Dodoma: Maadhimisho ya Mei Mosi, Waliofukuzwa kwa vyeti feki kulipwa, ahadi ya Nyongeza ya Mishahara yatolewa, Unyanyasaji kazini wakemewa

Dodoma: Maadhimisho ya Mei Mosi, Waliofukuzwa kwa vyeti feki kulipwa, ahadi ya Nyongeza ya Mishahara yatolewa, Unyanyasaji kazini wakemewa

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Tanzania inaungana na mataifa mengine katika kuazimisha siku hii ambayo itakuwa ni mara ya pili kwa Rais Samia Hassan kuwahutubia wafanyakazi baada ya kushika wadhifa huo.

Rais Samia atakuwa mgeni rasmi katika maadhimisho haya huku wafanyakazi akisubiri kwa hamu hotuba yake kutokana na ahadi aliyoitoa kwenye maadhimisho hayo mwaka jana Jijini Mwanza.

b2099e6d-988f-4e04-af38-89ffcf0e852c.jpg

Kilele cha Maadhimisho ya Sherehe ya Siku ya Wafanyakazi Duniani, Mei Mosi katika Uwanja wa Jamhuri Mkoani Dodoma.

Rais Samia Suluhu Hassan ameshawasili uwanjani na ratiba imeanza rasmi. Muda wowote kuanzia sasa waandamanaji wataanza kupita mbele ya Rais.

Wafanyakazi mbalimbali wameanza kupita mbele ya Rais katika mfumo wa maandamano wakiwa na mabango mbalimbali yenye ujumbe tofauti.

Maandamano ya wafanyakazi mbalimbali wa kampuni na taasisi mbalimbali wanaendelea kupita mbele ya Rais wakiwa na mabango yao, watu ni wengi uwanjani.

UJUMBE WA MISHAHARA YATAWALA
Ujumbe wa mishahara kwa wafanyakazi, maslahi bora na sensa ndivyo vimetawala katika mabango ya wafanyakazi katika kilele cha maadhimisho ya Sikukuu ya Wafanyakazi Dunia yanayofanyika katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

UTAMBULISHO
Viongozi wa dini wamekaribishwa kutoa neno na kuombea shughuli inayoendelea uwanjani hapa.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka anafanya utambulisho wa viongozi mbalimbali pamoja na taasisi na makampuni yaliyoshoriki kutoa mchango mkubwa wa kufanikiwa kwa shughuli hiyo.

Profesa Joyce Ndalichako ambaye ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na wenye Ulemavu anazungumza muda huu.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa anazungumza muda huu:
"Niwahakikishie wafanyakazi wote Nchini, Rais wetu anawajali sana, Nampongeza Rais wa Shirikisho la Wafanyakazi, nawapongeza wafanyakazi ambao wamejieleza wenyewe kwa mabango, sherehe ya mwaka 2022 imefana," - Kassim Majaliwa.

Muda huu wanatajwa wafanyakazi bora mbalimbali.

UJUMBE WA TUCTA
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), Hery Mkunda anasoma risala ya wafanyakazi.

"TUCTA tunakumbuka ahadi yako ya kuboresha maslahi ya wafanyakazi kwa mwaka huu. Tunapendekeza kiwango cha mfanyakazi kiwe angalau milioni 1.1 kwa mwezi.

"Hii ni kwa kuwa kiwango cha mshahara hakijapanda kwa muda mrefu, kuna mfumuko wa bei, gharama za maisha zimebadilika, tunaomba Serikali isikio kilio chetu.

"Tunaomba Serikali ielekeze taasisi zilizo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii kujiunga na vyama vya wafanyakazi tofauti na ilivyo sasa," - Henry Mkunda, Katibu wa TUCTA.
FRqZHDIWUAARHOQ.jpg
TUCTA WAPENDEKEZA MSHAHARA WA CHINI UWE TSH MILIONI 1
"Tunaomba Serikali iangalie wale wanaopewa ajira za muda mfupi, wanafanya hivyo hadi kwa miaka 10 wakipewa mikataba mifupi, Serikali iangalie na wapewe ajira za mkataba wa kudumu, mfano mmoja wapo ni TANESCO.

"Kima cha chini cha misharaha kimeendelea kuwa duni licha ya gharama za maisha kupanda, mathalani kwa sekta binafsi kwa watumishi wa majumbani ni Tsh. 40,000/- hadi Tsh. 60,000/-. Kwa wafanyakazi wa Umma kima cha chini ni Tsh. 315,000/-.

"Wafanyakazi hawajaongezwa mishahara kwa miaka 9 kwa Sekta Binafsi na miaka 7 kwa Sekta za Umma hali iliyosababisha kupungua hari ya kufanya kazi na kupunguza ufanisi mahali pa kazi.

"Tunapendekeza kiwango cha Tsh 1,010,000/= cha mshahara kiwe ndio kima cha chini kwa wafanyakazi," - Henry Mkunda, Katibu wa TUCTA.

RAIS ANAZUNGUMZA
Rais Samia ameanza kuzungumza, wafanyakazi wamemshangilia kwa nguvu baada ya kuanza kuzungumza.

“Nitoe salamu za pole kwa wafanyakazi na waajiri waliopoteza maisha tangu tilipokuwa pamoja Mei mwaka uliopita.

“Mafahari wawili wakipigana nyasi zinaumia, katika hili nyasi na wakubwa wote wameumia, hii imesababisha kupanda kwa gharama za maisha.

Wakati Rais Samia anazungumza adhana ikasikika atika msikiti uliopo jirani, amesimama kwa muda kupisha adhana kuendelea.

