Pre GE2025 Dodoma: Jeshi La Polisi lapigwa msasa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi kuhusu namna bora ya kuendesha Uchaguzi Mkuu 2025

Pre GE2025 Dodoma: Jeshi La Polisi lapigwa msasa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi kuhusu namna bora ya kuendesha Uchaguzi Mkuu 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Maafisa wa Polisi nchini wametakiwa kuimarisha uelewa wao kuhusu sheria zinazohusiana na uchaguzi ili kuepuka ushawishi wa kisiasa wa wanasiasa wanaojaribu kupotosha sheria hizo kwa maslahi yao.

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Kailima Ramadhani, alitoa wito huu wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya Wakuu wa Upelelezi wa Wilaya yaliyofanyika Oktoba 17, 2024, mkoani Dodoma.

Kailima alisisitiza umuhimu wa mafunzo haya katika kipindi hiki ambapo kuna Sheria Mpya mbili zinazosimamia masuala ya uchaguzi, ambazo ni Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani Na. 1 ya mwaka 2024, pamoja na Sheria ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Na. 2 ya mwaka 2024.

Tume ya uchaguzi.png

Kailima alisema kuwa, mafunzo haya yatasaidia Wakuu wa Upelelezi kuwa mabalozi wa kuhamasisha wananchi kujiandikisha na kuboresha taarifa zao katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.

Soma pia: Tume Huru ya Uchaguzi yakamilisha mchakato wa kutoa elimu kwa wananchi Zanzibar. Mchakato wa uandikishaji umeanza rasmi leo!

Aidha, washiriki walijifunza wajibu wa Jeshi la Polisi wakati wa uchaguzi, utambuzi wa bidhaa bandia, pamoja na masuala mengine muhimu yanayohusiana na mchakato wa uchaguzi. Lengo la mafunzo ni kuwajengea uelewa wa haki za vyama, wananchi, na makundi mengine katika kipindi chote cha uchaguzi.

PIA SOMA
- Kuelekea 2025 - INEC watoa elimu kwa Wakuu wa Polisi wa Wilaya (OCD) ili kuliweka tayari Jeshi la Polisi wakati wa mchakato wa Uchaguzi

Source: Tovuti ya INEC
 
Msasa uanzie kwa aina ya vijana wanaochukuliwa kusoma upolisi, sio form four failure!
 
Back
Top Bottom