ubarinolutu
JF-Expert Member
- Oct 22, 2012
- 2,424
- 4,954
RAIN BOW GRILL PUB HAPO NDO HUB YA BIASHARA YA DAWA ZA KULEVYA DODOMA, SISEMI KWAMBA MMILIKI NDO MUUZAJI HAPANA, HAPO NI TRADE CENTRE TU
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mzee,We utakuwa unatumia Skanka sio bure,kwani teja kumfahamu ndio ishara kwamba ni mdogo?OK tufanye ni mdogo kweli huoni kwamba kumkamata yeye ndio wanaelekea tuwakamata wakubwa kupitia yeye?Mtu unaambiwa ni Kinara wa dawa za kulevya jijini Dodoma bado unasema mdogo?ana athiri watu wangapi hapo kwenye jamii?
Safi mkuu, ila najiuliza hii biashara madawa ya kulevya Yana uhusiano gani dini ya Imani Fulani! Kila siku wao Tu!View attachment 3150376
MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imemkamata kinara wa dawa za kulevya jijini Dodoma, Suleiman Mbaruku Suleiman maarufu Nyanda mwenye umri wa miaka 52 ambaye mamlaka hiyo ilikuwa inamfuatilia kwa karibu kwa muda mrefu.
Nyanda alikuwa na mwenzake Kimwaga Msobi Lazaro mwenye umri wa miaka 37 ambapo hatua za kisheria dhidi yao zinaendelea.
Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Aretas Lyimo ameyasema hayo leo Novemba 12,2024 ofisini kwake jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari.
"Huyu Nyanda ni maarufu sana katika lile Jiji la Dodoma na waraibu ambao tunawatibu katika kituo pale Dodoma wengi wameharibiwa na huyu Nyanda.
"Mtuhumiwa Nyanda ni kinara wa biashara ya kulevya mkoani Dodoma ambaye tulikuwa tunamfuatilia kwa muda mrefu hadi tumemkamata.
Amesema wakazi hao wa Mtaa wa Kinyali uliopo Kata ya Viwanjani jijini humo walikutwa wakiwa na jumla ya gramu 392 za dawa za kulevya aina ya Heroin.
Wakati huo huo amesema, Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imefanya operesheni katika maeneo mbalimbali nchini kati ya Oktoba na Novemba 2024 na kufanikiwa kukamata kilogramu 1,066.105 za dawa za kulevya.
Sambamba na mililita 447 za dawa tiba zenye asili ya kulevya huku watuhumiwa 58 wakikamatwa katika operesheni hizo.
Kamishna Jenerali Lyimo amesema, kati ya dawa hizo kilogramu 687.32 za skanka na kilogramu moja ya hashishi zilikamatwa eneo la Goba jijini Dar es Salaam zikiwa zimefichwa ndani ya nyumba ya mtuhumiwa.
“Skanka ni aina ya bangi yenye kiwango kikubwa cha sumu, inavyosababisha madhara kiafya, vile vile hashishi ambayo hutengenezwa kwa mchanganyiko wa maua na mafuta ya mbegu za bangi, inapovutwa huzalisha kemikali hatari zinazoweza kusababisha magonjwa ya akili kwa haraka na mara nyingi jamii huamini kuwa watu wanaopatwa na magonjwa haya wamelogwa."
Amesema, katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, mamlaka ilikamata mililita 120 za dawa tiba zenye asili ya kulevya aina ya Codein zikiwa zinasafirishwa kwenda nje ya nchi, pamoja na mililita 327 zilizokutwa nyumbani kwa mtuhumiwa eneo la Tabata Kinyerezi.
Kamishna Jenerali Lyimo amesema,dawa hizo ziliingizwa nchini kinyume na taratibu zikiwa zimewekwa chapa bandia ya dawa za kuogeshea mbwa na paka ili kuepuka kubainika.
“Kukamatwa kwa dawa hizi ni ishara ya uwepo wa tatizo la matumizi holela ya dawa za tiba zenye asili ya kulevya, hali hii inachangiwa na kuimarika kwa udhibiti wa dawa za kulevya na kusababisha wafanyabiashara na watumiaji kutumia dawa tiba ya kulevya kama mbadala wa dawa za kulevya.”
