Documentary kupitia Azam Max si Yanga TV

MTAZAMO

JF-Expert Member
Joined
Feb 8, 2011
Posts
19,675
Reaction score
33,583
Wakuu,

Hizi timu zinaendeshwa kihuni sana sometimes! Wakati sisi Simba pamoja na raha tulizopata kwa usajili first class lakini tusisahau swala la ujenzi wa uwanja Bunju ni kama limekufa na hatujui kinachoendelea na hata issue ndogo ya kuzungusha walau ukuta ilipofikia hatuna taarifa rasmi.

Lakini wakati Lunyasi tukikumbushana hayo majanga, jamaa zetu wa jangwani walizindua Yanga TV kwa mbwembwe kubwa tukajua wenzetu wapo serious. Lakini kichekesho hata hiyo documentary yao inabidi ulipie Azam Max kuiona sio Yanga TV achilia mbali hata kujua maendeleo yake.

Anyway, pamoja na utani wetu wa jadi lakini ni vizuri tuwe na muendelezo mzuri kwenye projects zetu. Projects zinatangazwa kwa nguvu kubwa alafu baada ya muda hatuoni nguvu ikuwekwa huko.
 
Kwa wewe unaona kihuni sababu hutumii akili, we hujjui kuwa kwenye App hela inaingia kwa Yanga alafu baadae ndo itawekwa kwenye Yanga tv/Youtube
 
Wewe mwenye akili umeiangalia documentary wapi? Hiyo Yanga TV unajua kipindi chake hata kimoja?
 
Kama utawala wa Nchi ni mbovu ata sekta nyingine zitakuwa ovyo
 
Nadhani yanga waliingia mkataba na Azam Tv kuhusu umiliki wa matukio yote yanayoihusu yanga. Hiyo documentary nadhani inaingia humo, Azam ndio mwenye kuamua kila kitu. Ndio maana hata mechi vs kaizer chiefs Azam ndio walitoa baraka zote kwa super sport kuonyesha ile mechi.
 
Hata Yanga TV YouTube hakuna hiyo documentary acha fix. Alafu hizi fix zinakusaidia nini?
Documentary ni chanzo cha mapato pia haiwezi kuwekwa youtube wakati Azam media wana platform ya kulipia kwenye App yao na pesa inaingia, pia yanga wana mkataba na Azam media kuhusu haki miliki ya matangazo yake, nyie wapenda vya bure subiri iwekwe Youtube
 
Nadhani yanga waliingia mkataba na Azam Tv kuhusu umiliki wa matukio yote yanayoihusu yanga. Hiyo documentary nadhani inaingia humo, Azam ndio mwenye kuamua kila kitu. Ndio maana hata mechi vs kaizer chiefs Azam ndio walitoa baraka zote kwa super sport kuonyesha ile mechi.
Kwakuwa umesema unadhani nitaheshimu hilo. Kama michezo ambayo hatuna watu wasiojulikana hatuwezi kufikiri nje ya box tutaweza siasa kweli? Hivi unaamini matukio yote ya Yanga yanamilikiwa na Azam TV pekee? Kwamba hadi documentary ni swala la kimkataba?
 
Mbona jamaa kaelezea vizuri Sana. Na akichoelezea ndo Hali halisi
 
Hawa ndio Yanga wenye akili, nyie mnaofikiri muda wote ni kubishana Simba na Yanga endeleeni.
Screenshot_20230808_221106.jpg
 
Kwakuwa umesema unadhani nitaheshimu hilo. Kama michezo ambayo hatuna watu wasiojulikana hatuwezi kufikiri nje ya box tutaweza siasa kweli? Hivi unaamini matukio yote ya Yanga yanamilikiwa na Azam TV pekee? Kwamba hadi documentary ni swala la kimkataba?
Nimejaribu tuu kuwaza maana tuliambiwa mkataba wa Yanga na Azam media unahusu ushirikiano wa maudhui. Je kuna mipaka yoyote katika huo ushirikiano au maudhui yote ya Yanga lazima Azam media wahusike?. Sijui mkataba unasemaje ila najua Documentary ni mojawapo ya maudhui.
 
Hizi timu zetu kuna muda lazima tuwaulize maswali magumu ili waache maamuzi ya kijinga. Mfano sisi Simba, Viongozi waliamua Kakolanya asicheze bila kujali umuhimu wa mechi zilizo mbele! Ikatugharimu Morocco game ya kuvuka kwenda nusu fainali. Sasa hivi tetesi zinatembea issue ya Phiri issue sio kocha ni kiongozi anamkomoa mchezaji! Ujinga tu!
 
Kwakuwa umesema unadhani nitaheshimu hilo. Kama michezo ambayo hatuna watu wasiojulikana hatuwezi kufikiri nje ya box tutaweza siasa kweli? Hivi unaamini matukio yote ya Yanga yanamilikiwa na Azam TV pekee? Kwamba hadi documentary ni swala la kimkataba?
Yanga wana mkataba na Azam TV juu ya haki za matangazo hivyo kila shughuli za Yanga zinazo husu broadcasting ni mali ya Azam TV

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Wakuu,

Hizi timu zinaendeshwa kihuni sana sometimes! Wakati sisi Simba pamoja na raha tulizopata kwa usajili first class lakini tusisahau swala la ujenzi wa uwanja Bunju ni kama limekufa na hatujui kinachoendelea na hata issue ndogo ya kuzungusha walau ukuta ilipofikia hatuna taarifa rasmi.

Lakini wakati Lunyasi tukikumbushana hayo majanga, jamaa zetu wa jangwani walizindua Yanga TV kwa mbwembwe kubwa tukajua wenzetu wapo serious. Lakini kichekesho hata hiyo documentary yao inabidi ulipie Azam Max kuiona sio Yanga TV achilia mbali hata kujua maendeleo yake.

Anyway, pamoja na utani wetu wa jadi lakini ni vizuri tuwe na muendelezo mzuri kwenye projects zetu. Projects zinatangazwa kwa nguvu kubwa alafu baada ya muda hatuoni nguvu ikuwekwa huko.
unajua usiongee kitu bila kuwa na ufahamu,yanga tv sio popular kama azam max ambayo ni mastufu dunia nzima yanga inataka kipayo sio sifa
 
Back
Top Bottom