chenye choo ndani Kisha pesa anakuja kulipia mwnyw akifika uko.

Nesi kawaambia kua vyumba vizur kupata uku Ni changamoto, mpk uweke Oda mapema na nyie Kama jamaa kweli anakuja kesho mmechelewa hamkuniandaa mapema. Ila mwambie TU jamaa aje akifika uku tutatafuta polepole tutapata TU. Kweli binti na jamaa wakakubali.

Kesho yake kweli jamaa kasafiri,
Na kwasababu ya ugeni wa jamaa mkoa ule, Nesi akaombwa ampokee jamaa stendi na amtaftie lodge ya kulala ili kesho yake ampeleke jamaa akaripoti hospitali. Nesi akasema Haina shida.

Kweli jamaa kawasili stendi,ila usiku saa 2 kwa kuchelewa maana gar Yao ilipata shida njiani. Nesi kapigiwa Simu kamwambia usitoke hapo hapo stendi nakuja. Nesi kaja kufika saa 3.
Nesi kamuomba radhi jamaa kuchelewa alipata dharura kdg.

Jamaa kasema Haina shida Ila nilishataka nipande daladala za Kuja uko uko kwako niliskia wapiga debe wanatangaza iyo ruti Hapa stendi.

Nesi kamwambia ungejichanganya tu Kwenda kule hospital ingekula kwako.
Mimi sikai hospitali maana kule Ni nje ya mji na ungekwama tu Mana kule hamna lodge. Chakufanya ulale tu uku uku mjini nyumbani kwangu kesho ndo uende uko hospital.Jamaa akasema Haina shida.

[emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jamaa kabeba mizigo yake na kupakia kwny gari ya NESI na akapelekwa nyumbani kwa NESI.
Kufika Nesi kashuka na kwenda kufungua geti mwnyw na Kisha kuingiza Gari ndani. Kisha kafunga tena geti mwenyewe.

Jamaa kakaribishwa sebleni,
kamkuta mtoto mdg (kama miaka 5 hivi) anachezea tu PlayStation kwny computer iliyoko pale pale sebleni.
Nesi kamtambulisha ndo mwanae yule, na pale ndo nyumbn kwake anaishi mwenyewe mumewe bahat mbaya alifariki kisha kamuwashia tv jamaa na kumkabidhi rimoti aendelee yeye anaenda jikoni kuandaa chakula.

Baada ya kula jamaa kapelekwa nyumba ndogo ya uani (chumba na sebule self&furnished) kaonyeshwa sebleni na mahala pa kulala. Kisha mwenyeji wake akarud nyumba kubwa kulala.

Kulipokucha jamaa kapandishwa kwenye gar ya NESI, mtoto wa nesi kapelekwa shule na baada ya Hapo wakaelekea uko hospital kuripoti,
jamaa kakamilisha taratibu zote na kuambiwa ataanza intern yake iyo kesho rasmi. Jamaa Kamrudishia MREJESHO mwenyeji wake NESI.
Na nesi akamuitia usafiri wa bodaboda wake na kumwambia ampeleke kwake. Yeye bado MDA wake wa kazi haujaisha.

Sasa kesho yake baada ya kuanza intern yake, Akazoeana na wafanyakaz wenzie Basi akawa amewapa wazo lake la kutafta chumba maana alipo kajiegesha TU kwa mwenyeji wake NESI aliempokea.
Wakamwambia vyumba vinapatikana Ila Ni mjini mjini kule mitaani kwaiyo wakishatoka kazin ndo wakavione.
Jamaa kasema "fresh"

MDA wa Kaz umeisha akaondoka na hao rafiki zake Kwenda mjini kutafta vyumba. Zunguka zunguka na washakaji mpk saa 2 usiku vyumba anaviona ila havieleweki.
Nesi kapiga simu jamaa Yuko wapi, jamaa kamwambia Yuko anatafta vyumba, nesi kakata simu.

Umefka MDA wa kuondoka,
Kampigia simu nesi na kumuuliza kwake Ni mtaa gan vile kapasahau.
Nesi kasema apewe boda simu amuelekeze mwnyw. Boda kasema kapafahamu.

Jamaa kweli kafikishwa, kagonga nesi kamfungulia. Jamaa kaenda seblen nesi kampakulia chakula uku kavuta mdomo. Jamaa anakula nesi akaanza kulalamika.
"Ulichofanya sijapenda kabisa leo, umekuja hapa mjini Mimi ndo mwenyeji wako, afu hata wiki huna ushaanza kuzoeana zoeana na watu hovyo" jamaa kajitetea kua watu wenyewe Mbona Ni wafanyakaz wa pale pale hospitalini?

Nesi kasema,
"Hata Kama Ni wa kazini haijalishi,
Kwanza umeondoka kazin bila kuniaga umenikosea Sana afu wkt wa kurud ndo unanitafuta kuniulza nyumbn Ni wapi! Hivi wee ungepata matatzo uko mie ningejibu Nini? Nikueleweje?"

jamaa ikabd ajitetee kua alikwenda kutafta chumba,nyumba nzur adimu Sana ndo mana kachelewa kurudi.
Nesi kamwambia
"Hicho kiherehere cha kutafta nyumba haraka vipi umekitoa wapi, Si tulishakubaliana kabla hata ujaja uku chumba anaehusika kukutaftia ni mimi"

Akaongezea
"ujuea vitu vya kijinga wee Kaka unafanya Ni kunitukanisha kwa watu afu nna heshima zangu pale kazini. Weng Watafikiria nakufukuza kwangu ndo maana unahangaika hivyo"
Jamaa akasema usifikirie hivyo,kawaida bhana. Nesi akazidi kufoka. Jamaa Kuona nesi kapanic sn ikabd aombe tu radhi yaishe ale kisha akalale zake. Kweli yakaisha ila jamaa akabak na mshangao mwenyej vipi anamaindi vitu vidg vidg tu[emoji848]

[emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
SASA SIKU ILIYOFUATA,
Usiku wa saa 7 na nusu jamaa kalala zake, nesi kamgongea Tena mlango kwa Nguvu, jamaa mbio mbio kafungua. "aisee umegonga kwa nguvu sn umenistua, Vipi kwema? Mbona usku sn,Kuna nn sista?"
Nesi kajibu
"wee nae vipi,Mbona maswali ya polisi afu Niko nje, nikiuwawa je? Hebu nipishe ndani Kwangu bhana"
kampush jamaa na kuingia ndan kishaa kakaa kwny kochi.

Jamaa karudishia mlango kisha kukaa kumskiliza, nesi anasema kaja kamalizia kufumuliwa nywele zake Mana anaona kama jamaa anajisahaulisha jukum lake na yeye kesho anataka kwenda akasuke.

Duh! Jama kastuka na kumwambia usku ushaenda sn afu kachoka,
akalale afu atamfumua kesho. Nesi kasema hataki anataka leo leo. Kama kachoka alale masaa 2 apumzike akiamka atamkuta seblen anamsubir amfumue nywele zake. Jamaa akasema POA haina shida,mi nalala. Kweli jamaa Kaenda chumbn kulala.

Sasa akiwa chumbn taa imezimwa usngz ndo unampitia, akaskia mtu anaingia chumbn kwake kimya kimya na kujibwaga kitandan. Kisha kavuta Shuka alilojifunika jamaa nae kajifunika humo humo na kulala akigeukia upande mwngn (mzungu wa nne). Duh! Jamaa usngz ukakata kabisa. Yaan mpk kunakucha hakumgusa Wala kumsemesha na jamaa usngz haukuja kabisa.

Saa Moja akaskia kaamka kimya kimya na Kwenda kwake kule nyumba kubwa. Duh! Jamaa akabaki na mshangao[emoji848]

SASA JAMAA ALIPOFIKA KAZIN
ikabd amuite chemba yule rafk yake wa karibu amuombe ushaur inakuaje, hamwelewi mwenyeji wake NESI.
Akamsimulia Visa vyote nilivyoeleza hapo juu khs kumkaripia na kumfatilia fatilia, kumnunua zawadi, kupenda kumchungulia akivaa nguo, kumcheka alivobaki na boksa na Hadi ile kulala chumbn kwake mpk asbh ila hakumfanya kitu. Yote kasimulia.

Rafiki yake akamcheka Sana,
Akamwambia ulichokifanya umejiaibisha Sana kaka,wanaume hatuko hivyo. Huyu mwanamke anakutaka 100%. Ni singo mama uyo,Tena ni mjane namjua mumewe alifariki na kisukari ana mwaka wa pili hakazwi, Sasa na sijaskia mtu yy anaemkaza, ni nyege tu zinamsumbua uyo mwenyeji wako.
Usirembe sana Chap kamkate hiyo kiu yake hiyo chalii yangu acha uboya.

Wanawake wakikaa MDA mrefu hawajagongwa wanakua na makasiriko sana,hicho ndo kinachokutokea kila Mara anakukaripia.

Afu Mpk kukucheka uko na boksa tupu ujue kakudharau sn, afu kibaya zaid umelala nae kitanda kimoja mpk kunakucha ujamgonga wala kumsumbua sumbua hapo ndo amekudharau zaidi. Atahisi jogoo wako hapandi mtungi brother.

Fanya hima umgonge uweke heshima rafiki, hizi dharau anakuchukulia Kama mtoto wake nakuhakikishia zitakoma kabisa.Basi jamaa akasema poa,akijilengesha Tena napita nae,silembi. sipendi dharau mm. Ikawa imeisha hivyo.

[emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
SASA USIKU WAKO NYUMBANI,
Jamaa kakaa zake anaangalia tv, nesi baada ya kupika,mtoto wake keshakula na kwenda kulala.
Akamwambia jamaa kua sijiskii kula sahv. Au wee una njaa Sana nikupakulie ule. Jamaa akasema hapana, kawaida TU Niko fresh.
Nesi kasema Basi nifumue nywele zangu basi kesho nikasuke,nishachoka kuvaa mawigi Mimi, Jamaa kasema fresh lete chanuo Kisha njoo ulale Hapa mapajani nikufumue nywele.

Kweli nesi kaweka Kichwa na jamaa kuendelea kumfumua, Sasa Kuna MDA nesi akawa Kama kapitiwa usngz. Jamaa akajisemea kua fursa ya kumgonga uyu nesi ndo hii. Basi akawa anafumua akipata nafas anapitisha mkono kifuani ndani ya blauzi anashuka Hadi Kwny manyonyo anamtomasa tomasa. Nesi katulia tuli anajifanya usngz umemkolea.

Jamaa kapitisha mkono Hadi chini ya kitovu, kaingiza kwny kanga mpk Kwny papuchi. Kamtomasa tomasa nesi kalowa na kuanza kutoa miguno.
Hajakaa sawa nesi kainua shingo na kumpiga denda jamaa. Mambo hayakua mengi sn. Jamaa wakachojoana na kupingana show ya kibabe pale pale seblen Kwny kochi.

Baada ya show wote njaa zinauma,
Nesi kapakua chakula wamekula Kisha nesi kaaga anatoka sebleni anaenda chumbn kwake kulala. Jamaa nae kaaga anaenda kwny Kota yake ya nje kulala.

Basi mahusiano rasmi ya kimapenz Kati ya jamaa na nesi yakaanzia hapo.

Nesi akachangamka Sana,
Zawad zikawa hazikatiki kwa jamaa maana kipind icho jamaa analipwa Ela za intern ambazo Ni ndogo sn ulinganisha na mshahara na malupulupu aliyokua akipokea nesi yule,achilia mbali miradi inayomuingizia pesa aliyoachiwa na marehemu mumewe. Kwaiyo jamaa alkua Ni Kama analelewa pale, bills nying nyumbani na viwanja kwny bata alikua anaclear NESI mwnyw.

Penzi likakolea sn jamaa akasahau mpk kutafta chumba kupanga mpk zamu ya mchumba wake wa chuoni Kuja field ikafika. Mchumba wake kaja field pale pale hospitali, akashangaa jamaa miez yote bado Yuko kwa nesi hajatafta chumba Ila kwasababu alikua anamuamini sn nesi afu anamuona mtu mzima,hakuhofia chochote kile. Binti akawa anakaa kwao,anatoka ndo anaenda field pale hospitali bila tatzo. Wanakutana na jamaa kazini story za hapa na pale maisha yanaendelea.

Na nesi kwasababu hajui jamaa Kama Yuko Kwny mahusiano na yule binti anajiona Yuko peke ake kw jamaa, akawa anajiachia sn. Ila kwa jamaa ile tabia ikawa Ni mwiba mkali sn kuwabalance wote wawili maana wako ofisi Moja na uyo mpenz wake wa chuon bado hawajaachana anampenda Sana na ndo Alie na malengo nae.

Ikawa Ratiba ya kua na mpenz wake wa chuoni inabana Sana mana nesi Anakaba kila Kona Had Kwny ratiba zake binafsi akitoka Anataka ajue kaenda wapi,anarudi saa ngapi na yuko na nani. Akizingua nesi anakua mbogo.

Maji yalipozidi unga, mpenz wake wa chuoni Akawa anataka wakaonane private anamhitaji ikabd ampange kua wataenda kuoanana lodge, kule kwa nesi hapafai sio ustaarabu .avute subira. Binti kweli kakubali

Sasa Ikabd akaombe ushaur
Anachezaje hizi karata za wanawake wawili ofisi Moja na wote hawajuani.
Afu mmoja (nesi) anampendea pesa,Bata na matunzo, mwngn (binti) Ni true love.

Rafki yake akamshauri kua hatakiwi kuwapoteza wote au mmoja wapo,
kila mmoja ana umuhimu wake. Kumpeleka mwanachuo lodge au Kota yake haifai maana anafatilia Sana yule nesi,atawafumania itakua balaa.

Cha kufanya Ni adanganye kaenda kumtebelea rafk yake,Kisha atampatia geto waenjoy na uyo mchumba wake.
Jamaa kaafiki wazo Lile na kurudisha majibu kwa binti mwanachuo kua watatafta geto kwa rafk Yake wa pale kazin kwao wakakutane. Binti kakubali.

Kweli siku ya miadi imefika wikendi jamaa kamuaga nesi anaenda kutembea kwa rafki yake uyo. Nesi kakubali, jamaa na mwanachuo wameenda geto kwa rafki mtu wamefanya ya kufanya kila mtu kaenda zake. Salama salmini.
Na jamaa akaendelea kuzichanga vyema karata zake na wanawake wote wawili ofisi Moja, ila hawajuani.

[emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
SASA WIKENDI MOJA,
Jamaa kamuaga Nesi anaenda kwa rafiki Yake Kupiga story atarudi jioni.
Nesi kakubali, kumbe kachepuka kampitia na binti mwanachuo wameenda getto kwa uyo rafiki yake dokta mwenzake kufanya mapenz.

Wamefika wakamkuta rafki nae Yuko na mwanamke wake, jamaa akataka kugeuza kuwaacha Kwenda lodge. Rafiki kwa kumheshimu jamaa ikabd atoke na mtu wake wawaachie chumba wao wakatembee tembee mjini maana siku hiyo hawakua na Ratiba ya kufanyana. Mtu wake kakubali wamewaachia chumba wameondoka kuwaachia nafasi.

