Dodoma: Harambee iliyoendeshwa na Dkt. Magufuli yapelekea ukamilishwaji wa msikiti mkubwa

Dodoma: Harambee iliyoendeshwa na Dkt. Magufuli yapelekea ukamilishwaji wa msikiti mkubwa

مَا كَانَ لِلۡمُشۡرِكِينَ أَن يَعۡمُرُواْ مَسَٰجِدَ ٱللَّهِ شَٰهِدِينَ عَلَىٰٓ أَنفُسِهِم بِٱلۡكُفۡرِۚ أُوْلَٰٓئِكَ حَبِطَتۡ أَعۡمَٰلُهُمۡ وَفِي ٱلنَّارِ هُمۡ خَٰلِدُونَ
 
Ujenzi wa Msikiti wa Chamwino Mkoani Dodoma ambao Rais Magufuli aliahidi atashirikiana na Wananchi wengine kuujenga na akaanza kwa kuendesha harambee ya ujenzi wake akiwa Kanisani Chamwino, hatimaye umekamilika.

Itakumbukwa Jumapili ya August 23,2020 JPM alihudhuria Misa Takatifu na uzinduzi wa Kanisa Katoliki, Parokia ya Bikira Maria Imakulata,Ikulu Chamwino, Dodoma, ambapo alisema Waislamu pia walichangia ujenzi wa Kanisa hilo na kuwataka na Wakristo kuungana na Waislamu kuchangia ujenzi wa Msikiti Chamwino kupitia harambee aliyoiendesha Kanisani hapo.

JPM alisema "Kwenye michango tuliyochangisha hapa Kanisani kwa ajili ya ujenzi wa Msikiti Chamwino, tumepata jumla ya Tsh.Milioni 48 na Eflu 21, mifuko 48 ya cement na Lori 5 za mchanga, Rostam amechangia Mil 20, Bosa wa CRDB Nsekela Mil 10, pia CAG Kachere, Anthony Mavunde, RC Dodoma ni miongoni mwa waliochangia, sasa Msikiti utajengwa, Mimi nina Wasaidizi wangu wengine Waislamu yupo hai El Haji, wataswali kwenye Msikiti huo"

Twende na JPM 2020-2025

View attachment 1609855
View attachment 1609931
View attachment 1609932View attachment 1609933
President Magufuli Man of action & Man of the people
 
JPM is one of the kind, the president is delivering whatever he touches, Tanzanians should not allow anybody to create an atmosphere of change before he completes his mission. Viva JPM Hapa Kazi tu.
 
Shekhe Ponda Issa Ponda amesema Waisilamu wasihongwe Misikiti wakati Viongozi wao wakinyea debe na kuteswa ameyasema hayo Leo Tandahimba.
Wewe ndugu yangu kwa nini unatwambia mawazo ya huyo mtu mmoja. Bora ungetoa tu maoni yako wewe. Huyo unayemtaja siyo msemaji wa watanzania na hakuna sababu ya kujulisha umma alichokisema
 
Upo msikiti unaitwa msikiti wa Chamwino, picha zake zimesambaa kwa kasi zikieleza ulitokana na harambee.

Kwa mwonekano, ni msikiti mdogo kuliko msikiti wa Ghadafi uliopo Dodoma. Lakini pia tunayo misikini na nyumba nyingi za ibada ambazo kusambaza picha zake kwa baadhi inaweza kuwa faraja lakini kwa wengine yaweza kuwa kama masimango kwa sababu wanaosambaza siyo watumiaji na yawezekana ukakabidhiwa kwa wahusika.

Je, tunataka kuwaambia nini waumini kwa picha hizi?
 
Wamebanwa Mbavu, Huko Kigoma Zitto Kabwe ameshtukia mpango mkubwa wa kubambika na kuchakata Kura.

CCM kwa kushirikiana na Tume ya Uchaguzi wameandaa Vijana wa JKT waemde kubambika Kura Kigoma Mjini ma Wilaya zake.

Zitto Kabwe amewaapisha Vijana wa ACT Wazalendo na wa Chadema kuwa kuanzia Usiku waLeo watafanya Doria ili kiwabaini Wezi hao wa Kura na Vipigo vya haja kutolewa kadri iwezekanavyo.
 
Masheikh Ubwabwa wa CCM wazidi kuungana na kumhasidi Sheikh wa Umma Sheikh Ponda Issa Ponda.


Hawa viumbe wa Bakwata wanatia Aibu hilo shehe moja lilikuwa na video zake za vichekesho lakini sasa watu wamelichukia mbaya mpaka hawataki kuona video zake
 
Wamebanwa Mbavu, Huko Kigoma Zitto Kabwe ameshtukia mpango mkubwa wa kubambika na kuchakata Kura.

CCM kwa kushirikiana na Tume ya Uchaguzi wameandaa Vijana wa JKT waemde kubambika Kura Kigoma Mjini ma Wilaya zake.

Zitto Kabwe amewaapisha Vijana wa ACT Wazalendo na wa Chadema kuwa kuanzia Usiku waLeo watafanya Doria ili kiwabaini Wezi hao wa Kura na Vipigo vya haja kutolewa kadri iwezekanavyo.
Siku ya kufa nyani kila mti huteleza..

Bahati nzuri kila wanachopanga sirini kwa sasa kinavuja hadharani mchana kweupe, maana hata wao wenyewe wamechoshwa.

Wakubali kupumzika tu kwa amani
 
Dearesalaama kazi kwenu sisi tumeshamaliza.
 
Mbona Shehe Katimba hawakumuandama? Sasa hivi wanaleta question mark wanapomuandama Ponda.
 
Back
Top Bottom