Dodoma Jiji wamefika Itumbi - Mtaa wa Nghonghona, Dodoma kutatua kero za migogoro ya ardhi

Dodoma Jiji wamefika Itumbi - Mtaa wa Nghonghona, Dodoma kutatua kero za migogoro ya ardhi

A

Anonymous

Guest


Kwanza nianze kwa kusema asante sana JamiiForums kwa kufikisha ujumbe wetu kwa umma na hatimaye kufika kwa mabosi wa juu, kwani muda mfupi baada ya taarifa hiyo kuhusu changamoto ya ardhi kwa Wakazi wa eneo la Itumbi, Mtaa wa Nghonghona jijini Dodoma, wahusika wamefika na hatua zimeanza kuchukuliwa.

Maafisa wa Jiji walifika kuanzia Ijumaa iliyopita (Agosti 7, 2026) na kuanza kuchukua hatua ya kutatia changamoto tulizolalamikia kuhusu mipaka.

Hoja ya awali ~ Serikali itusaidie Wakazi wa Itumbi - Mtaa wa Nghonghona Dodoma maeneo yetu yanachukuliwa kimabavu

Wamesema wataendelea kuwepo hapo kwetu kwa siku saba ukiondoa siku za wikiendi, kutatua changamoto zilizopo zikiwemo za mipaka na maeneo mengine kuchukuliwa kinyume na utararibu.

Tunapongeza pia uongozi wa Dodoma Jiji kwa kufika na kuanza kushughulikia kwa kuwa changamoto ya kwetu hapa imekuwepo tangu Mwaka 2020.

Wito wetu ni kuwa kama inawezekana waongezea siku za kuwepo hapa au waongeze Maafisa kwa kuwa watu tupo wengi na migogoro ni mingi, kwani wapo ambao masuala yao yanashughulikiwa ofisini na wengine yanashughulikiwa site.
 
Back
Top Bottom