Dodoma: Hofu yatanda Nzuguni baada ya kundi la ‘Teleza’ kuwavamia Wanawake Usiku na kuwabaka

Dodoma: Hofu yatanda Nzuguni baada ya kundi la ‘Teleza’ kuwavamia Wanawake Usiku na kuwabaka

Mafyangula

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2025
Posts
557
Reaction score
1,039
Huko Arusha miaka kadhaa nyumba iliyopita alikuwa jamaa anaitwa teleza naye alikuwa na michezo hii. Baada akapotoa

Haya huko Dodoma wamejitokeza wengine, hii sasa ni balaa tu
========================

Wakazi wa Mtaa wa Nzuguni B, Kata ya Nzuguni, Jijini Dodoma wameingia katika hofu kubwa kufuatia kuibuka kwa kundi la vijana wanaojiita Teleza, wanaotuhumiwa kuvamia nyumba usiku kwa imani za kishirikina na kuwabaka wanawake.

Ni tukio linaloonekana kama sinema ya kutisha, lakini kwa wakazi wa Nzuguni B, ni hali halisi. Usiku wa Septemba 3, mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 20 (jina limehifadhiwa) alikumbwa na tukio hilo la kikatili, akisimulia kwa uchungu jinsi alivyoangukia mikononi mwa mmoja wa vijana wa kundi hilo.

“Nilistukia yupo kitandani… nilikuwa najigeuza kumwangalia mwanangu, nikashtuka kuona mtu amenishikia kisu. Akanambia nisipotulia atamuua mwanangu. Nilikuwa mwenyewe tu, sikuwa na jinsi,” ameeleza kwa sauti ya huzuni.

Kwa maelezo yake, kijana huyo aliingia akiwa na tochi yenye mwanga mkali na kisu, kisha kumtisha kwa kumuwekea mwanawe kisu shingoni kabla ya kutekeleza unyama huo.

Kwa sasa, taharuki imetanda mtaani huku wakazi wengi wakilazimika kulala kwa makundi kwa hofu ya kuvamiwa.
 
Huu mzigo wa malawama wote tuwatwike ccm, hao wasiojulikana wamewapa vijana code ya kutokujulikana mshahara wenyewe ndo huu sasa.
 
Back
Top Bottom