Sasa wako katkat wafanya mapenzi,
Wakaskia saut ya kike inagonga mlango, jamaa akamwambia mwanachuo akamskilize uyo atakua Dem wake rafiki kuna kitu atakua kasahau. Binti bila kujiandaa Sana akatoka na khanga Kwenda mlangoni kumskiliza aliegonga.
Kufungua TU, uso kwa uso NESI Huyu hapa.

Nesi kalianzisha, kamvuta binti nywele na kumburuza nje,kanga alojifunga ikabaki kwenye kitasa na kuanza kumpa kichapo kikali. Binti alivozidiwa kamngata nesi kwny titi na kuchomoka kurud ndani. Nesi kaingia ndani, Ugomv umekua mkubwa. Jamaa kaanza kuamulia Hali tete, Majirani walipojaa nao kuamulia.
Binti akapata upenyo, kachomoka na nguo zake kakimbia. Jamaa nae alipopata upenyo,akakimbia. Wakamwacha nesi yuko anapigizana kelele na majirani wa pale.

Baada ya hapo,
Jamaa akaenda kumbembeleza mwanachuo amsamehe yaishe. Binti kagoma kabisa na kadhamilia waachane kamfanyia usaliti mkubwa Sana kutembea na nesi aliemwamini na kumkabidhi ampokee amsaidie maswala yake ya intern.Jamaa bembeleza lakini wapi, tuma rafiki mtu bembeleza wapi.Binti kagoma kabisa kuelewa.

Sasa Hali ikawa tofauti kwa NESI
Nesi akazidisha mahaba kwa jamaa
Jamaa nae kule kwa binti akachoka kubembeleza akadhamilia anakua na NESI Moja kwa moja liwalo na liwe hawez kubembeleza mtu kila Mara haelewi, wanawake wako wengi bhana. Kweli rafk Yake nae akaridhia jamaa ampotezee binti maana binti keshaanza kujiona matawi kisa anambembelezwa mno.

Kweli baada ya jamaa kumpotezea binti, hata field pale binti akakatisha gafla na mawasiliano na binti yule yakafa rasmi. Jamaa nae akawa bize na nesi wake mpk wakafikia hatua intern imeisha jamaa anatakiwa aombe ajira rasmi.

Nesi alikua na connection kubwa sn wizarani na kwny uongozi wa ile hospital, mipango ikafanyika na jamaa akaajiriwa rasmi pale pale hospitalini na baada ya Hapo ikabidi wafunge ndoa rasmi kiserikali na nesi yule kutambulika rasmi MUME na MKE.

Sasa baada ya ndoa, sarakasi za nesi yule zikaanza upya.yaani Kisirani,wivu, ubabe na lugha za maudhi vikaanza upya.

1. KUNA SIKU
Jamaa katoka safari, kufika nyumban jamaa akamuita mtoto wa nesi aje ampatie chocolate Akawa haitiki. Ikabd amfate mtoto chumbn kwake. Kufika kakuta mtoto kaungua mguu na una malenge lenge. Kamuululiza mtoto hasemi chochote. Ikabd amfate mama ake kuulizia tatzo nn mtoto Mbona Kama kaungua.

Nesi akasema mtoto kaungua na maji moto bafuni kwenye shower,aliacha mlango wazi mtoto kafungulia koki ya maji Moto bila kuchanganyia yakamuunguza.
Jamaa akauliza kivipi maji ya shower yamuunguze haraka hivyo wkt kabla hayajatoka lazima kwanza heater iyachemshe,Ina maana mtoto aliwasha vp heater na kimo chake hafikii kwenye switch. Nesi akajibu kua aliacha kaiwasha.

Jamaa akauliza tena inawezekana vp mtoto aungue mguuni na maji moto ya shower, afu kichwani au mikononi asiungue. Nesi kapanic na kuanza kutukana kua asimuingilie kwny maisha yake na mwanae. Kama anautaka ukweli Ni kwamba mtoto kaiba chenji zake dressing table na Kwenda kununua chocolate. Keshamzuia tabia ya wizi hataki, hiyo ndo dawa yake kumuunguza na maji ya ugali. Duh! Jamaa akabaki na mshangao kwa ukatili ule,ila ikabd asiendelee kuhoji maana keshasema hayamhusu Ni mtoto wake,Kama anataka Basi azae wake ndo ahoji maswali ya polisi. Dokta akapotezea.

[emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
2. SIKU NYINGINE
Usiku mmoja ambao walifanya Sana mapenz, jamaa anaamka saa 3 asbh nesi keshaondoka kazini, anaenda kwenye dressing table akachukue mswaki akakuta pakti ya blister Moja ya vidonge vya P2 imefunguliwa vidonge viwili vimebanduliwa na Kuna glass ya maji iko nusu. Ikabd ahifadhi ili akirud jion amuulize nesi khs hizo p2.

Jion nesi karudi jamaa kamuita chumbn kumuuliza, Nesi mwanzoni akataa P2 sio zake. Alipombana zaidi nesi kakiri Ni zake na kameza yeye.
Kuulizia sababu kwanini kameza, nesi kasema hayuko tayar kuzaa na mwanaume anayeishi nyumbani kwake kwa sasa, Kama kweli anataka kuzaa nae ajenge nyumba nyngn kwa ajili ya mtoto wao atakaezaa nae.
jamaa kasema bado anajipanga maana kwasasa anawajengea wazazi wake uko kusini, akimaliza ndo atajenga nyumba Yake ya kuishi.
Sahv amvumilie. Nesi akawa Kama kaumuelewa. Ikawa imeisha hivyo.

3. Sasa IKIWA IMEPITA MIEZ MITATU
Tangu tukio la P2, Nesi akarud toka Safar akiwa mchovu Sana. Jamaa kwasababu alimmiss sn akaomba penzi.Nesi akasema Yuko PERIOD.

jamaa Ikabd amuache. Baada ya siku chache nesi yule kazidiwa akiwa kazini na kupewa kitanda apumzike. Tatizo akaambiwa Ni tumbo linamyonga sana nesi. Basi Watu wa maabara wakamchukua sampo za mkojo,damu,choo na ute wa kwenye uke kwa ajili ya vipimo. Majibu yalivokua tayar wakampelekea mmewe ambae Ni daktari pia pale pale (jamaa mwenyewe) . Jamaa kusoma Yale majibu upande wa mkojo akaona yanasoma positive for pregnancy. Duh! Akashangaa kwanza
Akadhan wamnatania, akenda maabara.

Akawaambia wapime Tena ajiridhishe, kweli kapima ikaonekana pia ndio anayo mimba,Tena kipimo kilivokolea itakua Ni mimba kubwa TU. Basi kwa akili yake akajua Ile mimba aliyomezea p2 miez 3 iliyopita imenasa kwelikweli na imegoma kuharboka. Basi kafurahi mno. Na kumpeleka taarifa nesi kua vipimo vimeonyesha anayo mimba. Itakua ndo chanzo chamaumivu y tumbo.
Nesi akabisha na akaoneshwa kutojali sana hizo taarifa.

Ikabd jamaa afanye utaratibu mkewe asogezwe kwny utrasound machine aweze kujua kijusi kitakua jinsia gan maana Kama iko kwny miezi 4 na kuendelea anaouwezo wa kuijua jinsia ya mtoto ajaye.

Kweli Ikabd nesi asogezwe kwny machine, Kuangalia tumboni wakaona ndani hamna kitu ni utitiri wa uchafu na nyama nyama zilizoharibika na kutoka kdg kidg, jamaa akaumia sn maana kajua kumbe tumbo Lile nesi alimeza madawa ya kutolea mimba na ile mimba kweli imetoka.

