Ile penalti waliyopata Simba kule Dodoma haikuwa halali, lakini mwamuzi aliwapa faida kwa kuwapa pointi 3. Timu ya Dodoma ililalamika, na kocha wao, Mexime, alionyesha kutoridhika. Lakini msemaji wa klabu aliwaambia waende TFF kama wana malalamiko zaidi!
Mechi dhidi ya Azam kule Zanzibar nayo haikuwa na amani. Kulikuwa na malalamiko mengi kuhusu magoli yaliyofungwa yakiwa offside, jambo ambalo lilimkasirisha sana kocha wa Azam. Hata hivyo, mashabiki na wanachama wa Simba walitetea matokeo hayo wakisema "hii ndiyo maana ya ubaya ubwela!"
Leo hii, mashabiki hao hao ambao hawana msimamo thabiti wanamlalamikia mwamuzi Kayoko. Wamesahau jinsi walivyodhulumu wenzao kwa msaada wa marefa. Hii ni sawa na utahira wa kiwango cha SGR! Kila mmoja anajua msemo, "ukiua kwa upanga, na wewe utakufa kwa upanga." Kama mwamuzi wa Dodoma alifanya makosa ya kibinadamu, basi hata Kayoko ametenda vile vile—ni makosa ya kibinadamu.
Haiwezekani mwamuzi akifanya makosa yanayokufaidi wewe, unafurahia na kusema amepitiwa tu. Lakini akifanya makosa kwa mwenzako, unaanza kutoa malalamiko ya kila aina. Hiyo si sawa hata kidogo! Neno "ubaya ubwela" litawarudia wenyewe maana sasa imejulikana wazi ni nini kinachomaanishwa. Ubaya na upendeleo kwa njia yoyote ile, ya halali au ya ovyo, ni mambo yanayojulikana kwa mashabiki hao. Lakini mwisho wa siku, tutafika mahali ambapo "ubaya ubwege" utawachoma wenyewe.
Wakati wenzako wanapolianzisha, wanajua pia jinsi ya kulimaliza. Hapo tutabaki tukiangalia nani atakuwa bingwa mwishoni mwa msimu.