kama kuna mechanism hapo wamenishika...
Dogo nenda kapige shule hiyo, acha uzembe. So far naweza kukuhakikishia kuwa, katika kozi zote zilizoko SUA. BVM au Bachellor of Veterinary Medicine ndo inalipa zaidi na inauhakika wa kazi. Hata ngazi ya mshahara wake katika rank za serikali iko mbali ukilinganisha na taaluma nyingine. Wakati wengine wanaanzia TGSD, Vet doc anaanzia TGSF, big difference. Maeneo yake ya kufanya kazi ni kama ifuatavyo:
1. Kama muajiriwa wa serikali ukiwa kama daktar wa mifugo wa wilaya
2.Tanzania foods and drugs authority
3.Reserch institutes/ Medical and Veterinary e.g. National institute for Medical research, Ifakara health Institute,Animal health research institutes etc
3.Drugs companies - eg.ANUPCO, KELA,(These are international drugs companies operating in Tanzania),etc
4.Interchick, Amadori, Kenchick and other poultry producing companies
5.TBS - Toxicologist
6. Zaidi ya yote, ni miongoni mwa taaluma chache sana zenye room kubwa ya self employment, kwa maana ya kutibu au kuanzisha shamba lako la mifugo, ukitake advantage ya utaalamu wako (This is rarely done kutokana na nature yetu watanzania).
Kwa hiyo kijana, nenda kapige shule, Mimi nimesoma veterinary medicine SUA sasa hivi nipo Rwanda nafanya kazi huku katika taasis ya utafiti wa magonjwa ya binadamu namshukuru mungu. Wenzangu niliosoma nao pale SUA wakiwa course nyingine, huku wakitucheka BVMs kwa kuwa tulikuwa bize na hakuna muda wa kusocialize kivile, wengi wao ni mabank teller hapo DSM.
ZINGATIO:
Hii kozi si ngumu, ila inahitaji kujitoa kidogo, kwa maana hakuna muda wa kupotea hivihivi.Hii ni nature ya any medical related course, there is alot of stuffs to read, with limited time. Kama unawasiwasi na uwezo wako wa kujitoa kwa ajili ya kazi moja tu, yaani masomo, nakushauri uiondoe kwenye machaguo yako hii kozi, kwani hata semester mbili hutomaliza.
Fanya uchaguzi sahihi kwa ajili ya hatma ya maisha yako. Kamwe usije kujutia uchaguzi wako.