Nesi alivoambiwa ukweli, kapanic na kusema hawezi kumzalia mtoto wkt anaishi kwny nyumba ya marehemu mumewe, hivi anadhan ndugu wa mume wakija kujua amezalishwa kwny nyumba ya marehem kaka yao na mwanaume mwingine itakuaje.

Jamaa Akitaka amzalie Basi amjengee kwanza. Na hiyo mimbankweli kaitoa makusudi. Basi Jamaa akasema POA, mwaka huu nanunua kiwanja na mwakani nakujengea unizalie mtoto MKE wangu. Nesi kasema sawaHaina shida. Maisha yakaendelea.

[emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
4. SASA KUNA SIKU
Jamaa Yuko na mkewe kwenye bustani, yeye anamwagilia maua mkewe anachezea Simu.
Basi Simu ya jamaa ikaita. Akaileta mkewe na kumuweka loudspika kaishikilia maana jamaa mkononi alishikilia bomba la maji. Akapewa taarifa ya gafla na yule rafiki yake wa kazini kua yule binti Aliekua mpenz wake wa zaman chuoni na aliefanyia field pale kazin kwao walieachana Kaletwa mahututi na kalazwa pale. Ndo wako wanafanya wawezalo kumsaidia maana anapumua kwa shida sana. Jamaa akajibu kua "POA,nakuja hapo chap basi"

Jamaa kaenda kunawa na kuvaa haraka ili kuelekea uko hospital.
Ile anatoka Nesi akamwambia "subir Kuna kitu umesahau mme wangu"
Nesi kaenda ndani na kuleta sindano ndogo mbili na kichupa kidogo Cha insulin.

Jamaa kauliza ya nn hii? Nesi kajibu kua Hii ndo revenge murua kabisa kwa fedhuli yule mwanamke kwa kuning'ata titi langu kipind kile cha ugomvi nmewafumania, alidhan atanikimbia daima Sasa Hii inaenda kummaliza kimya kimya na hamna mtu atajua. Naomba msaada wako mme wangu.

Jamaa akabaki mdomo wazi,
Nesi akaongezea kua chukua Hii insulin utakua unamchoma kidg kidg kwenye unyayo wa mguu na hamna atakaestukia maana hamna dokta au polisi anakaguaga nyayo za miguu Kama zimechomwa.

MWISHO wa siku kongosho lake litakufa ataugua kisukari mpk anafariki Watu wote watajua kafa kwa kisukari. Kwa alichonifanyia Huyu mwanamke hii alama ya meno Yake kwenye titi langu akiendelea kuishi nafsi yangu itaniuma Sana, fanya hivyo mme wangu nakuomba.

Jamaa ikabidi afoke kua huo upumbavu hawezi kuufanya kamwe,hata Kama wameshaachana na alimng'ata kumuua Ni kisasi Cha kipumbavu mno, ataenda kumsaidia Kama wagonjwa wengine hamna kibaya chochote binti yule kamfanyia.
Jamaa kampokonya nesi Ile chupa ya insulin na kuipasua pale pale chini kwny pavement za nyumba yao.

Nesi kakasirika Sana na kasema Kama hawez kuifanya hiyo kazi Basi nitaenda kuifanya mimi mwnyw, ngoja nikavae niende huko hospitali.nesi kaingia ndani kuvaa na kweli katoka na gari yake.

Jamaa kuona vile akajua huyu nesi Yuko serious kwny hili hatanii. atamuua huyu binti akichelewa. Basi Jamaa Kachukua boda fasta na kuwahi hospital kabla nesi hajafika.

Akafika na kuita taxi na kuomba haraka mgonjwa huyu kuhamishwa hospitali nyngn, wenzie wakauliza nn tatzo.Akawadanganya kua huu ugonjwa wake unatibiwaga na daktari maalum,anamhamisha mgonjwa haraka wasije kumpoteza na hali yake ya dharula na kushindwa kupumua vile.basi wenzie wakabariki.

Nesi anafika tu, akakuta ndo binti anaingizwa kwny taxi kuhamishwa hospitali nyngn. Nesi Akanuna balaa.
Jamaa kamhamishia hospital ya serikali na kusaidiana na madaktari wa pale kumsaidia binti uku akimlinda mpk pale alipopata nafuu. Jamaa ndo Ikabd kuwaachia ndugu zake waendelee na yeye kurudi nyumbn kwake kule kwa NESI ikiwa zishapita zaidi ya siku 4 tangu ameondoka kwa nesi.

ALIPOFIKA nyumbn kamkuta nesi sebleni kanuna, nesi kamwambia jamaa kua arudi uko uko alikotoka. Jamaa ikabd ajisimamie kua huu upuuz wa kupelekeshwa pelekeshwa na mkewe ufike mahali sasa ukome. Basi wakaanza kufokeana. Katika kufokeana NESI kakasirika na kuelekea jikoni na Kuchukua kisu, Kisha kaenda funga mlango wa sebleni na kumwambia jamaa kua hiki kisu anamuua afu Nayeye anajiua.
Jamaa akahisi masihara, kaenda zake chumbani.

Ghafla nesi kaja na kisu speed kumchoma, purukushani jamaa akakiwahi kile kisu kukizuia kwa kukishika kwny makali na mikono mpk akampokonya kwa Nguvu akampiga vibao akadondoka chini na kuondoka pale uku viganja vyake vikivuja damu.
Akaenda Moja kwa moja rafki yake hospital, jamaa kamfanyia dressing na kumshaur hili suala lifike polisi maana huyu mwanamke ana roho ngumu Sana. Anaweza kumuua.

Kufika polisi ile kesi ikaishia kwny usuluhisi TU dawati la jinsia wakikazania kua ule ni ugomvi wa Wanandoa Ni wivu wa kimapenz, jamaa akashauriwa na rafk Yake kua yule mwanamke kadhamiria. Na atamuua kweli, Cha kufanya aondoke kabisa pale nyumbn. Kweli jamaa walipotoka TU polisi, kaenda kwa nesi kabeba nguo na vitu vyake vya muhimu na kuondoka na kwenda kukaa kwa rafki yake huyo kwa Muda.

[emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
IKIWA NI SIKU YA 3 KWA RAFIKI YAKE
jamaa akaskia kua yule nesi alienda pale hospital alikolazwa yule binti. Jamaa akajua kua huyu binti atauwawa TU maana yule nesi anaconnection pale hospital ya serikali,na Kama kweli kadhamiria kumuua atamuua kweli. Basi Akaenda kuwashaur ndugu wamtoa pale. Ndugu wakabisha maana waliona jamaa Ni Kama anawasumbulia TU mgonjwa wao wkt walipomleta keshaanza kupata nafuu.

Ikabd jamaa amwambie ukweli binti mwnyw kua pale alipo hayuko salama, nesi anamuwinda amuue ndo maana alimhamisha kule anakofanyia kazi, na Hapa kashaskia nesi alikuja kuja.
Kuna uwezekano kaja kupanga namna ya kummalizia kabisa. Binti kapata hofu.

Basi binti akakubali kuhamishwa pale na ikapangwa watoroke pale hospitali, binti jion kajifanya anafanya mazoezi kuelekea eneo la mochwari ambako jamaa Keshaandaa Gari, kweli binti katoroshwa na kupelekwa lodge na matibabu yote yaliyoendelea akawa anasimamia jamaa kule kule lodge bila yeyote kujua isipokua yule rafk tu yake pale kazin.