Pia,amesema kumekuwa na ongezeko la watumiaji wakubwa wa dawa za kulevya aina ya skanka ikiwa wanaoongoza ni wanawake, huku sababu ya ongezeko hilo ikitajwa kuwa ni kupambana na msongo wa mawazo ambao umekuwa ukiwasumbua hasa ukitokana na udanganyifu wanaokutana nao kwenye uhusiano wa kimapenzi.
Pia, amesema licha ya mbinu nyingi kutumiwa na wafanyabiashara wa dawa za kulevya ili kuingiza dawa za kulevya nchini ikiwemo kutoa rushwa, mamlaka imejipanga kuhakikisha kila mbinu inadhibitiwa.
Amesema, mamlaka imekuja na mkakati kabambe wa kuhakikisha mizigo yote inayoingia nchini kupitia mipakani inakaguliwa kwa kutumia scanner maalum na pale ambapo kuna mizigo itapita ikiwa na dawa za kulevya, Afisa aliyehusika na ukaguzi atawajibishwa mara moja.
Huyu mangi Yuko makini sana ila nchi hii ilivyo hovyo atatengenezewa mizengwe!!!Kazi nzuri kamishna
Hakuna kazi yoyote wanayoifanya zaidi ya sanaa.Laiti mngejua, jamaa wanafanya kazi haswa
Hata mie nataka nimwone......ila kwa jina na umri nikihusisha na hiyo aka Nyanda kama namfahamu ila sina uhakika maana niliishi Dom kitambo sanaMwenye picha ya Nyanda tafadhali...
Na wanapiga fedha hawa jamaa kupitia matatizo ya waraibu ya madawa ya kulevya, sema tu watu hawajui nyuma ya paziaHakuna kazi yoyote wanayoifanya zaidi ya sanaa.
Wakati huo huo amesema, Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imefanya operesheni katika maeneo mbalimbali nchini kati ya Oktoba na Novemba 2024 na kufanikiwa kukamata kilogramu 1,066.105 za dawa za kulevya.UJINGA MTUPU..Bado mnakamata dagaa yaani kama huyo jamaa anajulikana na mateja basi ni wa kawaida sana. Mapapa wa hii biashara hawajulikani na mateja wao ndio wanaingiza nchini kwa kushirikiana na wanasisasa wakubwa pamoja na watendaji wakuu wa vyombo vyetu vya ulinzi hususan polisi na tiss
Muislam mwenzetu huyo aachiweHuyo afinywe tu.
Muislam siyo Uislam.Muislam mwenzetu huyo aachiwe
Upo sahihi kabisaUJINGA MTUPU..Bado mnakamata dagaa yaani kama huyo jamaa anajulikana na mateja basi ni wa kawaida sana. Mapapa wa hii biashara hawajulikani na mateja wao ndio wanaingiza nchini kwa kushirikiana na wanasisasa wakubwa pamoja na watendaji wakuu wa vyombo vyetu vya ulinzi hususan polisi na tiss
Sure Kamishna anajitahidi sana ..KONGOLE kwakeKazi nzuri kamishna
Tatizo watu wanataka watu wakamatwe kwa mihemkoLaiti mngejua, jamaa wanafanya kazi haswa
Siku akikanyaga nyaya za Ridhwan mtamwimbia nyimbo ya parapanda.Huyu mangi Yuko makini sana ila nchi hii ilivyo hovyo atatengenezewa mizengwe!!!
waanze kumkamata Siro yeye ndie kinara wa hizo kituWe utakuwa unatumia Skanka sio bure,kwani teja kumfahamu ndio ishara kwamba ni mdogo?OK tufanye ni mdogo kweli huoni kwamba kumkamata yeye ndio wanaelekea tuwakamata wakubwa kupitia yeye?Mtu unaambiwa ni Kinara wa dawa za kulevya jijini Dodoma bado unasema mdogo?ana athiri watu wangapi hapo kwenye jamii?
Yule aliepewa ubalozi au?waanze kumkamata Siro yeye ndie kinara wa hizo kitu
🤣😂🤣😂😂🤣Classmate wako umemsahau au kisa kadakwa na skanka ??