Dodoma: Jeshi la Polisi lamuita Cyprian Musiba kwa mahojiano kuhusu tuhuma za kutaka kuuawa

Dodoma: Jeshi la Polisi lamuita Cyprian Musiba kwa mahojiano kuhusu tuhuma za kutaka kuuawa

Ameitwa aende kama mlalamijaji,na si wamemkamata,lakini wasitutoe kwenye msitari,Kabendela ameachiwa leo.
 
Wanampa tu airtime huyu mbwa....... Anyway mtetezi huyu wa raisi hawezi kukamatwa atakua ameitwa tu kunywa Chai maana hizi ni movie tu km ila ya Gaidi wa mapango ya amboni.....
 

Kamanda machachari was Polisi mkoa wa Dodoma maarufu kama 'mzee wa kuchakaza kama mbwa koko' amefunguka kuwa "kijana wao" Cyprian Musiba ametishiwa kuuawa kama ilivyoandikwa kwenye magazeti yake ya Tanzanite kuwa Zitto Kabwe kaleta Mjerumani amuue na polisi Mara moja wameamua kufuatilia kwa kina.

Dodoma hiyohiyo, miaka miwili iliyopita mbunge alishambuliwa kwa risasi zaidi ya magazine nzima mchana lakini polisi hawakuchunguza na hawatachunguza kamwe. Lakini "KIJANA WETU" kaja na story ya kusadikika tayari RPC kaingia kazini kumhami "kijana wetu".


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Eti "kijana wao", kumbe kweli huwa wanamtuma kwa zile shughuli zao za kijinga kuchafua watu kwa tuhuma za uongo zisizo na kichwa wala miguu.

Kumbe Makamba, Membe na Kinana walikuwa sahihi kusema huyo mjinga anatumwa, ila hii aibu kuna siku wataibeba, what goes around always comes around.

At least for the time being, wacha washamba waendelee kufurahia ujinga wao kama watatawala milele.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu RPC namkubali sana. Yaani mlitaka hadi mtu awe maiti halafu mseme alikuwa anatania?? Huyo atakuwa sio Polisi.

Huwezi linganisha shambulizi la Lisu na mpango mkakati wa kutaka kumuua Musiba.
Lisu hakuwahi kujaribiwa kuuawa ila sasa kama angerudi nadhani ndiyo mngejua kuwa Tz kuna ulinzi imara. Mwambieni arudi tu. Musiba awekewe ulinzi 24/7/52. Hatutaki kumpoteza mtu hata mmoja tena
 
Huyu RPC namkubali sana. Yaani mlitaka hadi mtu awe maiti halafu mseme alikuwa anatania?? Huyo atakuwa sio Polisi. Huwezi linganisha shambulizi la Lisu na mpango mkakati wa kutaka kumuua Musiba.
Lisu hakuwahi kujaribiwa kuuawa ila sasa kama angerudi nadhani ndiyo mngejua kuwa Tz kuna ulinzi imara. Mwambieni arudi tu. Musiba awekewe ulinzi 24/7/52. Hatutaki kumpoteza mtu hata mmoja tena

Unahitaji kula virutubisho kichwa kiko empty
 
Hii inaitwa Mike Pompeo effect! Hspohapo mara Kibendera ameachiwa baada ya kukiri makosa.

Wahakikishe director wa hii movie amehitimu masomo vizuri isiwe kama zile series zilizopita.
Isije ikawa kama ile picha iliyo dairektiwa na mambo ya kileo
 

Pamoja na mambo mengine
Musiba,amewataja viongozi kadhaa kuhusika na mpango huo wa mauwaji dhidi yake akiwemo Zito Kabwe, Januari Makamba pia mpango huo unahusisha professional assassin mdungiaji wa kimataifa kutoka ujerumani ambae tayari ameshawasili hapa nchini, pia amezihusisha nchi za magharibi kuhusika na mpango huo wa mauaji.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyo ni potential candidate. Ni kijana wao hawawezi kumuumiza.
 
Back
Top Bottom