Binti akiendelea na matibabu kule lodge,jamaa akaenda kuprocess talaka mahakamani waachane kabisa na yule NESI. Mahakamani jamaa kaulizwa khs kugawana Mali,akasema Hana haja ya Mali, anachotaka Ni waachane TU. Nesi katumiwa wito kua anahitajika mahakamani, hakuja. Hata alivopigiwa simu akasema hajaachana na mumewe Bado anampenda, uko mahakamani yeye haji.Basi baada ya nesi kukaidi wito Mara 3 ikabd mahakama ivunje ndoa ile na jamaa kakabidhiwa divorce certificate akaendelee na maisha yake mengine.

Sasa baada ya kuachana na nesi,
Na yule binti kupona, wakaenda kupanga nyumba na wakaanza kuishi pamoja. Jamaa kaenda kuonekana kwao binti,kawasilisha barua na kapewa baraka zote. Wameishi Kama miez 3 binti akajihisi ana mimba. Kupima kweli kanasa mimba ya jamaa. Basi wakakubaliana kua wafunge ndoa mapema kabla mimba haijawa kubwa itakua aibu ili sasa wafungue ukurasa wa mapenz yao upya Kama Wanandoa rasmi.

Sasa siku Moja jamaa akiwa wodini,nesi kamfata na kumwambia kua kaskia ana mpango wa kufunga ndoa na yule binti.Kwaiyo Anaomba sana msamaha warudiane Kama kuna sehem kakosea atajirekebisha,jamaa kwambia haiwezekani atafute mwanaume mwngn TU,yeye keshamove on tayari na hataki Tena mazoea na yeye kabisa. Wameshindwana.

Nesi kwa hasira akamwambia kua hiyo ndoa haitofanikiwa, labda Kam sio yeye (kataja kabila lake) juu ya uso huu wa ardhi. Jamaa kasema asimbabaishe na ndoa itafungwa na Hakuna kitu ataweza kufanya. Basi nesi kaondoka pale kwa hasira.

[emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
MWEZI KABLA YA HARUSI
Sasa ikiwa umebaki mwezi mmoja kabla ya harusi yake na binti, dokta akawa kaazima gari ndogo kwa ajili ya kurahisisha mizunguko na ufuatiliaji wa michango na mambo kadhaa ya harusi Yao inayogarajiwa. Kuna siku akawa anazunguka na iyo gari ndogo uku na kule akastuka Kuna Gari nyngn inamfuatilia kila anapokunja kona nayo gari inakunja. Akisimama, nayo inasimama. Machale yakamcheza.

Ikabd atafute sehemu public asimame na kuwauliza kwann wanamfatilia fatilia. Ile kashuka TU akaifata Iyo gari na kuwauliza kwann wanamfatilia, hawakujibu kitu. Gafla anatupa macho siti ya nyuma anamuona nesi kakaa na wanaume wawili Kama mabaunsa. Basi akaona ishakua shari Hii,ikabdi aondoke zake.

Kweli karud kwny Gari yake na kuelekea polisi kuripoti kinachoendelea maana huyu mtalaka wake anamfatilia kila Kona, endapo akipatwa na matatizo yyt wamtafute kumhoji. Nesi alipoitwa polisi kuhojiwa akasema jamaa anajistukia TU,yeye alikua Kwny mizunguko yake ya kawaida TU Hana mpango nae washaachana zaman sana. Basi ikawa imeisha hivyo, Ila jamaa Hana amani kabisa.

Ikiwa imebaki wiki 2 kabla ya harusi,
Yuko na anakunywa chai kujiandaa Kwenda kazini akaskia hodi mlangoni.
Ikabd aende Kufungua, ile anafungua akamuona NESI Yuko na mabaunsa wawili afu Hasemi kitu anatabasamu. Jamaa Ikabd awaulize kilichowaleta pale nyumbani kwake Ni Nini, wakawa hawamjibu kitu. Akawaambia waondoke kwake, hawataki.

Basi akawaambia kama hawaondoki anapiga Simu polisi wamemvamia nyumbn kwake.Walipoona kainua simu anataka Kupiga polisi, wakaondoka pale. Jamaa akabaki na mshangao huyu nesi mtalaka wake anachotaka Ni Nini,keshamuacha na maisha yake sasa anamfata fata nn kila anakoenda. Basi akaendelea na shughuli zake.

WIKI MOJA KABLA YA HARUSI
Kuna siku jamaa Katoka kazini,kagonga hajafunguliwa kaingia Moja kwa moja kamuona chumbn kajilaza kitandan. Akajua uyu Usngz na uchovu wa mimba unamsumbua.

Akaenda Moja kw Moja jikon na kujipanga chakula na kula mwnyw.
Baada ya kula Ikabd aende bedroom kubadili nguo ili akaoge. Gafla anaangalia kwny droo ya kitanda akaona mashumaa,kijiko chenye masizi , mabaki ya unga unga na sindano moja inayoonekana Kama imeshatumika. Jamaa akaogopa na Kupiga Simu polisi. Alipoona wanachelewa akaita majirani wamemwamsha haamki na inaneokana keshakua wa baridi tayar. Maana ake mkewe kafariki. Kila mtu akasikitika pale.

Polisi Wamefika pale Wakakagua eneo Lile wakasema huyu atakua kajidunga madawa, inaonekana ame-overdose.
Ila Ngoja mwili upelekwe hospital watatwambia Kama kweli ni madawa au sio kweli. Basi mwili umepelekwa hospital na majibu yakarudi kua kweli alijidunga madawa na damu yake inaoenekana kua HEROIN nyingi Sana pamoja na insulin nyingi inaonekana alikua na kisukari kabla. Kisukari na heroini Ni sumu ya hatari.

Jamaa akahis kuna mchezo mchafu umefanyika maana Kuna kipind yule nesi aliwahi kusema angemuua kwa insulin. Akawaambia hivyo polisi.
Polisi wakasema hata isingekua insulin kwa heroin aliyokutwa nayo kwny damu Ni nyingi mno afu Ni mjamzito pia, pia kisukari alichonacho lazima TU hata kwa heroin kidg angefariki TU.

Jamaa akabisha Sana, wakaja na ndugu wa mke kua hajawai kuugua kisukari Wala kutumia madawa ya kulevya tangu binti yao kakua. Polisi hawakupenda kuwasikiliz kwa maana mabinti waliokulia dsm hasa vyuoni wanatumia sn madawa afu wanajificha, usikute hata mmewe alikua anamficha. Akitoka ndo anayatumia maana hata kijiko alichokutwa anatumia kuchomea heroin kinaonekana kimeshatumika MDA mrefu, hajaanza siku Ile tu aliyokutwa kafariki. Basi jalada la uchunguzi likafungwa na wakaruhusu mwili ule uzikwe. Jamaa aliumia Sana

[emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
BAADA YA MSIBA
jamaa akawa kaumia Sana, akawa hatoki ndani mwingi wa mawazo kila kukicha. Sasa Kuna siku Watu washatawanyika kabaki mwnyw nyumban. Nesi yule akaja na wafanyakazi wenzie kumuona na kumpa pole ya msiba, wakampa na rambirambi zao Kisha wakaondoka.

MDA Si mrefu baada ya kuondoka,
Akamuona NESI peke anarud pale,
Akamuuliza kilichomrudisha nn, nesi kasema kaja kumfariji maana anaonekana Ni mwingi wa mawazo.
Jamaa akamjibu kua haitaji kufarijiwa na yeye, Ni Bora TU aondoke maana keshajua kila alichokifanya na huu msiba anajua 100% yeye ndo mhusika.
Nesi akacheka sana, Kisha kaondoka pale. Jamaa kabaki na maumivu yake.

