Dodoma: Mabasi yapigwa marufuku kuruhusu abiria kujisaidia ovyo

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Halmashauri ya Jiji la Dodoma imepiga marufuku mabasi ya abiria kuruhusu abiria kuchimba dawa (kujisaidia) kwenye maeneo yasiyo rasmi, na kwamba endapo wakibainika watapigwa faini ya Sh. 200,000 au kifungo cha miezi sita jela.

Sambamba na hilo, imeagiza mabasi hayo kupuliziwa dawa za kuua wadudu ikiwamo kunguni ndani ya siku saba kwa kuwa wamekuwa wakiwadhuru abiria.

Kauli hiyo ilitolewa juzi na Ofisa Afya wa Jiji la Dodoma, Abdallah Mahiya, katika ukaguzi wa mabasi yaendayo mikoani pamoja na usafi wa maeneo ya mama ntilie kwenye kituo cha mabasi cha Nanenane.

Alisema kumekuwa na tabia ya mabasi kusimama ovyo na abiria wakijisaidia kwenye maeneo yasiyo rasmi hali inayochangia uchafu wa mazingira.

"Kwa mujibu wa sheria ni marufuku kwa mtu yeyote abiria au mmiliki wa gari kujisaidia sehemu isiyo rasmi na faini yake ni Sh. 200,000 au kifungu cha miezi sita jela au vyote kwa pamoja,” alisema.

Mahiya aliwataka wananchi kuhakikisha hakuna basi linalosimama maeneo ambayo hakuna vyoo kwa kuwa ni jambo la hatari kwa wakazi wa maeneo hayo kwa watu kujisaidia ovyo.

"Basi linasimama maeneo ya watu au kwenye shule watu wanajisaidia halafu watoto wanaosoma pale wakiwa wanafanya usafi wanashika vinyesi vyao jambo ambalo ni hatari kwa afya," alisema.

Aidha, alisema katika ukaguzi huo wamebaini mabasi kuwa na wadudu dhurifu kama vile kunguni, mende na kuwataka ifikapo Januari 24, mwaka huu yawe yamepulizwa dawa za kuua wadudu hao.

"Tumefanya ukaguzi kwa mabasi zaidi ya 20 hadi sasa tumebaini mengi hayapuliziwi dawa za kuua wadudu, vizima moto vingi havitumiki kuna nyingine hazina vizima moto baadhi vimekaa kama maonyesho, pia visanduku vya kuhifadhia dawa za huduma ya kwanza hakuna vingine vina upungufu havina dawa,” alisema.

Aliagiza kila basi kuhakikisha lina kisanduku cha huduma ya kwanza na dawa zinazotakiwa.

"Si kuwa tupu waweke wembe maalum za upasuaji si kuwa na wembe wa kawaida, vitunza taka viwapo na vitumike si kuwekwa kama urembo na madereva waache tabia ya kutupa taka ovyo njiani," alisema.

Kuhusu usafi maeneo ya vyakula, alieleza kuwa wafanyabiashara wengi wanazijua sheria, lakini wanazipuuza kwa kutovaa sare wakati wa kuhudumia wateja na kutozingatia kanuni za usafi.

Chanzo: IPP Media
 
U

Vipi wanaochfua hali ya hewa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom