Dodoma: Auawa na polisi baada ya kuwashambulia kwa mishale iliyohisiwa kuwa na sumu

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2021
Posts
1,147
Reaction score
2,008
Jeshi la polisi limethibitisha kuuawa kwa risasi Nada Songo(45), mkazi wa wilaya ya Chemba, katika harakati za kumkamata baada ya kuwashambulia askari na wananchi kwa mishale iliyodhaniwa kuwa na sumu.

Kamanda wa Polisi Mkoani humo, Martin Otieno amesema mtuhumiwa alifariki mara baada ya kupigwa risasi na askari maeneo ya kifuani na mguu wa kulia wakati akiwashambulia askari hao kwa mishale Agosti 28. Ameongeza kuwa marehemu alikuwa anakaidi kukamatwa baada ya kutuhumiwa kutishia kuua raia kwa silaha za jadi mnamo Agosti 27.

......................................

Mkazi wa kijiji cha Chioli, kata ya Songolo wilayani Chemba, Mkoa wa Dodoma, Nada Songo (45), ameuawa na Jeshi la Polisi kwa kosa la kuwashambulia askari na wananchi kwa mishale yenye sumu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Agosti 29, 2022, Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma, Martin Otieno amesema jana Jumapili mtuhumiwa huyo alifanya matukio hayo katika kijiji hicho.

Amesema mtuhumiwa huyo amefariki mara baada ya kupigwa risasi na askari maeneo ya kifuani na mguu wa kulia wakati akiwashambulia askari hao kwa mishale inayodhaniwa kuwa na sumu.

Amesema marehemu alikuwa anakaidi kukamatwa kuhusiana na kosa ambalo alikuwa anatuhumiwa nalo la kutishia kuwaua wananchi kwa silaha za jadi.

Amesema chanzo cha tukio hilo ni Agosti 27, 2022, mtuhumiwa alishambulia wanakijiji kwa kuwatishia kwa mishale yenye sumu. “Askari polisi walipokwenda kwa ajili ya ukamataji, mtuhumiwa alitoroka na kukataa amri halali ya kukamatwa kuhusiana na makosa yake."

Amesema Agosti 28, 2022 polisi walipata taarifa ya kurejea kwa mtuhumiwa huyo huku akiendelea kutishia usalama wa watu katika kitongoji hicho.Kamanda Otieno amesema askari walipokwenda kumkamata aliwashambulia kwa kutumia mishale ambayo inadhaniwa ina sumu na kumjeruhi askari namba H.9377 PC William.

Amesema askari huyo amejeruhiwa tumboni upande wa kushoto na akari wa akiba aitwaye Madodo Juma ambaye alijeruhiwa kwa mshale mguu wa kulia.

Chanzo: Mwananchi
 
Bottom line we have a very trigger happy men's in uniforms, ndio maana tunahitaji Katiba mpya,hapa hii case police ni suspect means hawawezi kujichunguza, IPID ndio ingechunguza case hii,but tumo in a shithole country aliyepigwa risasi kesha kuwa another statistics
 
Tozo zote hizi kwa nini wachunguze na kuwapa mzigo mzito walipa kodi? Bora jamaa katangulia atuachie ugali.
 
Pumbavu sana wewe na katili mno, na sijui kama unajumuika kwenye nyumba za ibada, wewe umesikia only one side of the story na tayari umefanya uamuzi wako wa kishenzi, elewa nchi hii political leaders are living large in the sea of poverty, na hali inakua mbaya zaidi na upumbavu wa working class kama wewe
 
Tayari nimeshakuwini kisaikolojia
 
Polisi mimi siwezi kuwaamini kenge nyie haiwezekani umpige mtu risasi ya kifuani wakati hana silaha ya moto.

mambo mengine mngekua mnakaa tu kimya
Wee jamaa daah!!
Ivi unajua maana ya silaha? Unajua mshale wa sumu ukoje??
 
Jeshi la polisi limethibitisha kuuawa kwa risasi Nada Songo(45), mkazi wa wilaya ya Chemba, katika harakati za kumkamata baada ya kuwashambulia askari na wananchi kwa mishale iliyodhaniwa kuwa na sumu.

Kamanda wa Polisi Mkoani humo, Martin Otieno amesema mtuhumiwa alifariki mara baada ya kupigwa risasi na askari maeneo ya kifuani na mguu wa kulia wakati akiwashambulia askari hao kwa mishale Agosti 28. Ameongeza kuwa marehemu alikuwa anakaidi kukamatwa baada ya kutuhumiwa kutishia kuua raia kwa silaha za jadi mnamo Agosti 27.

......................................

Mkazi wa kijiji cha Chioli, kata ya Songolo wilayani Chemba, Mkoa wa Dodoma, Nada Songo (45), ameuawa na Jeshi la Polisi kwa kosa la kuwashambulia askari na wananchi kwa mishale yenye sumu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Agosti 29, 2022, Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma, Martin Otieno amesema jana Jumapili mtuhumiwa huyo alifanya matukio hayo katika kijiji hicho.

Amesema mtuhumiwa huyo amefariki mara baada ya kupigwa risasi na askari maeneo ya kifuani na mguu wa kulia wakati akiwashambulia askari hao kwa mishale inayodhaniwa kuwa na sumu.

Amesema marehemu alikuwa anakaidi kukamatwa kuhusiana na kosa ambalo alikuwa anatuhumiwa nalo la kutishia kuwaua wananchi kwa silaha za jadi.

Amesema chanzo cha tukio hilo ni Agosti 27, 2022, mtuhumiwa alishambulia wanakijiji kwa kuwatishia kwa mishale yenye sumu. “Askari polisi walipokwenda kwa ajili ya ukamataji, mtuhumiwa alitoroka na kukataa amri halali ya kukamatwa kuhusiana na makosa yake."

Amesema Agosti 28, 2022 polisi walipata taarifa ya kurejea kwa mtuhumiwa huyo huku akiendelea kutishia usalama wa watu katika kitongoji hicho.Kamanda Otieno amesema askari walipokwenda kumkamata aliwashambulia kwa kutumia mishale ambayo inadhaniwa ina sumu na kumjeruhi askari namba H.9377 PC William.

Amesema askari huyo amejeruhiwa tumboni upande wa kushoto na akari wa akiba aitwaye Madodo Juma ambaye alijeruhiwa kwa mshale mguu wa kulia.

Chanzo: Mwananchi
Askali wetu nao ni vilaza sana,yaani mtu ana mshale,mnapiga risasi mnaua?!kwanini msipige risasi ya begani au bomu la machozi,au tumieni mbwa amkamate,kila kitu nchi hii ni bandia na hovyo kabisa,Cha maana nchi hii ni Diamond na Tundu lisu tu.
 
sawa !
ila una bunduki unaweza ukatishwa na mwenye mshale ?

kwa nini wasimpige hata ya bega au mguu nk. ?

unaua kabisa ?

na mbona hawasemi chanzo cha kufanya vurugu ni nini ?
Wee jamaa daah!!
Ivi unajua maana ya silaha? Unajua mshale wa sumu ukoje??
 
Kuna wana hawajui mshale wa sumu ulivo...ukikupata ata kidogo walah huponi...kwanza testing tu ya sumu yake ukijikata alafu damu ianze kutiririka..halafu ukaweka mshale wenye sumu chini ya jeraha linalovuja damu..damu inarudi juu kuikimbia sumu...sasa imagine.ikikupata...

NB: ndugu zetu nao hawaaminikagi
 
Back
Top Bottom