Baada ya siku 2 nesi karud kwa jamaa,
This time kaja kiupole sn akamwambia aache kumuwazia aliekufa maana haiwez kubadili chochote kilichokwisha tokea na hawez kurudi huyo anaemlilia kila kukicha. Anaomba warudiane tu mahusiano Yao upya ili amfariji kumpitisha ktk kipind iki kigumu.

Jamaa akamjibu Kama alidhan kumuua mkewe ndo itakua ticket ya wao kurudiana,kajidanganya sana.
Aondoke haraka Sana pale nyumbn kwake hamhitaji Tena kwenye maisha yake.Nesi akamjibu kua hata afanyeje kuachana na yeye hiyo asahau na atakua na yeye kwa gharama yoyote ile atake au asitake. Basi wakaanza kujibizana sana jamaa anasema Toka nje- nesi anajibu sitoki, majiran wakaanza kujaa pale. Ikabd NESI AONDOKE pale.

Sasa jamaa alivoona Hali imekua sio, akamuita rafiki yake wa kazini na kumuomba ushaur. Jamaa akamshauri pale ahame maana Kama mkewe aliweza kudhurika pale na huyu mwanamke anakuja pale kila mara, Kuna siku atakosa Watu wa kumsaidia afu huyu mwanamke atamuua Kama alivomuua mkewe.
Kweli jamaa kahama pale akaenda kupanga kwingine.

Ikapita Kama miez 2 kimya na yule nesi wanapitana tu kwny korido za hospitali kila mtu kashika 50 zake.
Sasa Kuna siku jamaa saa 6 za usiku katoka kuangalia mpira, Yuko kwa mguu kuelekea kwake. Gafla nesi yule Yuko mbele yake kaja kamblock njia, jamaa akamsukuma na kuendelea na safari. Nesi kazid kumfata nyuma. Akafika mbele baunsa mmoja katokea na kumblock njia jamaa. Anageuka nyuma na nesi huyu Hapa. Hana pa kukimbilia kablockiwa mbele na nyuma

Akauliza tatzo nn, Ni kipi kibaya kawafanyia mpk wanamghasi ghasi hivi njiani. Nesi kasema Anataka kuzaa nae leo leo,Yuko siku za hatari.
Jamaa akapuuza akataka kuondka. Yule baunsa mbele akamblock, Kisha nesi akaamrisha jamaa waende wote kwenye Gari yake. Kufika Nesi akaingia kwny Gari na jamaa, mabaunsa wakabaki nje.

Kisha nesi akamuelezea jamaa kua bado anampenda sn, sio kwamab anamtosha Bali hawez kukaa mbali na yeye anaomba waende wote kwake, anahitaj sn wasahau yaliyopita na anahitaj kuzaa na yeye na Leo Yuko siku za hatari. Jamaa kasema hilo haiwezekani. Nesi akasema Kama haiwezekani Basi wazae wote TU abaki na mtoto kama kumbukumb yake. Jamaa akasema alishahitaji kuzaa nae sana kipind kile akikaa kwake ila nesi mwnyw hakuhitaji kuzaa nae ndo maana alikua akimeza p2 na kutoa mimba yake. Hadanganyiki kizembe namna Hii.

Nesi akabadilika na kukasirika Sana Kisha kumuuliza "unazaa na Mimi au huzai na Mimi, niamue nnavoona inafaa Mimi?"
Jamaa kuona vile afu keshatiwa mtu kati na usiku ule saa 6 Hana hata wa kumsaidia, akasema tutazaa tu Haina shida. Nesi kamwambia basi ongoza Twende tukafanyie nyumbn kwako usiku huu huu.

Jamaa akasema kwangu nilikopanga haifai, wapo ndugu zake marehem MKE wangu, haitaleta picha nzuri Twende tukafanyie lodge, nesi kakubali. Kawaambia vijana wake waingie ndani. Mmoja akaendesha mpk lodge kwny aliyochagua jamaa.
Jamaa anaenda lodge Ila mawazo chungu mzima, huyu mwanamke Ni mkatili Sana, usikute anatumia kigezo Cha kuzaa na mm ili aniue kimya kimya uko uko ndani lodge. Cha kufanya hapa nifanye kila mbinu niwatoroke usiku huu huu.

Basi Baada ya jamaa kufika lodge,
Wakaoneshwa chumba chao wale mabaunsa wakabaki nje ya lodge sehem ya restaurant wakipata vinywaji, wao wakaingia chumbani.
Jamaa kaingia bafuni kaoga, Kisha kamwambia nesi nae akaoge. Ile nesi kaenda kuoga jamaa akatoka kimya kimya ili atoroke, kufika counter anatoa macho nje akawaona wale mabaunsa wamekaa wanapata vinywaji, akajua Hapa kupita ni ngumu.

Ikabd amwombe mhudumu amfungulie mlango wa nyuma, Kuna mgeni wake Anataka kumuingizia mle lodge usiku huu hataki apite mlango wa mbele Kuna Watu pale. Mhudumu kakubali na kaenda mfungulia mlango wa nyuma.

Jamaa alipofunguliwa TU, katoka mbio na kuondoka Kwenda kwa rafiki yake na kumsimulia kila kikichojiri alivyotekwa usiku ule akitoka kuangalia mpira na kilichojiri kule lodge alivowatoroka. Jamaa akamwambia alale pale, kule kwake sio salama Tena Kisha kesho asbh wataenda kuripoti hiLi tukio kituo Cha polisi. Basi akalala kwa rafiki Yake.

[emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
KESHO yake kulipokucha jamaa Ikabd aamkie kituo Cha polisi kuripoti, kawasimulia maaskali pale mapokezi khs kilichotokea usiku wa Jana na nyendo za huyo aliekua MKE wake kumgonga zonga na kumtisha maisha. Afande akachukua Simu na kumpigia nesi aje anahitajika kituoni. Hakuchukua MDA nesi kafika kituoni ila kaishia nje. Jamaa kamuonesha afande kua mtalaka wake ndo yule pale nje tayar keshafika.

Afande akamuita nesi aje ahojiwe,
Nesi kamjibu afande kua haojiwi na mbwa, anahojiwa na mwenye mbwa.
Afande yule akawa Kama kapanic wakaanza kujibizana mbovu na nesi, hawakukaa Sasa OCD akawa kafika kaelekea ofsin kwake. Nesi yule kamfata na kapitiliza Moja kwa moja kaunta na kuelekea ofsin kwa ocd.

Hakukaa Sana,OCD akawaita jamaa na NESI ofsini kwake wazungumze.
Yule afande akataka kuingia akazuiwa, Basi OCD akawasihi wamalize tofauti zao afu jamaa akaambiwa aache kumzushia nesi kua kamuua mkewe maana ataitwa kuthibitisha Maneno Yake atashindwa na atalazimika kumlipa fidia nesi.

Jamaa alipojieleza Sana, OCD akasema yeye keshamaliza na waondoke ofsini kwake, hakuna kibaya chochote kitampata. Wakamalize tofauti zao huyu NESI anampenda Sana. Basi ikawa imeisha hivyo pale kituoni.

Jamaa alipomrudishia MREJESHO rafiki yake, rafki yake akasema uyo OCD atakua keshahongwa Hana Cha kumtetea jamaa, kinachotakiwa na kupiga kimya TU asizoeane na nesi yule Tena.

Basi Kuna jumamosi moja jamaa alikua off hakwenda kazini akiendelea kuishi kwa rafki yake uyo wa kazin kwae kisirisiri. Basi ile Anataka kutoka nje akawaona wale mabaunsa wawili wanaotembea na NESI wameketi nje kwenye viti vya plastic na mpangaji mwenzao mmoja wanakunywa pamoja konyagi na kuvuta sigara.

Kwa hofu jamaa Huenda wamemfata pale kumdhuru, Ikabd amfahamishe rafki yake aje nyumbn Mara Moja.
Rafki yake kufika akasema Hapa siondoki mpk nijue mwisho wa hawa jamaa, kama watakudhuru Basi tutapambana nao mpk kieleweke.

kweli wakasubiri mpk wale mabaunsa wakaondoka. Walipoondoka rafk yake jamaa Ikabd ajisogeze kwa mwenyeji wao ambae Ni mpangaj mwenzake aliebaki anakunywa konyagi peke yake pale ampigishe story uku akimdadisi Zaid hao jamaa walikuja na mishe gan pale, Wana mahusiano gani. Ni watu was Aina gani.

Basi mpk jioni Hakuna alichoambulia, Zaid ya kuambiwa Ni Yale Ni wateja wake kwny madili yao ya kikazi , ukiona wamekuja pale ujue Kuna tukio la hela wanaenda kupiga maana wale sio Watu kuremba, Ni watu wa kazi kazi.

Jamaa kwa hofu akawa anaogopa Hadi kutoka nje.

Hajakaa sawa,
Kuna siku katembelewa na mgeni,
Kutoka nje Ni bodaboda wake wa zaman kipind akiishi kwa nesi, akamwambia kaka nakuomba Sana twende pemben tukaongee,Ni kwa faida yako. Kwasababu ya hofu akasema hawez kutoka pale peke yake,ukzngtia uyo boda anahusiana na NESI. Ikabd ampige rafk Yake aje wamsikilize

[emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kweli rafk Yake kaja,
Wakaenda sehem flan Kuna korongo na nyasi ndefu na kuanza kuongea. Jamaa akasema Hana MDA Sana ila amekuja pale kumtahadharisha jamaa akae attention Yuko kwny mishen ya kuuwawa na NESI aliyekua MKE wake wa zamani, na mipango yote iko tayar na yeye Ni sehemu ya mpango kwahiyo anaomba kuahidiwa usiri kwanza kabla hajaendelea na chochote. Duh! Wakashangaa.
Wakamwambia usiri Ni uhakika.

Boda akaongezea kua,
MDA wowote pale nyumbn kwao usiku watavamiwa na majambazi na atauwawa yeye TU na Kisingizio kitakua Ni tukio la ujambazi na uporaji Maana Kuna fremu za Maduka nje ya iyo nyumba Yao wanayoishi.
Na mchora ramani Ni mpangaji mwenzao PUSHA ambae aliwapokea mabaunsa juzi Na yeye kama bodaboda ndie aliwaleta wale mabaunsa pale kwa maelekezo ya Nesi mwnyw kwa ajili ya mchoro. Kwaiyo Kama wanaweza kuanzia kesho jamaa ahame kabia na asilale pale.

Rafki Yake akasema zitakua tetesi au usikute boda nae katumwa kuwapeleleza. Boda akawaambia Kama hawamwamini Basi wasilale ndani wiki lote hili afu wataona Kama litapigwa tukio au halitapigwa,

Ila anaomba wamsitiri maana huu mchongo wa Siri kammegea tu maana anajua mengi ya yule nesi ila kaamua kumlinda jamaa maana Ni mengi mema kamfanyia ikiwemo kuokoa maisha ya mama Yake pale hospitali bill malipo yoyote. Jamaa kweli akakumbuka kua Kuna mama alikuja kazidiwa Hana pesa,akamtibia bure na kumfanyia mpango wa rufaa akapelekwa muhimbili kwa matibabu zaidi Ila Ni zaman sn ashasahau.


Boda akaongezea kua mpk sasa bunduki ishakua tayar na wakodishaji wa bunduki ile na risasi za baruti Ni maaskali wa pale pale mjini. Basi wakaachana nae, boda akapewa elfu 20 ya shukran na kumuahidi Kama ishu Ni kweli watampa elfu 80 ya ziada. Boda akasema sawa watamjuza.

Kweli usiku ule Jamaa akaenda kulala lodge,rafk Yake akaenda kulala nyumban kwake asubiri kushuhudia hilo tukio la ujambazi.

KESHO Yake kulipokucha Akampigia jamaa kua Mbona kuko salama, uyu boda atakua anadanganya au katumwa kukuseti TU uingie kingi. Basi wakakubaliana kua jamaa aendelee kubaki kule lodge ili Kama Kuna vitu dogo kaseti basi vifeli.
Kweli jamaa akaendelea kubaki lodge.

[emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa siku ya 3 tangu jamaa Yuko lodge, Asbuh KESHO yake jamaa anamfata lodge mbio mbio kua kule nyumban kwao wezi wamevamia Jana Yake na kupiga risasi juu, wamfunga mtaa na mlinzi wao kauwawa kwa mapanga na wamekuja kwa wapangaji nako wamevunja milango yote wapangaji wote wametolewa nje na kusachiwa na kuporwa Simu na pesa. Kumbe Yule bodaboda aliewatonya alikua sahii. Basi wakawaza Kwenda kuliripoti polisi, ikaonekana sio POA watakua wamemchoma boda aliewamegea hiyo siri. Basi Ikabd jamaa aendelee kujificha uko uko lodge. Rafiki akarudi eneo la tukio na kumuachia jamaa hella za matumizi.

KESHO yake jamaa kafatwa lodge na kuambiwa na rafki Yake kua yule Pusha mpangaj mwenzao alikua akimsema Sana yeye kua hili tukio huenda tumepigwa na mtu wa humu humu ndani, uyu dokta alikua akiishi na mwenzake kabla ya tukio na Sasa huyo mwenzake haonekani na siku ya tukio wote tumelazwa hapa nje. jamaa haonekani. Kwaiyo wapangaj wenzie wamemshukia wanataka jamaa aende polisi aeleze alipo rafki yake na wajue siku ya tukio alikua wapi uyo dokta mwenzake.

Dah! Ikabd kwanza wampigie boda wamweleze habar zile. Boda akawaambia Kama alivosema kua pusha ndie msoma ramani, lawama Ni kwamba pusha kawapotosha wenzie.

Sasa Hapo yanatafutwa mazingira kusahihisha makosa ya pusha ili jamaa aingie kwny mtego Tena amalizwe vizuri na hata hao polisi wanaotaka kukuhoji usikute ndio hao hao waliowaazimisha majambazi bunduki, usiende. Hapa Cha kufanya Ni kupotea TU, asithubutu Kwenda kituoni watakumalizia kabisa kimya kimya. Basi Ikabd usiku huo huo jamaa atoroke asafiri kurudi dar kwa kudandia malori ya kutokea Nairobi.

Baada ya kufika dar,
Rafk yake akampigia kua presha uku Ni kubwa hivi Sasa kawekwa ndani, hiyo yote ni kwa ajili yake, kwaiyo asirud uku ila aende TU akaripoti vituo vya polisi huku dar ili asipate matatizo na hiLi suala lijulikane kwa wakubwa wasije kumdhuru na yeye.

Kweli jamaa kaenda kujisalimisha Centro, kamtafuta askali anayemuamini na kumuelezea kila kitu. Afande akataka kumjua uyo boda, jamaa akasita kumtaja. Basi afande akasema atalifuatilia suala lake afu atamjuza kafikia wapi.

Baada ya MDA jamaa akasema Kama imeshindikana alipeleke mbele maana rafiki yake anasota ndani na ushahidi wote uko wazi khs zile njama. yule afande akamwambia jamaa asiwe na shaka,kila kitu Kiko sawa, kule kaskazini rafk Yake hatopata shida na ataachiwa kesho kutwa Ila na yeye asihangaike Sana Kwenda ngazi za juu. Amwachie yeye atalimaliza tu.

