Dodoma City vs Arusha City (The Battle of Tanzania Capital City vs EAC Capital City)

Kuhusu bwawa nadhani umewahi sikia mradi wa bwawa la Farkwa ,Hilo ondoa shaka litakuwa kubwa kuliko hata Kidunda Dam.

Pesa ilipatikana ila nashani wanaendelea na mambo ya clearance sijui mazingira na mambo kama hayo..

Hayo mengine ni minor issues have nothing to do with the economy.
 
Broo Kwa taarifa Yako ,idara na taasisi za serikali zilizohamia Hadi Sasa ni chini ya 70% ,zinahamia Kwa stage kadiri ya serikali inavyopata pesa.

Kwa hiyo kuhusu ujenzi Bado upo saaana achilia mbali miundombinu mingine ya Kisasa ambayo inaendelea na itakayokuja Hadi Mji ufanane na Makao Makuu ya Nchi.

Huko baadae Balozi zote zinatakiwa kuhamia Dom,kinachokwamisha ni kwamba hakuna Airport Bado na taasisi zingine nyeti za kiusalama Bado hazijakamilisha kuhamia in full.
 
Uwekezaji wa viwanda na biashara unaofanyika dodoma ni mkubwa tu hii ni mbali na ujio wa serikali kama unavosema wewe, dodoma sasa ina wawekezaji wengi sana....Arusha ikasome tena chekechea, Mwanza bado sana kwa dodoma ya sasa...Dar es salaam ilishakuwa siku nyingi dodoma iko njiani kuitafuta dar japo siku dodoma inakuwa kama dar tutegemee morogoro, pwani nayo kuwa miji mikubwa.
 
..yaani mkuu unaamini kabisa kukiwa na airport mpya dom basi balozi zitahamia?ahahahah..sasa hv si airport ipo au mpaka International Airport?..well fahamu tu hata ikijengwa International Airport sio kigezo cha balozi kujaribu hata kuhamia dom..majirani tu hapo uganda embassy zote zipo kampala ila International airport ipo entebbe!..so preferred international airport kwa tz bado itabakia kuwa dsm na KIA kwa miaka mingi sana..sioni International flights zikija dom wakati hakuna abiria wa kutosha..hizi mambo ni economy na sio siasa!
 
Acha kuchekesha mkuu eti hakuna abiria wa kutosha yaani Dodoma ikose abiria wakati ni makao makuu ya serikali,chama(maamuzi yote makubwa ya kitaifa/kinchi hufanyika Dodoma utake usitake),bunge,mahakama,idara zote za serikali(fikiria idadi ya watumishi wa serikali na wageni wengine wanaoenda Dom kilasiku kwenda kusolve issues zao) ,taasisi zote za serikali,wafanyabiashara,wafanyakazi,wawekezaji,vyuo vikuu,viwanda plus uwekezaji mkubwa wa serikali.
Just imagine kama Mbeya wamejengewa Songwe International Airport ....Dodoma kwa hizo added advantages walizonazo walipaswa kuwa na viwanja viwili vya ndege vya kimataifa.
 
..mkuu hoja yangu sio kuwa na International airport..hoja ni balozi kuhamia kama kuna International Airport...kwa dom hata kama kuna International Airport tatu hakuna International flights zitakazoenda..elewa kuwa na International Airport na kuwa International flights ni vitu viwili tofauti..unaweza kuwa na International Airport jina ila hakuna International flights hata moja inayoenda kama hiyo ya songwe.!
 
Kwa nini hizo ndege zisiende ikizingatiwa kwamba ni jirani kwenda Ruaha National park kutokea Msalato Intel Airport?

Kinachoubeba uwanja wa KIA ni Utalii labda na ukumbi wa AICC ,vivyo hivyo tunategemea na Ruaha, Udzungwana shughuli za Kilimo plus shughuli za Kiserikali Kuubeba uwanja wa Ndege wa Dom.

Abuja ni uwanja wa 3 Kwa Ukubwa na wingi wa Abiria Nigeria kwani Kuna nini ambacho Watu wanafuata?
 
Mkishavuta bangi zenu mnabaki kuropokwa tu
Tunawakumbusha watu wa Arusha na Mwanza,Kwa Mara nyingine Dodoma imewapiga bao kwenye FDI kwa mwezi August.Zaifi ya bil.100 zinaensa kuwekezwa.

Nawakumbusha pia Toka January hakuna mwezi imepita bila kuripoti private investments so wale wa hadithi za Sijui Ni miradi ya Serikali Waanze kujiandaa kisaikolojia
 
Ndani ya miezi miwili mwanza imerekodi miradi 11 ..dodoma 6 Arusha 3 [emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]
 
Leta na takwimu za July
 
Ndani ya miezi miwili mwanza imerekodi miradi 11 ..dodoma 6 Arusha 3 [emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]
Kinacho mata ni value si ajabu Kagera itawapita kiuchumi hivi hivi mnaona.

Wewe endelea kushangilia namba ya miradi.
 
Kwan hyo miradi ni ya FDI tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…