Pre GE2025 Dodoma: Machinga kusherekea siku ya kuzaliwa Rais Samia kwa kutoa punguzo la 30% kwa bidhaa zote

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Wakuu,

Kunaanza kunoga hukoπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚.

=====

Your browser is not able to display this video.

Wamachinga wa Soko la Wazi la Machinga Complex, jijini Dodoma, wameandaa sherehe ya kipekee kuadhimisha siku ya kuzaliwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, itakayofanyika Januari 27, 2025.

Katika kusherehekea tukio hilo, wamachinga hao wametangaza punguzo la asilimia 30 kwa bidhaa zote sokoni hapo.

Mwenyekiti wa soko hilo, Nyamageni Kingamkono, amesema hatua hiyo ni njia ya kumshukuru Rais Samia kwa jitihada zake za kuboresha maisha ya wafanyabiashara wadogo.

Pia soma: Wafanyabiashara Dodoma Wamshukuru Rais Samia kwa Ujenzi wa Machinga Complex

Sherehe hiyo itapambwa na burudani za kipekee kutoka kwa wasanii wa soko hilo, ambapo mfanyabiashara Shehani Edwards amesema kuwa itakuwa ni siku ya pekee kwa taifa.

Wafanyabiashara hao wamesisitiza kuwa hatua hiyo ni ishara ya kutambua mchango wa Rais Samia katika maendeleo ya sekta ya biashara ndogondogo nchini.
 
Badala waombe Kupunguziwa Kodi wanapunguza bei kujipunguzia faida.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…