Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Ufafanuzi kuhusu changamoto ya Majisafi Kisasa - Dodoma
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) inakiri na kutambua changamoto iliyopo ya hali ya upatikanaji wa huduma ya majisafi katika baadhi ya maeneo ya Kisasa kutokana na kupungua kwa uzalishaji katika baadhi ya vyanzo vinavyopeleka maji katika maeneo hayo.
Upungufu huo wa maji umesababisha maeneo ya Kisasa Bwawani, Kisasa East karibu na relini, Nyumba 300 kuanzia msikitini na Mwangaza kukosa huduma ya maji, huku Mamlaka ikichukua jitihada za dharura za muda mfupi kutatua changamoto hiyo.
Mhandisi Bernard Rugayi ni Mkurugenzi wa Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira ambaye amewahakikishia wananchi na wateja wa Kisasa kuwa wavumilivu kwa kuwa tayari DUWASA imefanya utafiti wa eneo la kuchimba kisima kirefu kitakachohudumia maeneo hayo ili kuboresha hali ya huduma ya maji.
Kazi ya uchimbaji wa kisima eneo la Kisasa utaanza siku ya Jumatatu Oktoba 07, 2024 na Mkandarasi ameshapatikana kwa ajili ya kuanza kazi.
Imetolewa na:
Rahel Muhando
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma - DUWASA
01.10.2024
Pia, soma;
KERO - Kero ya maji safi jijini Dodoma, Waziri Aweso ingilia kati