Doctors nisaidieni dawa ya kusafisha figo na mfumo mzima wa mkojo

Doctors nisaidieni dawa ya kusafisha figo na mfumo mzima wa mkojo

Mr Suprize

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2014
Posts
869
Reaction score
961
Habari zenu wakuu!
Samahani naomba msaada wa jina la dawa inayopatikana phamarcy au kwenye maduka ya dawa inayoweza kusafisha figo na mfumo mzima wa mkojo ili nikainunue..pia kwa wale wanaozijua dawa za asili msisite kushare uzoefu wenu na wapi zinaweza kupatikana hizo dawa.

Natanguliza shukrani zangu
 
Figo zako zina uchafu wa aina gani.?Tuanzie hapo
 
Ungesema tatizo linalokusumbua ungepata msaada vizuri zaidi. Kwa niaba ya Joseverest
tatzo ni kwamba kuna maumivu nyuma ya mgongo maeneo ya figo , pia ukinibana mkojo kuna maumivu makali nayapata maeneo hayo ya figo, so naamini mfumo wa mkojo kwa ujumla unauchafu
 
tatzo ni kwamba kuna maumivu nyuma ya mgongo maeneo ya figo , pia ukinibana mkojo kuna maumivu makali nayapata maeneo hayo ya figo, so naamini mfumo wa mkojo kwa ujumla unauchafu
Umeenda hospital kupima?
 
Ungepima kwanza upate kujua tatizo hasa ni nini ili uweze kupata ushauri/matibabu sahihi.
 
Kunywa maji mengi tuu...kwasiku walau lita 4 kiendelea
 
nakunywa maji mengi sana nahisi yanapelekea matatizo kwenye figo na mfumo wa mkojo
Kunywa maji mengi ni vizuri kwa afya ya figo.Mtu inabidi anywe walau lita moja na nusu kwa siku.

Iwapo una kiu kali na mwili unachoka sana na hamu ya kula imeongeka na unakojoa mkojo mwingi kuliko kawaida basi ukapime ugonjwa wa kisukari.
 
Sawa mkuu ,tukiachana na kunywa maji kwa hiyo hakuna dawa iliyopo phamarcy inayosaidia kusafisha figo?

Sent from my 5023F using JamiiForums mobile app
 
Tumia maji mengi na Aloe vera itakusaidia...

Ukiwa unafanya hivyo nenda hospitali ukapimwe kabisa ijulikane dawa gani wakupe..

Pole sana ndugu
 
Figo ni very sensitive organ nenda kaonane na maspecialist watakupima na kukupa ushauri sahihi.
 
Ndugu acha kabisa swala linaitwa uginjwa wa figo,mm yalinikuta ila paka sasa niko poa
1.Tambua kwamba figo lina athiriwa Na vitu vingine,kama matumiz ya dawa za kutuliza maumivu kwa muda mrefu,matumiz ya dawa ya asili,presha ya kudumu isiyotumiwa dawa,matumiz makubwa ya pombe kali n.k
Dalili maumivu ya mgongo,homa kali,kuishiwa pumzi,kuchoka sana,kusikia radha tofaut ya mdomo,kukosa mkojo,mwili kuvimba hasa miguuni Na usoni.

Figo haina dawa ya kusafisha asikudanganye mtu,mm nilienda paka India,matibabu ya figo ni dialysis yan kuchuja damu kwa nje Na ni ghar sana kwa wiki ni unatakiwa kufanya mara 3na kila session ni 230,000.ni swala endelevu paka utakapokuja pandikiziwa figo lingine,nakushaur kapime ila kwasasa kazana sana kula matango,yikiti maji,punguza sana chumvi,ni fate inbox nipe namba yako nitakuelekeza mengi zaid,ila nakushaur usilogwe kutumia sawa asilia kwa sasa utaua kabisa hizo figo
 
Back
Top Bottom