Sheria zingine za ajabu sana.
Kuna mambo yanaendeshwa kisiasa, sheria hii walitunga wabunge wanao jiita wawakilishi wa watu.
Mtu anatangaza anatafutwa kuuwawa na wenye dhamana ya kukulinda wanakukamata kwanini umetangaza na kufichua mpango ovu dhidi yako.
Najua kuna watu watashangilia badala ya kuilaani na kuomba ifutwe hii sheria, watashangilia sababu imemdhuru Musiba ila ikiwakuta wao au wanao wapenda utasikia kelele nyingi na malalamiko.
Jambo hili litatokea tena kwa mtu mwingine karibuni tusirudi kupiga kelele.