RAIS SAMIA AGUSIA UNYANYASAJI KAZINI, SHERIA HAITUMIKI VIZURI
Rais Samia Suluhu ameagiza Wizara ya Kazi na Kamisheni ya Kazi kufuatilia na kuchukua hatua unyanyasaji unaofanyika sehemu za kazi.

“Kumekuwa na malalamiko ya vitendo vya unyanyasaji na udhalilishaji, Sheria Tawala za Mikoa Namba 19 ya Mwaka 1997, imewapa mamlaka Mkuu wa Mkoa na Wilaya kumuweka mahabusu mtumishi yeyote wa umma anayefanya kosa la kuhatarisha usalama wake au wa umma.

“Kifungu hiki cha sheria kimekuwa kikitumika vibaya, mfanyakazi akisimama akazungumza ukweli anakumbana na kifungu hiki cha sheria,” Rais Samia.

SAMIA: NAKUBALI VIWANGO VYA MISHAHARA HAVIKIDHI MAHITAJI
“Ujumbe wa Wafanyakazi wa mwaka huu nimeuelewa vyema, kauli mbiu yenu ya “Mishahara na Maslahi Bora kwa Wafanyakazi Ndio Kilio Chetu na Kazi Iendelee”.

Kauli mbiu inabeba changamoto mbalimbali zinazowakabili wafanyakazi, nakubaliana na ninyi kuwa viwango vya mishahara vya sasa havikidhi mahitaji hususani nyakati kama hizi ambapo gharama za maisha zimepanda,” - Rais Samia katika Maadhimisho ya Mei Mosi, Dodoma.

SAMIA: STAHIKI ZA MTUMISHI ZIANDALIWE MIEZI 6 KABLA YA KUSTAAFU
Rais Samia Suluhu ameagiza waajiri kuandaa malipo ya wastaafu miezi sita kabla ya muda wa kustaafu kwa kuwa huwa inajulikana, hiyo ni baada ya kukiri kupokea malalamiko ya malipo ya mafao na nauli kwa wastaafu.

“Kabla ya mtumishi kuondoka ofisini awe ameandaliwa stahiki zake zote na mafao yake yote kwa kuwa inajulikana na mtumishi anatoa taarifa.

“Mifuko ya hifadhi nayo ifanye uhakiki ndani ya miezi sita ili mstaafu ikifika muda wa kuondoka apate stahiki zake kwa wakati,” - Rais Samia.

============================

SIKU YA WAFANYAKAZI DUNIANI ILIVYOANZA

Sikukuu ya Wafanyakazi duniani ni kumbukumbu ya mauaji ya halaiki ya mwaka 1886 yaliyotokea katika Viwanja vya Haymarket, Chicago Nchini Marekani.

Askari Polisi walikuwa wakitawanya mkusanyiko wa wafanyakazi wakati wa mgomo wa kupinga saa nane za kazi, mtu asiyejulikana alirusha bomu lililoua na kujeruhi askari kadhaa, nao walirejesha shambulizi kwa kurusha risasi kwa Wafanyakazi na kuwaua wanne.

Siku hii huwa ni Sikukuu katika nchi nyingi duniani maalum kwa ajili ya Wafanyakazi.
 
kilio kikubwa cha watumishi ni mishahara,
lkn nadhani kuna watumishi wanalipwa mamilioni, sasa kweli hao wanapaswa kuongezwa?! sidhani.
wanao paswa ni wale wa kima cha kawaida/chini. ili angalau na wao wainuke
 
Kilele cha Maadhimisho ya Sherehe ya Siku ya Wafanyakazi Duniani, Mei Mosi katika Uwanja wa Jamhuri Mkoani Dodoma.

Rais Samia Suluhu Hassan ameshawasili uwanjani na ratiba imeanza rasmi. Muda wowote kuanzia sasa waandamanaji wataanza kupita mbele ya Rais.

Wafanyakazi mbalimbali wameanza kupita mbele ya Rais katika mfumo wa maandamano wakiwa na mabango mbalimbali yenye ujumbe tofauti.

============================

SIKU YA WAFANYAKAZI DUNIANI ILIVYOANZA

Sikukuu ya Wafanyakazi duniani ni kumbukumbu ya mauaji ya halaiki ya mwaka 1886 yaliyotokea katika Viwanja vya Haymarket, Chicago Nchini Marekani.

Askari Polisi walikuwa wakitawanya mkusanyiko wa wafanyakazi wakati wa mgomo wa kupinga saa nane za kazi, mtu asiyejulikana alirusha bomu lililoua na kujeruhi askari kadhaa, nao walirejesha shambulizi kwa kurusha risasi kwa Wafanyakazi na kuwaua wanne.

Siku hii huwa ni Sikukuu katika nchi nyingi duniani maalum kwa ajili ya Wafanyakazi.
Thanks for this.
P
 
Mishahara inazingatia kiwango cha elimu na umri kazini. Haiwezekani darasa la saba akafanana na degree holder labda kwa wabunge.

Akipandisha wote watapandishwa
 
Mwenye link ya YouTube aiweke chaap

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kilio kikubwa cha watumishi ni mishahara,
lkn nadhani kuna watumishi wanalipwa mamilioni, sasa kweli hao wanapaswa kuongezwa?! sidhani.
wanao paswa ni wale wa kima cha kawaida/chini. ili angalau na wao wainuke
Lakini Kuna wakati SERIKALI ilituaminisha kuwa hakuna senior service man/woman atakayelipwa zaidi ya 15m. Binafsi nashangaa kusikia haya Tena.
 
Mishahara inazingatia kiwango cha elimu na umri kazini. Haiwezekani darasa la saba akafanana na degree holder labda kwa wabunge.

Akipandisha wote watapandishwa
Dah....hapa ndiyo sielewagi....na sitokaa nielewe kamwe 🤣🤣🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom