DOCTOR: Kwa Damu yako hii na Mke wako, Kamwe Hamuwezi kupata mtoto/watoto!

iPad ya Apple

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2013
Posts
322
Reaction score
126
Wana JF poleni na shughuri za Kila cku! Nimejitokeza Mbele yenu kuomba Masada kufuatia majibu tuliyopata kutoka kwa Dk mmoja. Ni hivi Mimi na Mke wangu tangu tumefunga ndoa sasa ni zaidi ya Mwaka mmoja na nusu Mke wangu alihangaika sana kupata ujauzito lakini baada Kama ya miezi 6 alifanikiwa mimba ikanasa.

Tulipata furaha sana baada ya kuomba sana na hatimaye Mungu akajibu maombi yetu, kwa bahati mbaya sana furaha ilidumu kwa miezi 2 tu kwani wife alijikuta amepata tatizo la miscarriage. Ilibidi twende hospitali alisafishwa salama, lakini ikabidi tuombe ushauri kwa Dk kwanini hii Hali imetokea ndipo Dk ktk kumuuliza wife Kuwa alitumia kitu gani eg. Chakula au kinywaji kilichopelekea Hali hii? Basi ktk mahojiano ya muda mrf na Dk ilibainika Kuwa wife kuna cku alitumia vitunguu swaumu vilivyopondwapondwa akachanganya na asali akala, hii ni kawaida yake kwani anapopata homa ndogo hutumia vitu hvyo huwa hapendi kutumia dawa za hospital.basi Dk aka conclude Kuwa ndo chanzo cha miscarriage.

Baada ya miezi 2 akapata tena ujauzito uliodumu kwa miezi 3 tu nao ukatoka, tukaenda tena hospital na Dk akatupima magrupu ya Damu zetu wote vipimo vikasema tuna Damu Group A positive na ndipo akasema kwa Damu zenu hizi Hamuwezi kupata mtoto. Ikitokea Mke wangu akapata ujauzito hadi hatua ya kujifungua basi atajifungua Kiumbe ambacho c riziki na hata kikiwa riziki basi mtoto huyo atafariki baada ya muda Fulani sababu Damu zenu hazipatani yaani positive na positive lazima zikwepane.

NB. Damu zetu Kuwa Group A positive simaanishi Kuwa ni HIV Positive la hasha!

Ngugu zangu naombeni msaada wenu kwani ndoa Yangu sasa ipo mashakani hakuna mwenye furaha ni simanzi na majonzi tu Kila cku. Kosa lilifanyika kwa kutopima magrupu ya Damu zetu mapema Kabla ya kufunga Ndoa. Naombeni msaada wenu Jamani.
 
Dah, poleni sana, kweli inauma sana. Ila nashangaa how comes hizo group za damu zisiendane, angali zamani kilichokuwa kinasumbua ni group za negative (mambo ya rhesus factor) na ambazo pia siku hizi kuna utaalam na wanazaa kawaida na mtoto anaishi. Subiri wataalam watakujibu. Ila hata kama mngekuwa negative nakuambia NOTHING IS IMPOSIBLE BEFORE GOD na wala usikate tamaa
 
Suala la kutokea kwa sponteneous miscarriage kwa mkeo involves a lot of factors (work shop of factors sio suala la ku conclude tu kwa maandishi ambayo umeandika zinahitajika details za kuhojiwa pia mke wako pamoja na vipimo vya kidaktari kibao...sio damu peke yake,inahitajika mpime au Apime ultrasound ili ijulikane ana fibroids,congenital abnormalities n.k pamoja na vipimo kibao vya maabara eg VDRL,Antibodies)
Kwa ushauri tu naomba u google factors for sponteneous Abortion or Miscarriage soma nadhani utapata idea ya nn naeleza then come back na details then uulize wapi hujaelewa

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Asante mkuu pia tumeshapima hicho kipimo cha VDRL, kisonono na kichocho majibu yalikuwa negative.
 
Kwenye matatizo ya uzazi usiwe unaamini sana conclusion za dakta mmoja tu. Madaktari huwa wanazidiana ujuzi wa kujua tatizo na kutibu. Kuna mtu ninayemfahamu dakta aliwahi kumwambia mkewe hana kizazi. Alipoenda kwa dakta mwingine alipewa ushauri na dawa. Sasa wana watoto wawili!.
 
Asante mkuu pia tumeshapima hicho kipimo cha VDRL, kisonono na kichocho majibu yalikuwa negative.

Mkuu huyo uliyeenda kwake sio daktari, ni janga. Hakuna magroup ya damu yanayokinzana kupata mimba. Rhesus +ve na Rhesus -ve zinakinzana, lakini kwa utaalamu wa sasa (kama alivyoeleza mchangiaji hapo juu), matibabu spesheli hufanywa na mtoto huzaliwa.
Kuna mawili: Labda mke wako ni R -ve na wewe ni R+ve, may be hukumuelewa Dr. Kapime tena na kama ndivyo muende hpstali kubwa mtasaidiwa.
Vinginevyo Itakuwa mkeo au wewe kuna tatizo la kiafya. Nakushauri utumie dawa za mimea zaidi (kuna member humu alileta thread juu ya clinic fulani ipo shekilango, itafute)...
 
Maelezo yaliyotolewa sio ya kitaalam. Hilo la kitunguu swaumu na la group la damu hayana maelezo ya kutosha kitaalam.

Jaribu kuhakikisha kuwa anayekuhudumia ni daktari.

Nimeona video kuwa kuna watu wanafungua vituo feki vya huduma na kufanya mpaka operation! Mmoja wao kafunguliwa kesi tayari, alikuwa Mbezi na kibanda chake cha huduma. Watu wa namna hii wanaweza kutoa maelezo yasiyo ya kisayansi kama haya uliyoandika hapa.
 
Mie ni B+ na wife ni B+,mtoto wetu kaanza baby class mwezi huu..........huyo si daktari hata kidogo.....
 
Nenda kaonane na gynae watatu wengine na usikie watakuambia nini. Kabla haujajitia hofu. Uko mkoa gani tukupe recommendation?
 
poleni sana wahusika wahii kitu, ni kweli kwani hata tafiti zinaoensha kuwa binadamu wenye damu tajwa duniani ni wachache sana. ila msikate tamaa endeleeni kutafuta ushauri na vipimo nadhani kuna siku mtafanikia kupata suruhu ya jambo lenu.
 
Wana JF poleni na shughuri za Kila cku! Nimejitokeza Mbele yenu kuomba Masada kufuatia majibu tuliyopata kutoka kwa Dk mmoja. Ni hivi Mimi na Mke wangu tangu tumefunga ndoa sasa ni zaidi ya Mwaka mmoja na nusu Mke wangu alihangaika sana kupata ujauzito lakini baada Kama ya miezi 6 alifanikiwa mimba ikanasa.

Tulipata furaha sana baada ya kuomba sana na hatimaye Mungu akajibu maombi yetu, kwa bahati mbaya sana furaha ilidumu kwa miezi 2 tu kwani wife alijikuta amepata tatizo la miscarriage. Ilibidi twende hospitali alisafishwa salama, lakini ikabidi tuombe ushauri kwa Dk kwanini hii Hali imetokea ndipo Dk ktk kumuuliza wife Kuwa alitumia kitu gani eg. Chakula au kinywaji kilichopelekea Hali hii? Basi ktk mahojiano ya muda mrf na Dk ilibainika Kuwa wife kuna cku alitumia vitunguu swaumu vilivyopondwapondwa akachanganya na asali akala, hii ni kawaida yake kwani anapopata homa ndogo hutumia vitu hvyo huwa hapendi kutumia dawa za hospital.basi Dk aka conclude Kuwa ndo chanzo cha miscarriage.

Baada ya miezi 2 akapata tena ujauzito uliodumu kwa miezi 3 tu nao ukatoka, tukaenda tena hospital na Dk akatupima magrupu ya Damu zetu wote vipimo vikasema tuna Damu Group A positive na ndipo akasema kwa Damu zenu hizi Hamuwezi kupata mtoto. Ikitokea Mke wangu akapata ujauzito hadi hatua ya kujifungua basi atajifungua Kiumbe ambacho c riziki na hata kikiwa riziki basi mtoto huyo atafariki baada ya muda Fulani sababu Damu zenu hazipatani yaani positive na positive lazima zikwepane.

NB. Damu zetu Kuwa Group A positive simaanishi Kuwa ni HIV Positive la hasha!

Ngugu zangu naombeni msaada wenu kwani ndoa Yangu sasa ipo mashakani hakuna mwenye furaha ni simanzi na majonzi tu Kila cku. Kosa lilifanyika kwa kutopima magrupu ya Damu zetu mapema Kabla ya kufunga Ndoa. Naombeni msaada wenu Jamani.

Duh, huyo Doctor mbona mimi simwelewi? Hebu kwanza tazama hii?

ABO2.jpg

Rh.jpg

Paternity_Blood_type_Chart.jpg
 
mkuu nashukuru kwa Hiyo chati ya ufafanuzi hakika imetupa Amani hapa nyumbani , kwani toka tumeambiwa hivyo na daktari, wife amekuwa mtu wa kulia tu Kila cku, nimijuunga JF 21july 2013. Kwasasabu ya kutafuta ushaur naona sasa naweza kufanikiwa zaidi. Aksanteni wakuu.
 
mh hao ni ni ma gynecologist kweli ? kama moja wenu angekuwa negative labda ingeweza kuwa sababu ambayo pia siku hizi inatibika na watu wanapata watoto, mimi na mwenzangu wote ni o+ na tuna watoto, swala la kuwa wazazi wote ni + sidhani kama ni sababu kabisa, nakushauri uende kwa madaktari bingwa wa wanawake na uzazi zaidi ya watatu utapata suluhu. wala usivunjike moyo so long as ana uwezo wa kuconcive naamini mtapata mtoto. labda ungesema upo mkoa gani ili hata watu wakushauri madaktari wazuri unaoweza kuwaona na wakakusaidia. usikate tamaa
 
Mie ni B+ na wife ni B+,mtoto wetu kaanza baby class mwezi huu..........huyo si daktari hata kidogo.....

mimi Ni A+ na mume wangu pia A+ !na tuna watoto wawili mmoja yuko secondary school! na sikuwahi kusikia wala kuambiwa kuwa damu zetu haziendani! na wala sijawahi kupata miscarriage! ndo kwanza nasikia leo hii na wala siamini kabisa,labda Kuna sababu ambayo mmoja wenu kaomba isiwekwe wazi, so Dr kaamua kuwaambia uongo ambao kwa akili zake akadhani hamtafuatilia kujua ukweli!
 
Ila kwa kweli kwa jinsi mie nilivyo na maswali kwa madaktari.....huyo daktari ingembidi kuleta ubao anieleweshe....yaan unadanganywa kirahisi namna hiyo....!!!No wonder biology ikawa compulsory!!!
 
mh hao ni ni ma gynecologist kweli ? Kama moja wenu angekuwa negative labda ingeweza kuwa sababu ambayo pia siku hizi inatibika na watu wanapata watoto, mimi na mwenzangu wote ni o+ na tuna watoto, swala la kuwa wazazi wote ni + sidhani kama ni sababu kabisa, nakushauri uende kwa madaktari bingwa wa wanawake na uzazi zaidi ya watatu utapata suluhu. Wala usivunjike moyo so long as ana uwezo wa kuconcive naamini mtapata mtoto. Labda ungesema upo mkoa gani ili hata watu wakushauri madaktari wazuri unaoweza kuwaona na wakakusaidia. Usikate tamaa

nipo mwanza mkuu. Nashukuru kwa msaada.
 
Back
Top Bottom