Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi CCM (NEC) kimefanyika leo tarehe 29 Aprili, 2021 katika Makao Makuu cha Chama, White House Jijini Dodoma.
Kikao hicho kimehudhuriwa na Mjumbe wa NEC Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar) Dkt. Ali Mohamed Shein pamoja na Makamu Mwenyekiti CCM Tanzania Bara Philip Mangula
View attachment 1767527
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM (Bara) Rodrick Mpogolo akizungumza katika .
View attachment 1767526
Mjumbe wa NEC Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa katika kikao hicho cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi CCM (NEC) kilichofanyika leo tarehe 29 Aprili, 2021 katika Makao Makuu cha Chama White House Jijini Dodoma.
View attachment 1767525
Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar) Dkt. Ali Mohamed Shein akiwa katika kikao hicho cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi CCM (NEC) kilichofanyika leo tarehe 29 Aprili, 2021 katika Makao Makuu cha Chama White House Jijini Dodoma.
View attachment 1767529
Wajumbe mbalimbali wa NEC wakiwa katika Kikao hicho cha NEC kilichofanyika leo tarehe 29 Aprili, 2021 katika Makao Makuu cha Chama White House Jijini Dodoma.
PICHA NA IKULU