Basi kweli baada ya siku 2 rafki Yake jamaa akaachiwa na ile kesi ikawa imefutwa. Afande akamletea taarifa kua Cha kufanya atafute kazi huku dar, asirud Tena kule mkoani maana huenda maadui zake wakawa wanamuwinda Zaid. Jamaa akauliza maadui zake Ni wapi. afande akasema tuachane nayo,hayo Ni maoni yake TU kwa faida yake. Akiamua kuyafata ayafuate,akiona hayafai ayaache afanye anachokiona ni sahii. Bas jamaa akauchukua ushaur wa afande na hajurudi Tena mkoani Hadi leo.

KATAFUTA KAZI PENGINE na kwasasa kaajiliwa Taasisi Moja maalum ya kutibu magonjwa ya organ flani ya mwili.Kaoa ana watoto wawili na anaishi maisha mengine tofauti kabisa Ila anasema ilimchukua zaidi ya mwaka mzima kuishi na kutembea kwa amani kila sehem anapokua hapa dar kwa hofu ya kuwindwa au kuuwawa na huyo aliyekua MKE wake wa zamani uyo nesi.

######Mwisho######

My take:
Kuna la kujifunza hapa,
Hiii ni true story nmesimuliwa na mwanajf mwenzetu mkongwe humu MMU siku ya xmass tulipoonana live, akanambia baada ya kuisoma ile story ya yule mwanamke aliyewaua pole pole mume wake,mjamzito na mtoto kwa sumu kidg kdg. Naye Kashawishika, na ya kwake pia iletwe humu.

Aliomba nimsaidie kuweka vizur ktk maandishi,sio mwandishi mzuri ili wadau wake MMU na jf kiujumla wapate kuisoma na kujifunza. Nashkuru Mungu niliahidi ntatekeleza na leo nmemtimizia Hilo[emoji1431]

Kama Kuna kitu nmesahau ktk story yake atanikumbusha mwnyw kupitia comments (Kama atapenda Wana jf wamjue) au kwny pm (Kama hapendi kujulikana).

Kwa heshima na tahadhima,
NAWASILISHA WAKUU [emoji1431]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa siku ya 3 tangu jamaa Yuko lodge, Asbuh KESHO yake jamaa anamfata lodge mbio mbio kua kule nyumban kwao wezi wamevamia Jana Yake na kupiga risasi juu, wamfunga mtaa na mlinzi wao kauwawa kwa mapanga na wamekuja kwa wapangaji nako wamevunja milango yote wapangaji wote wametolewa nje na kusachiwa na kuporwa Simu na pesa. Kumbe Yule bodaboda aliewatonya alikua sahii. Basi wakawaza Kwenda kuliripoti polisi, ikaonekana sio POA watakua wamemchoma boda aliewamegea hiyo siri. Basi Ikabd jamaa aendelee kujificha uko uko lodge. Rafiki akarudi eneo la tukio na kumuachia jamaa hella za matumizi.

KESHO yake jamaa kafatwa lodge na kuambiwa na rafki Yake kua yule Pusha mpangaj mwenzao alikua akimsema Sana yeye kua hili tukio huenda tumepigwa na mtu wa humu humu ndani, uyu dokta alikua akiishi na mwenzake kabla ya tukio na Sasa huyo mwenzake haonekani na siku ya tukio wote tumelazwa hapa nje. jamaa haonekani. Kwaiyo wapangaj wenzie wamemshukia wanataka jamaa aende polisi aeleze alipo rafki yake na wajue siku ya tukio alikua wapi uyo dokta mwenzake.

Dah! Ikabd kwanza wampigie boda wamweleze habar zile. Boda akawaambia Kama alivosema kua pusha ndie msoma ramani, lawama Ni kwamba pusha kawapotosha wenzie.

Sasa Hapo yanatafutwa mazingira kusahihisha makosa ya pusha ili jamaa aingie kwny mtego Tena amalizwe vizuri na hata hao polisi wanaotaka kukuhoji usikute ndio hao hao waliowaazimisha majambazi bunduki, usiende. Hapa Cha kufanya Ni kupotea TU, asithubutu Kwenda kituoni watakumalizia kabisa kimya kimya. Basi Ikabd usiku huo huo jamaa atoroke asafiri kurudi dar kwa kudandia malori ya kutokea Nairobi.

Baada ya kufika dar,
Rafk yake akampigia kua presha uku Ni kubwa hivi Sasa kawekwa ndani, hiyo yote ni kwa ajili yake, kwaiyo asirud uku ila aende TU akaripoti vituo vya polisi huku dar ili asipate matatizo na hiLi suala lijulikane kwa wakubwa wasije kumdhuru na yeye.

Kweli jamaa kaenda kujisalimisha Centro, kamtafuta askali anayemuamini na kumuelezea kila kitu. Afande akataka kumjua uyo boda, jamaa akasita kumtaja. Basi afande akasema atalifuatilia suala lake afu atamjuza kafikia wapi.

Baada ya MDA jamaa akasema Kama imeshindikana alipeleke mbele maana rafiki yake anasota ndani na ushahidi wote uko wazi khs zile njama. yule afande akamwambia jamaa asiwe na shaka,kila kitu Kiko sawa, kule kaskazini rafk Yake hatopata shida na ataachiwa kesho kutwa Ila na yeye asihangaike Sana Kwenda ngazi za juu. Amwachie yeye atalimaliza tu.

Basi kweli baada ya siku 2 rafki Yake jamaa akaachiwa na ile kesi ikawa imefutwa. Afande akamletea taarifa kua Cha kufanya atafute kazi huku dar, asirud Tena kule mkoani maana huenda maadui zake wakawa wanamuwinda Zaid. Jamaa akauliza maadui zake Ni wapi. afande akasema tuachane nayo,hayo Ni maoni yake TU kwa faida yake. Akiamua kuyafata ayafuate,akiona hayafai ayaache afanye anachokiona ni sahii. Bas jamaa akauchukua ushaur wa afande na hajurudi Tena mkoani Hadi leo.

KATAFUTA KAZI PENGINE na kwasasa kaajiliwa Taasisi Moja maalum ya kutibu magonjwa ya organ flani ya mwili.Kaoa ana watoto wawili na anaishi maisha mengine tofauti kabisa Ila anasema ilimchukua zaidi ya mwaka mzima kuishi na kutembea kwa amani kila sehem anapokua hapa dar kwa hofu ya kuwindwa au kuuwawa na huyo aliyekua MKE wake wa zamani uyo nesi.

######Mwisho######

My take:
Kuna la kujifunza hapa,
Hiii ni true story nmesimuliwa na mwanajf mwenzetu mkongwe humu MMU siku ya xmass tulipoonana live, akanambia baada ya kuisoma ile story ya yule mwanamke aliyewaua pole pole mume wake,mjamzito na mtoto kwa sumu kidg kdg. Naye Kashawishika, na ya kwake pia iletwe humu.

Aliomba nimsaidie kuweka vizur ktk maandishi,sio mwandishi mzuri ili wadau wake MMU na jf kiujumla wapate kuisoma na kujifunza. Nashkuru Mungu niliahidi ntatekeleza na leo nmemtimizia Hilo[emoji1431]

Kama Kuna kitu nmesahau ktk story yake atanikumbusha mwnyw kupitia comments (Kama atapenda Wana jf wamjue) au kwny pm (Kama hapendi kujulikana).

Kwa heshima na tahadhima,
NAWASILISHA WAKUU [emoji1431]

Sent using Jamii Forums mobile app
Daaah haya maisha haya[emoji25][emoji25]
 
Back
Top Bottom