KERO Dodoma Jiji- tatizo la maji taka yanayotirika waziwazi lipatiwe ufumbuzi

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

N'yadikwa

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2014
Posts
8,308
Reaction score
12,812
Wakazi na wadau wa Jiji la Dodoma, kuna jambo ambalo kwa kweli linahitaji majibu na hatua za haraka kutoka kwa mamlaka husika.

Ukipita maeneo mbalimbali ya Jiji la Dodoma, ikiwemo NSSF, Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT), mfereji wa eneo la Soko la SabaSaba karibu na Nabaki Africa, Chako ni Chako, pamoja na maeneo mengine, utakutana na mifereji ambayo maji taka yanatiririka waziwazi.

Hali hii inazua maswali kadhaa:
  1. Mfumo wa majitaka wa Jiji unafanya kazi ipasavyo?
  2. Mamlaka inayohusika na huduma za majitaka inafuatilia kutatua hali hii?
  3. Maafisa afya wa Jiji wanafanya ukaguzi wa maeneo haya mara kwa mara?
  4. Ni hatua gani zinazochukuliwa dhidi ya vyanzo vinavyosababisha maji taka kutiririka kwenye maeneo ya wazi?
  5. Je, kuna mpango maalum wa kutatua tatizo hili kwa kudumu, badala ya kushughulikia malalamiko kila yanapotokea?
Hili si suala la harufu mbaya pekee. Maji taka yanayotiririka wazi yanaweza kuathiri usafi wa mazingira, ubora wa maisha ya wananchi na usalama wa maeneo yanayozunguka.

Jiji la Dodoma ni makao makuu ya nchi na linaendelea kukua kwa kasi. Miundombinu ya majitaka inapaswa kwenda sambamba na ukuaji huo.

Wito wangu kwa Dodoma City Council, mamlaka inayosimamia huduma za majitaka na maafisa afya:

👉 Fanyeni ukaguzi wa maeneo haya.
👉 Tambueni chanzo cha tatizo.
👉 Chukueni hatua kwa maeneo yanayokiuka taratibu.
👉 Toeni taarifa kwa wananchi kuhusu mpango wa kutatua tatizo hili kwa kudumu.

Wananchi wana haki ya kuuliza: Je, mifereji hii inajulikana na mamlaka? Kama inajulikana, kwa nini imeachwa maji taka yatiririke waziwazi kwa muda mrefu?

Eneo jingine ni pale kwenye mahoteli jirani na City Boys Lodge mkabala na airport.

Majitaka kutiririka hovyo ni kero kubwa sana.

Picha: mfereji wa majitaka chuo kikuu huria pale.

921781.jpg
 
Attachments

  • 921781.jpg
    921781.jpg
    669.9 KB · Views: 8

View attachment 3672474
Mitaa inatoa harufu
 
Back
Top Bottom