Dodoma: Madereva watano wa bodaboda wamefariki dunia papo hapo baada ya kugongwa na lori lililofeli breki eneo la Makulu

Dodoma: Madereva watano wa bodaboda wamefariki dunia papo hapo baada ya kugongwa na lori lililofeli breki eneo la Makulu

tonicimmobility

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2025
Posts
493
Reaction score
1,040
Watu watano ambao ni madereva bodaboda wamefariki dunia papo hapo baada ya kugongwa na lori lililofeli breki eneo la Dodoma Makulu jijini Dodoma usiku wa kuamkia leo.

Lori lilikuwa linatokea kwenye barabara inayotokea Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) ambapo lilifeli breki na kwenda kuparamia Kijiwe cha Bodaboda cha Amani kilichopo kando ya barabara hiyo na kusababisha maafa.

Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gallus Hyera amesema tukio hilo limetokea jana Desemba 11, 2025 saa 2:30 usiku ambapo katika ajali hiyo mtu mmoja alijeruhiwa ambaye ni utingo wa lori hilo.

1765528391136.png

Kamanda Hyera amesema athari nyingine iliyosababishwa na ajali hiyo ni uharibifu wa pikipiki za vijana hao pamoja na kuharibiwa kwa ukuta wa uzio wa nyumba iliyokuwa karibu na barabara ambao uligongwa na lori hilo.

Amesema kutokana na eneo hilo kuwa la hatari kwa waendesha vyombo vya moto na watembea kwa miguu Jeshi la Polisi litaimarisha usalama katika eneo hilo.
 
R.I.P Comrades. Mpumzike pema peponi
 
Hawa wajinga wasipochukuliwa hatua wataua watu wengi sana. Huwa nawaona sana njia ya Mji Mwema-Kimbiji Kigamboni.
Yani wanaendesha utafikiri subaru! Wenyewe wanakuambia nyepesi kuendesha
 
Dereva lorry kaua watu makusudi Kilima cha chimwaga sio poa kikali sana(ukipanda tu unaona hali ya hewa imebadilika) so lazima ujiridhishe kama breki zipo sawa........madereva bajaji wanashuka free kutoka chimwaga mpaka makulu center nawaangaliaga tu ujinga wao wa kubana mafuta.
 
Back
Top Bottom